UN: Kila baada ya sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali za barabarani

UN: Kila baada ya sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali za barabarani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kila sekunde 24 mtu mmoja anakufa kwenye ajali ya barabarani! Ndivyo ulivyoanza ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika maadhimisho ya leo ya siku ya kukumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani.

Katibu Mkuu anasema katika kuadhimisha siku hii ni wakati wa kutafakari juu ya vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani.

Mtu mmoja katika kila sekundi 24 ina maana watu takribani watatu katika dakika moja na jumla ya watu 72 kwa siku nzima ya saa 24.

“Mwaka huu maudhui yanamulika umuhimu wa kupunguza mwendokasi barabarani ili kuzuia vifo na majeraha, hususan miongoni mwa vijana wa kike na wa kiume pindi wanapokuwa ndio kwanza wameanza maisha yao ya utu uzima,”amesema Guterres akiongeza, “pia waenda kwa miguu na watu wenye ulemavu.”

Ajali za barabarani yatajwa kuwa sababu kuu ya vifo vya vijana


Ajali za barabarani yatajwa kuwa sababu kuu ya vifo vya vijana

Guterres anatoa wito kwa kina nchi, kampuni na raia kusaidia juhudi za kitaifa na kimataifa za kuhakikisha barabara zinakuwa salama zaidi hususan kwenye nchi za kipato cha chini na kati ambako zaidi ya asilimia 90 ya vifo vitokanavyo na ajali barabarani hutokea.

Amesihi pia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuridhia mikataba ya kimataifa ya usalama barabarani na kutekeleza mipango kazi yote ya utekelezaji.

Kwa wahisani, ametoa wito waimarishe michango yao ya kifedha na kiufundi kupitia mfuko wa Umoja wa Mataifa wa usalama barabarani.

Katibu Mkuu amesema “tunapotazamia mkutano wa mwaka ujao wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mbinu za kuimraisha usalama barabarani, hebu na tukumbuke kuwa kila mmoja wetu ana jukumu la kufanya ili barabara zetu ziwe salama. Leo na kila siku tuazimie barabara ziwe salama kwa kila mtu kokote aliko.”

Siku ya kukumbuka waliokufa au waliojeruhiwa kutokana na ajali za barabarani inatokana na azimio namba 60/5 tarehe 1 Desemba mwaka 2005 lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, huku mwaka 2020 Umoja wa Mataifa ukitangaza muongo mmoja wa kuimarisha usalama barabarani kuanzia mwaka 2020 hadi 2030.

Chanzo: UN Swahili
 
Mkuu as long as unapumua na una uwezo wa kupost JF nadhani wewe haukuhusu,hii ni kwa wale waliofariki.
Kwa nini waliokufa? Nadhani wangetenga fungu kwa majeruhi ingekuwa poa sana maana wahanga tungepata mgao wetu.

Sasa hao waliokufa wangewaacha tu wamepumzika kwa amani
 
Niligongwa na bodaboda almanusura niondoke duniani ila Mungu amenisaidia japo natembea kwa kuchechemea
Pole sana mkuu. mwenyezi Mungu aendelee kukusimamia upone urejee hali yako ya awali na uendelee na majukumu yako vema!!!
 
2.5×60×24×365= 1,314,000

Watu wengi mno aisee!.
 
acheni ufala !

sasa hv si tungekua tumeshaisha ?

mnajua binadamu mmoja anatumia miaka mingapi mpaka kua mtu mzima ?
 
Back
Top Bottom