Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ingawa ni utaratibu wa Magharibi kusherehekea simu ya kuzaliwa, taratibu nyingi tulizoona zinafaa tuliiga kutoka kwa Wakoloni wetu kuanzia Waarabu na hata Wazungu.
Siku ya kuzaliwa ni muhimu sana kwa mtoto, hii ni sherehe yake yeye binafsi. Tofauti na sikukuu za dini zinazojumuisha jamii. Kuna familia zinazobahatika kuwa na watoto wawili wenye siku moja ya kuzaliwa.
Mtoto kuanzia miaka mitatu anaanza kuhifadhi kumbukumbu, kuanza kuona kisherehe kimeandaliwa kwaajili yake inamjengea imani kuwa na yeye ana thaminiwa.
Watoto wadogo huwa hawajali sana zawadi. Kitu cha muhimu kwao ni chakula, kupendeza, kuimbiwa na kukata keki. Kinachoendelea ni kuachwa acheze na wageni wake. Pilau hasa kama hailiwi kila siku nyumbani na fanta huwamaliza kabisa watoto. Tena soda yenyewe unaweza kugawa chupa moja kwa watoto watatu kama hali ina akili uchumi wa Mwigulu.
Picha ni muhimu pia kwa kumbukumbu. Nime kura a na watoto ambao hawakubahatika kuwa na maisha haya wengine ni kutokana na wazazi kutoelewa umuhimu, au kutolelewa na wazazi wao. Wengi wameamua watoto hawatakosa kitu walichokosa wao wakiwa wadogo.