Priscusjt muro
New Member
- Aug 12, 2022
- 1
- 0
Utangulizi
Mawazo ya siasa za ujamaa yalichagizwa Sana na mwana falsafa mashuhuri katika Karne ya 19 aliyeitwa "Karl Marx" lakini katika Karne ya 20 Nchi nyingi duniani ziliipokea siasa ya ujamaa kwa vitendo. Urusi ya kale (USSR) pamoja na jamuhuri ya watu wa china yalikuwa ndio mataifa ya mwanzo kabisa kuitekeleza siasa ya ujamaa kwa vitendo, ingawa kulikuwa na umwagaji damu Sana ila manufaa yake yalidumu hata Leo.
Maana ya siasa za ujamaa
Siasa ya ujamaa ni mfumo wa uongozi wa serikali ambapo maamuzi yote ya uzalishaji na utoaji wa huduma kwa wananchi yapo chini ya serikali. Mali za binafsi hutaifishwa na kuwa za serikali serikali ndio inaongoza mifumo yote ya maisha kwa kuzingatia usawa. Yaani katika ujamaa hakuna mtu kumiliki Mali zaidi ya mwenzake.
Chanzo. Comrade shibitali.C.K.Tumaini.
Ubora wa siasa za ujamaa
1. Ujamaa unaleta maendeleo ya haraka Sana katika taifa. Mfano Urusi ya kale(USSR) na china, baada ya Vladimir Lenin kufanya mapinduzi makubwa Urusi miaka ya 1917 akifanya utaifishaji wa Mali nyingi zikawa za serikali akaanzidha sera ya viwanda, pia alitoa msaada mkubwa katika maendeleo ya teknolojia hivyo Urusi ya kale USSR likawa taifa kubwa kwa muda mfupi pia aliunganisha mataifa mbalimbali ya ulaya mashariki na akatengeneza taifa lilioitwa USSR likawa taifa kubwa sana ulimwenguni na tishio. Lakini pia mwaka 1949 jamuhuri ya watu wa China chini ya Mao Zedong kulifanyika mapinduzi makubwa yaliyojulikana kama ya kikomunisti(Chinese communist revolution).
Baada ya hapo idadi ya watu ilikuwa kubwa mno katika taifa Hilo hivyo sera ya kilimo ilianzishwa ikifahamika kama sera ya kilimo Cha kijani ili kukidhi mahitaji ya watu ya chakula. Pia sera ya viwanda ilibadilishwa na Mao Zedong mwaka 1954. Iliitwa mpango wa miaka mitano wa viwanda ulileta maendeleo makubwa Sana na ya haraka katika taifa la china kwa miaka michache baadae watu walimizana kufanya kazi kwa kufata sera zilizopo hivyo maendeleo yalikuja mapema Sana china. Tofauti na mataifa ya kibepari(kibeberu) ya ulaya na Marekani yalitumia zaidi ya miaka mia na hamsini kufika hapo yalipo Leo. Mfano Marekani ilipata uhuru wake mwaka 1776, lakini mwaka 1945 baada ya vita kuu ya pili ya Dunia ndio Marekani ilipata kuja kuwa taifa lenye uchumi mkubwa na ushawishi Duniani mbele ya uingereza na wakati huo Urusi ya kale USSR nalo likiwa taifa la pili kwa ushawishi dunia nchi zote mbili zilikuwa na siasa tofauti. Chanzo. Norman Lowe na comrade shibitali.C.K.Tumaini
Lakini nchi ya Uchina mwaka 1949 ndio ilifanya mapinduzi ya kijamaa Hadi kufikia mwaka 2000 china moja kati ya mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi Duniani
2. Siasa za ujamaa zinaleta usawa katika taifa na upendo unazidi baina ya watu. Kwa sababu siasa ya ujamaa inasisitiza usawa katika binadamu kwaiyo kwenye taifa la kikomunisti hakuna atakayemzidi mwingine kipato lazima wote mfanye kazi na karibu watu wote muwe na kiwango sawa Cha maisha ndio maana Kuna utaifishaji wa Mali za watu binafsi na Zinakuwa za serikali. Baada ya hapo Mali zote Zinakuwa za taifa kwa sababu zitatumika na kwa watu wengine
Hitimisho na ushauri
Siasa za ujamaa zina fanya watu wengi wanafanya kazi na kunufaika na kazi zao kwa sababu Kuna usawa, huduma za jamii zinatolewa na serikali. Ingawa lazima kuwe na umwagaji damu Sana lakini baada ya hapo Kuna faida nyingi na maendeleo ya haraka. Lakini pia Kuna vita baridi kati ya mataifa ya kibepari na kijamaa. Hivyo kwa Sasa hivi taifa litakalo kubali siasa ya ujamaa litaingia katika mzozo na mataifa ya ulaya na Marekani. Kama tunavyoona kwa Cuba, Korea kaskazini na china. Ni busara kubwa ya viongozi ndio inaweza kutuingiza humo na tukawa salama bila mzozo na mataifa ya ulaya na Marekani.

Upvote
0