Umuhimu wa Tv Guard na Stabilizer katika matumizi ya umeme majumbani

Umuhimu wa Tv Guard na Stabilizer katika matumizi ya umeme majumbani

Ni extension nyingi sana zinakuja na surge protections (Zingine hata huwezi kujua lakini zinayo). Sasa surge protector inafanya kazi ya kuzuia umeme unaopanda ghafla (Kama vile wakati radi inapopiga na kuungana na umeme wa Tanesco). Na nilazima umeme upande kwa kasi sana ndipo surge protector itakapofanya kazi yake vyema.

umeme wa Tanzania ni kati ya 220V hadi 240V huo ndio wa kawaida,

>sasa endapo umeme utashuka chini ya 220V , mathalani ukaenda hadi 180V basi kuna vifaa havitaweza kufanya kazi, na
1.Surge protector haiwezi kusaidia chochote hapo, itapitisha umeme huo huo.
2. TV guard/ Fridge guard itazima kabisa kwa muda wa dakika 5 au hadi umeme urudi kwenye hali yake.
3. Starbilizer itaupandisha hadi 220V au zaidi kulingana na ubora wake.
4. UPS itaukataa huo umeme , na itaanza kutumia backup yake ya battery huku ikipiga alarm.

>sasa endapo umeme unachezacheza
1.Surge protector haiwezi kusaidia chochote hapo, itapitisha umeme huo huo.
2. TV guard/ Fridge guard itazima kabisa hadi umeme urudi kwenye hali yake.
3. Starbilizer itakuwa inaurekebisha na kuhakikisha output ipo kwenye range salama kulingana na ubora wake.
4. UPS itajitahidi kuurekebisha, kuukataa na kuukubali huku ikipiga alarm na kunyamaza.

>sasa endapo umeme umepanda kupita 240V , mfano 260V
1.Surge protector baada ya muda itakata umeme au zingine zinakata umeme na kuungua (kulingana na muundo).
2. TV guard/ Fridge guard itazima na kama haina ubora inaweza kuruhusu baadae au inaweza kuungua..
3. Starbilizer itakuwa itajitahidi kuurudisha kwenye range salama kulingana na ubora wake au inaweza kuungua au kukata fuse.
4. UPS itaukataa, itaanza kutumia backup yake huku ikipiga Alarm na inaweza kuunguza surge protector yake na kukata fuse.
Maelezo yako nimeyaelewa lakini hii extension ina njia 7 za kulinda kifaa cha umeme.Sio kama extensio zile za kawaida.Haina tofauti na Fridge/TV guard na inapatikana kwa bei nafuu.Angalia specifications
WhatsApp Image 2019-01-17 at 18.10.35(1).jpeg
WhatsApp Image 2019-01-17 at 18.10.35.jpeg
zake.
 
Yes unaweza kutumia na itakusaidia na vifuatavyo:
- Surge protection (Umeme mkubwa wa ghafla)
-Umeme unaocheza cheza (Fluctuation)
-Umeme mkubwa uliozidi.

Hasara zake:
-Umeme ukicheza itajizima kwa dakika kadhaa, hapo lazima usubirie tu hata kama unaangalia Taarifa ya habari
-Inachelewa kuwaka unapoiwasha.
-Umeme ukiwa mdogo itajizima.
Point
 
Naongezea hapo. Unaposema watts 1000 hiyo ipo direct na RMS wakati wa convention ya electrical power kuwa Sauti. Na hiyo watts 1000 imegawanyika katika 5.1 channels. Yaani spika sita za system yako ambapo mbilí ni Front Stereo na mbili ni Soround ambazo ni Back na moja ni Center na pia moja ni Ni Passive Woofer.

So unaweza ona kila spika ndogo ina watts 160. Soo ni 160 watts X 5 speakers ambapo utapata 800 Watts na watts 200 Zilizo baki ni za Passive Subwoofer.

Hii ndio njia sahihi ya kupima vifaa uwezo wa vifaa vya mziki kwa kutumia RMS watts. Pia kuna baadhi ya Watu au makampuni hutumia kitu kinaitwa PMPO ambayo sio njia sahihi sana.
Hapo kwenye pmpo tupe somo hesabu zake zinakuaje maana kuna mtu Facebook marketplace anauza home theater singsung hizi za kichina anadai ni watt 4500 kakomaa kinoma iyo sio watt 4500 japo sijui formula yake
 
Natumia TV Guard na Fridge Guard ila nilikuwa sina hii elimu. Uzi wa 2018 lakini bado unaishi bila kupoteza maana.
Hongera sana wadau kwa michango yenu imenipa elimu nzuri.
 
Tv guard na fridge guard ni tofauti?
Pitia comments hapo juu kuna mdau kaeleza vizuri sana kuhusu utofauti kati ya TV Guard na Fridge Guard.
Kwa kifupi tu ameeleza utafauti upo kwenye uwezo (watts) kwa maana kuwa TV Guard ina watt chache ukilinganisha na TV Guard.
Kwa upande wangu kila kimoja kinatumika kivyake maana TV na Fridge havikai karibu. TV iko sebuleni wakati Fridge ipo jiloni. Hivyo kila kimoja kinatumia relevant Guard.
 
Wandungu Tv yangu ime ungua baada ya kupigwa shot haiwaki. Aina ni sony inch 32 kabla sija peleka kwa fundi na kutumia gharama kunaa alie wahi tokea na tatizo kama hili na Tv ika tengenezwa kwa gharama isio zidi 100k
 
stabilizer hupandisha umeme ukipungua, au kuupunguza ukizidi.

umeme unakua level mida ya asubui na mchana, na hushuka (undervoltage/brownout) pale watumiaji wanapoongezeka , mida ya jioni na usiku.

umeme huweza kupanda (over voltage) mda wowote ule, system za tanesiko zikicheza

stabilizer haina nguvu ya kutosha kulinda chombo dhidi ya surge/spikes

surge ni umeme kupanda ghafla :

a. radi ikitokea (inline surges),

b. umeme umerudi baada ya kukatika , (power back surges)

c. kuwaka na kuzima kwa 'inductive loads' mf: friji, friza, ac ) (inline surges).

-lile friji (compressor-motor) lako linapowaka na kuzima umeme unacheza vibaya mno (voltage sags and swells ) .

hapa ndipo tv guard/fridge guard inapokua na manufaa kwani hulinda chombo dhidi ya surge(spikes),

a. inline surges ( sababu ni friji na radi )

b. power back surges (umeme kurudi mkubwa ghafla hudumu sekunde chache sana )

funga stabilizer kwenye vifaa vya electrical kama friji, friza,

funga guard kwenye vifaa vya electronics kama tv, radio,

Cons: Izi guard hujizima pindi kunapokua na over/under-voltage (badala ya kui adjust)

vifaa kama desktop pc , ivi hasa inaitaji UPS ( ambayo ina stabilizer pamoja na surge arrestor ambazo zote ziko effective )
Brilliant explanation man
 
Hivi tv guard inaweza linda pia fridge naona imekua specify as tv guard what about fridge guard
 
Back
Top Bottom