Kwa nini Tv guard itakuwa bora zaidi wakati hii extension iko sensitive sana.Hebu nisaidie nielewe maana mimi sioni haja ya kutumia hata stabilizer nikiwa na hii extension.
Ni extension nyingi sana zinakuja na surge protections (Zingine hata huwezi kujua lakini zinayo). Sasa surge protector inafanya kazi ya kuzuia umeme unaopanda ghafla (Kama vile wakati radi inapopiga na kuungana na umeme wa Tanesco). Na nilazima umeme upande kwa kasi sana ndipo surge protector itakapofanya kazi yake vyema.
umeme wa Tanzania ni kati ya 220V hadi 240V huo ndio wa kawaida,
>sasa endapo umeme utashuka chini ya 220V , mathalani ukaenda hadi 180V basi kuna vifaa havitaweza kufanya kazi, na
1.Surge protector haiwezi kusaidia chochote hapo, itapitisha umeme huo huo.
2. TV guard/ Fridge guard itazima kabisa kwa muda wa dakika 5 au hadi umeme urudi kwenye hali yake.
3. Starbilizer itaupandisha hadi 220V au zaidi kulingana na ubora wake.
4. UPS itaukataa huo umeme , na itaanza kutumia backup yake ya battery huku ikipiga alarm.
>sasa endapo umeme unachezacheza
1.Surge protector haiwezi kusaidia chochote hapo, itapitisha umeme huo huo.
2. TV guard/ Fridge guard itazima kabisa hadi umeme urudi kwenye hali yake.
3. Starbilizer itakuwa inaurekebisha na kuhakikisha output ipo kwenye range salama kulingana na ubora wake.
4. UPS itajitahidi kuurekebisha, kuukataa na kuukubali huku ikipiga alarm na kunyamaza.
>sasa endapo umeme umepanda kupita 240V , mfano 260V
1.Surge protector baada ya muda itakata umeme au zingine zinakata umeme na kuungua (kulingana na muundo).
2. TV guard/ Fridge guard itazima na kama haina ubora inaweza kuruhusu baadae au inaweza kuungua..
3. Starbilizer itakuwa itajitahidi kuurudisha kwenye range salama kulingana na ubora wake au inaweza kuungua au kukata fuse.
4. UPS itaukataa, itaanza kutumia backup yake huku ikipiga Alarm na inaweza kuunguza surge protector yake na kukata fuse.