BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
UMUHIMU WA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020.
Maaskofu katika DR Congo walitoa mchango mkubwa sana katika kuifanya ya DRC kuwa na utulivu kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu. Ushiriki wao katika kuyaunganisha makundi au vyama ndani ya DRC hauwezi kusahaulika. Maaskofu wa Malawi nao walitoa mchango mkubwa sana katika kuiingiza Malawi katika ramani ya Kidemokrasia na kulijengea misingi imara ya kidemokrasia taifa hilo mwanzoni mwa miaka ya 90.
Mazingira ya Tanzania ni tofauti kidogo na mazingira ya nchi tajwa hapo juu. Hata hivyo, hii haiondoi nafasi ya viongozi wa dini walioko Tanzania katika kushauri na kujenga mshikamano na utulivu ndani ya nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Moja ya njia ya kujenga utulivu na mshikamano huo ni pamoja na Vyama vya Siasa kuunda Umoja utakaowezesha kusimamisha mgombea mmoja anayekubalika katika baadhi ya maeneo au nafasi. Ushirikiano huo wa kuachiana nafasi na maeneo utaondoa hatari ya kuwagawa zaidi watu. Umoja huo utaonekana zaidi baadaye hata ndani ya Bunge na Mabaraza ya Madiwani kwa vyama vilivyoshirikiana. Hii itavipa heshima zaidi vyombo hivyo hapo baadaye. Kuunda Ushirikiano katika Uchaguzi sio tu kwa vyama vya upinzani, bali inafaa hata kwa chama tawala kutafuta washirika wengine kutoka upinzani ili kuimarisha nguvu na ushawishi kama ANC inavyofanya kule Afrika Kusini.
Hivyo, sisi tunavishauri vyama vya siasa pamoja na watia nia wao kufikiria kwa kina na bila ubinafsi uwezekano wa kuungana na kumuunga mkono mgombea mmoja anayekubalika zaidi katika eneo au ngazi husika. Sisi tunaona umuhimu wa vyama vyote na wagombea wao kuweka pembeni ubinafsi na kuangalia maslahi mapana ya watu na nchi kwa ujumla.
Ni heri kwa chama na mgombea kupata nusu ya matarajio kupitia muungano wa ushirikiano kuliko kukosa kila kitu kupitia ubinafsi. Faida kubwa ya muungano wa ushirikiano ni kuwa kukitokea tatizo ni rahisi kushughulika na taasisi chache lakini imara zilizo katika umoja kuliko kushughulika na taasisi nyingi zilizo dhaifu katika utengano wao!
Sisi tunautuma ujumbe huu kwa viongozi wote wa vyama vya siasa pamoja na watia nia wao katika ngazi zote na maeneo mbalimbali kuutafakari kwa kina ushauri huu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki