Umuhimu wa siku ya kuzaliwa kwa mtoto (birthday)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ingawa ni utaratibu wa Magharibi kusherehekea simu ya kuzaliwa, taratibu nyingi tulizoona zinafaa tuliiga kutoka kwa Wakoloni wetu kuanzia Waarabu na hata Wazungu.

Siku ya kuzaliwa ni muhimu sana kwa mtoto, hii ni sherehe yake yeye binafsi. Tofauti na sikukuu za dini zinazojumuisha jamii. Kuna familia zinazobahatika kuwa na watoto wawili wenye siku moja ya kuzaliwa.

Mtoto kuanzia miaka mitatu anaanza kuhifadhi kumbukumbu, kuanza kuona kisherehe kimeandaliwa kwaajili yake inamjengea imani kuwa na yeye ana thaminiwa.

Watoto wadogo huwa hawajali sana zawadi. Kitu cha muhimu kwao ni chakula, kupendeza, kuimbiwa na kukata keki. Kinachoendelea ni kuachwa acheze na wageni wake. Pilau hasa kama hailiwi kila siku nyumbani na fanta huwamaliza kabisa watoto. Tena soda yenyewe unaweza kugawa chupa moja kwa watoto watatu kama hali ina akili uchumi wa Mwigulu.

Picha ni muhimu pia kwa kumbukumbu. Nime kura a na watoto ambao hawakubahatika kuwa na maisha haya wengine ni kutokana na wazazi kutoelewa umuhimu, au kutolelewa na wazazi wao. Wengi wameamua watoto hawatakosa kitu walichokosa wao wakiwa wadogo.
 
Sisi tulio zaliwa polini huko hayo mambo tumekuja kuyajua town huku lakini wazazi wetu walikua wanatupenda sana tu ..Hata wanangu ujinga huo hawataki kusikia na wanasoma private na kila mara wanasema tumekula keki fulani ilikua happybirthday yake lakini wao hata hawataki wanasema tangu lini msukuma akala happy birthday[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mifuko inatoboka kweri kweri ya mwanangu inakaribia ila nimeshawaambia wafanye sarakasi zote wanazojua sitoi zaidi ya laki 1.
 
Laki moja inatosha sana, anapata nguo, 30,000, mama ana safisha viatu vyake vya Idd au Christmas . Mama ananunua mayai na unga keki simple inapikwa nyumbani na pilau.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Ingawa ni utaratibu wa Magharibi kusherehekea simu ya kuzaliwa, taratibu nyingi tulizoona zinafaa tuliiga kutoka kwa Wakoloni wetu kuanzia Waarabu na hata Wazungu.

Siku ya kuzaliwa ni muhimu sana kwa mtoto, hii ni sherehe yake yeye binafsi. Tofauti na sikukuu za dini zinazojumuisha jamii. Kuna familia zinazobahatika kuwa na watoto wawili wenye siku moja ya kuzaliwa.

Mtoto kuanzia miaka mitatu anaanza kuhifadhi kumbukumbu, kuanza kuona kisherehe kimeandaliwa kwaajili yake inamjengea imani kuwa na yeye ana thaminiwa.

Watoto wadogo huwa hawajali sana zawadi. Kitu cha muhimu kwao ni chakula, kupendeza, kuimbiwa na kukata keki. Kinachoendelea ni kuachwa acheze na wageni wake. Pilau hasa kama hailiwi kila siku nyumbani na fanta huwamaliza kabisa watoto. Tena soda yenyewe unaweza kugawa chupa moja kwa watoto watatu kama hali ina akili uchumi wa Mwigulu.

Picha ni muhimu pia kwa kumbukumbu. Nime kura a na watoto ambao hawakubahatika kuwa na maisha haya wengine ni kutokana na wazazi kutoelewa umuhimu, au kutolelewa na wazazi wao. Wengi wameamua watoto hawatakosa kitu walichokosa wao wakiwa wadogo.
Sijawahi fanya na haitokuja kutokea
 
Back
Top Bottom