UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Tumuombee
 
Mradi wa steiglers gorge ni unnecessary na ecological destructive, hilo halina mjadala.

Tuna gesi ambayo mpaka leo iko under utilised.
Tuna makaa ya mawe, the cheapest source of energy tunayoweza kutumia. Its destructive pia lakini on the good side yako kwenye maeneo ambayo ni remote and not in one of the largest protected reserve site in the world.
Tuna uwezo wakuproduce wind energy in a large quantity, ila mpaka leo hakuna any signs ya kuanzisha mradi huo.
Tuna a long coastline yenye uwezo wakutuwezesha kuproduce energy kupitia tidal waves.
Tuna uwezo wa kupower miji mingi midogo Tanzania kwa kutumia umeme wa jua tu.

Ila vyote hivyo hamna mpango navyo au hamtaki kuvitekeleza in full.

Juzi juzi a few years back serikali imetoka kuiomba UN kufanya boundary change ya selous kwa ajili ya uranium mining ambayo in the end itakuja kuproduce a ton of radioactive waste ambayo ita-affect the game reserve.

Hapo hapo kuna swala la ujangili humo kwenye hiyo reserve, kwenye idadi ya tembo wameshuka toka 60,000+ in 2009 mpaka 10,000+ in 2013. Tumekaa tu, wala hakuna serious effort kukabiliana na hilo.

Tena sasa mnataka mjenge a hydro plant ambayo ita-flood a large area of the reserve na kuharibu the ecosystem ya eneo hilo,just from the construction alone.

Yani sisi ni kuharibu haribu tuu...

Hydro plants zetu nyingi if not all, zimetengenezwa wakati wa mkoloni, hivi mnadhani wangeshindwa kujenga hiyo hydro plant kwenye hiyo reserve. Mnadhani ni wajinga sana mpaka wakaamua kuachana na hiyo idea. Tena walikuwa na uwezo both financially na engineering wise, kwasababu kama waliweza kutekeleza a large project such as reli ya kati, project kama hii isingewashinda.

Muda mwingine tusiwe wabishi, natuangalie impact ya vitu tunavyotaka kufanya.

I agree with you kwenye main contention. Ila tuwe wakweli pia, kukosa umeme wa uhakika na unapopatikana kuwa wa gharama kubwa sana nayo ni changamoto kubwa sana. Altenatives zote unazosema, ni very expensive kama sio kwenye uwekezaji wake basi ni gharama za kimazingira.

And to be honesty, I really hate the idea of Africa being the "Guardian of eco systems etc", wakati wao hawafanyi hivyo. They care a lot about the animals in the wild than the people in Africa.
 
Yah kwani huyajui makampuni yanayoikamua Tanesco kama Ng'ombe amabayo hayajaongezewa mikataba ya kuuzia Tanesco umeme yaliyokua yanalipwa 400m kila sku
Kuna watu wanajitoa ufahamu wa kutetea nchi.
Nafikiri wamenunuliwa.
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Acha ujinga wewe, umeme wa kutumia nguvu za maji ushapitwa na wakati. Tuna gas songosongo, tuna makaa ya mawe liganga, tuna uranium Dodoma, bado tunahangaika na maji? Jamani maamuzi mengine tuwe tunayapinga, sio bendera fuata upepo. Mimi niko upande wa UN full stop.
 
Ni kweli ila pia sio dalili nzuri sana kwa yanayotunyemelea maana inaonekana kana kwamba tunatengwa kiaina kimataifa. Huku UN kule US kwa issue ya ushirikiano na NK. Si busara kusema tu "shikilia hapo hapo"; wao wameshikilia mpini sisi makali. Busara ni kutafuta suluhu sahihi ya namna ya kutoka tuliponasa ili tusonge mbele bila mikwaruzano isiyo ya lazima na "wakubwa". Mwisho wa siku tutaumia sisi tukiendelea kushupaza shingo. Sina hakika kama utanielewa.
Hela zenyewe za mkopo, ngebe zote hizo. Yakowapi ya interchange Ubungo, imegeuka fly over poleni CCM mnaemtegemea mtu mmoja.
 
Yah kwani huyajui makampuni yanayoikamua Tanesco kama Ng'ombe amabayo hayajaongezewa mikataba ya kuuzia Tanesco umeme yaliyokua yanalipwa 400m kila sku
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba ni hayo makampuni ndiyo yapo behind all this?! Btw, kama hoja ni kampuni zinazoikamua TANESCO, mbona hatukuwasikia hao UNESCO au taasisi yoyote ikipinga ujenzi wa bomba la gas ambalo serikali pia ilisema itakuwa ndio mwisho wa uhaba wa umeme?!

In addition, huo mradi wa Stigler ukishakuwa materialized unadhani utajengwa na wanani kama sio makampuni yenye asili ile ile? Mitambo toka nchi zile zile! Vipuri toka pande zile zile! Experts toka kule kule... and so much more!

So, do you really believe hayo makampuni hayautamani huu mradi ufanyike?!

Itoshe tu kusema kwamba Tanzania sio nchi ya kwanza na wala haitakuwa ya mwisho kwa UNESCO ku-criticise miradi iliyokuwa planned kwenye World Heritage Sites kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo! Selous Games Reserve ni moja ya World Heritage Sites ambazo UNESCO wana-finance protection yake!

So long as hizi World Heritage Sites zinakuwa under UNESCO, they will always criticize jambo lolote wanaloona litahatarisha wanachokilinda!

Kimsingi; hawakukatazi kufanya utakacho lakini watapinga kwa sababu ni wajibu wao!

Kama nchi imejitosheleza unaweza kuwavimbia cuz' all they can do ni ku-withdrawal site husika from among world heritage sites!

Kama ni nchi ya kutegemea misaada na external financing; wataenda kukusubiria huko... watafanya lobbying kuhakikisha you get no financing! Hili ndilo lilimfanya JK aufyate kwenye Stigler Gorge kwa sababu alitarajia financing from Brazil!

That said, acheni hizi porojo za eti cjui Dowans mara IPTL! UNESCO wanatimiza wajibu wao!

Na kama hamuwataki; Tanzania inaruhusiwa ku-withdrawal... hata Ronald Reagan, back 1983 aliitoa USA from UNESCO!
 
Acha ujinga wewe, umeme wa kutumia nguvu za maji ushapitwa na wakati. Tuna gas songosongo, tuna makaa ya mawe liganga, tuna uranium Dodoma, bado tunahangaika na maji? Jamani maamuzi mengine tuwe tunayapinga, sio bendera fuata upepo. Mimi niko upande wa UN full stop.
Sibishani na pusi asiyejua tofauti kati ya koroboi na taa ya umeme.
 
It is sad kwa mtu kujikita katika kukubaliana na thinking ya watu wasioitakia mema nchi hii.
To buy the UN view ati kwa vile wanafadhili miradi humu Tanzania, so we should dance to their whims is a radher absurd .
Sijui watanzania tutatoka lini kstika haya mawazo ya. Utegemezi kifikra, kwamba maendeleo yatakuja kwa ufadhili wa mzungu, na si vinginevyo.

So , If UNESCO or any UN affiliate so decides, umeme wa DOWANS, AGGREKO, IPTL, ni sawasawa llakini wa Steigkers Gorge, hapana.
My foot , watanzania tunasafari ndefu kujikomboa kifikra.
 
This is what we call Mental slavery
Free yourself from that...

I love how you are quoting mistari ila hujuwi maana yake kwani ungeelewa maana yake wala usingeweka hiyo mistari ni kwa sababu inakulenga wewe moja kwa moja. Pole though.
 
Mkuu wako wengi nimewaona humu.
Tatizo kubwa ni kama ni viongozi serikalini.
Magufuli ana kazi kubwa kuwabadilisha fikra.
 
I love how you are quoting mistari ila hujuwi maana yake kwani ungeelewa maana yake wala usingeweka hiyo mistari ni kwa sababu inakulenga wewe moja kwa moja. Pole though.
Mkuu wako wengi nimewaona humu.
Tatizo kubwa ni kama ni viongozi serikalini.
Magufuli ana kazi kubwa kuwabadilisha fikra.
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.

Kwa kuwa Mradi huu ni kwa faida yetu sisi watanzania,ifike wakati tusimamie misimamo yetu.
UN imeshindwa kuzuia vita Congo,Siria na vitisho vinavyo endelea kati ya USA na Korea, watuache tutekeleze miradi yetu ya maendeleo.
Ni matumaini ya watanzania kuwa Serikali haitasikiliza hawa watu wa UN kwani adha ya umeme na gharama zinazowakuta wa Tanzania haziwagusi UN
 
It is sad kwa mtu kujikita katika kukubaliana na thinking ya watu wasioitakia mema nchi hii.
To buy the UN view ati kwa vile wanafadhili miradi humu Tanzania, so we should dance to their whims is a radher absurd .
Sijui watanzania tutatoka lini kstika haya mawazo ya. Utegemezi kifikra, kwamba maendeleo yatakuja kwa ufadhili wa mzungu, na si vinginevyo.

So , If UNESCO or any UN affiliate so decides, umeme wa DOWANS, AGGREKO, IPTL, ni sawasawa llakini wa Steigkers Gorge, hapana.
My foot , watanzania tunasafari ndefu kujikomboa kifikra.
Tatizo lenu nyie watu mnajifanya nyinyi ndo Wazalendo sana na ndio wenye uchungu sana na matokeo yake hoja zenu zinatawaliwa zaidi na hisia eti za kuonewa!!

Hivi suala la ku-buy UN View umelitoa wapi?! Kwani UN waliingia na vifaru Tanzania pale UNESCO walipoitaja Selous as a part of the world sites?

Narudia... Selous Game Reserve ni World Heritage Site! Hizi World Heritage Sites zipo duniani kote including US, Germany, UK, Canada and the like! Tena wenzetu, huwa wanafanya hata lobbying ya hali ya juu ili baadhi ya maeneo yao yawe World Heritage Sites ili ku-boost tourism!

So, huko kote WHS zinakuwa UNESCO monitoring ! Therefore, wanachofanya UNESCO hivi sasa ni wajibu wao unless kama hujui majukumu ya UNESCO! Hizo simulizi kuhusu akina Dowans, IPTL cjui nini na nini ni porojo zenu tu!!

Sometimes jaribuni kutumia angalau common sense!

UNESCO ndio wamei-list Selous Game Reserve as a World Heritage Site! Sehemu yoyote inapokuwa listed as a World Heritages Site maana yake inatakiwa kuwa protected!!

Sasa pamoja na yote hayo mnatarajia UNESCO watakaa kimya endapo wanahisi kile wanachokilinda kitakuwa hatarini kupotea?! Na kama watakuwa wanakaa kimya; kuna umuhimu gani basi wa wao kuendelea kuwa na hizo World Heritage Sites?! Yaani unaanzisha child care center to save street children lakini watu wakitaka hao watoto wakafanye u-House Girl majumbani kwao, au kutembeza pipi barabarani; unawaachia tu waondoke nao!! Sasa nini umuhimu wa hiyo child care center?

Btw, hivi umeelewa nilichoandika kuhusu financing part?!

Narudia... UNESCO huwa wana-fund hizi protected sites! Sasa ulitarajia wawe wana-fund but still wakae kimya wanapoona hatari ya wanachogharamia?

Na ndipo nikasema; kimsingi huwa hawakatazi bali huwa wanapinga na huo ni wajibu wao!!

Ndipo nikasema na hapa jitahidi kuelewa!

Kama nchi itatumia domestic financing for project husika (kwenye heritage site); all UNESCO can do is to threaten to delist a particular site na wameshawahi kufanya hivyo Germany!

Lakini kwa nchi inayotegemea external funding, UNESCO wanaweza kufanya lobbying kuhakikisha you don't get financing!

Huo pia, ni wajibu wao!

Hawa UNESCO huwa wanafanya hizi criticism hata kwenye developed world kwahiyo madai kuhusu akina Dowans ni baseless!

Kinachowasaidia developed world ni kwa sababu hawategemei external funding na kwahiyo silaha pekee ya UNESCO inakuwa kutishia delisting ya site husika though pia huwa wanafanya lobbying with world conservationist radicals.

Hizi smart countries zinafahamu umuhimu wa kuwa WHS kwa ajili ya utalii!!

So, wakati mnaendelea na huo uzalendo fake, smart governments wanachofanya ni lobbying ya kubadilisha mipaka ili eneo wanalotaka kufanya project yao liondolewe na kuwa nje ya mipaka ya World Heritage Site!

Na kwa Tanzania hiyo ni muhimu zaidi kwa sababu hatuna uwezo wa ku-finance ile project with domestic sources na matokeo yake tutategemea external financing. Kama UNESCO watakomaa, wanaweza kufanya lobbying kuhakikisha no external financing!

Ushauri kama huo aliwahi kuutoa Tundu Lissu kwamba if you want to deal with people like Acacia, you've to withdrawal first from mikataba inayowalinda!

Kama kawaida yenu; watu mkajifanya ndo mna uchungu sana na akina Lissu ni traitors lakini matokeo yake, "Wazalendo" mnawadai Acacia more than 400 Trillion lakini hamna base ya kufungua madai hata mahakama ya Ilala!

Halafu acheni hizi porojo za "umeme" over UNESCO "interests". Hizo ni porojo za kuficha kushindwa kwa serikali kutatua changamoto ya umeme!! Bomba la gas Mtwara to DSM linatumika chini ya 10% huku nchi ikiwa imegundua more than 50 trillion cubic feet of natural gas lakini mnataka kuaminisha watu kwamba uhaba wa umeme ni kwa sababu UN wanazuia Stigler Gorge project! Yale yale ya kusingizia uhaba wa maji na Mkataba wa Matumizi ya Mto Nile wakati hata Mkoa wa Pwani una uhaba wa maji huku wakiwa na Mto Rufiji ambao haupo kwenye Mkataba wa Matumizi ya Mto Nile!
 
Acha ujinga wewe, umeme wa kutumia nguvu za maji ushapitwa na wakati. Tuna gas songosongo, tuna makaa ya mawe liganga, tuna uranium Dodoma, bado tunahangaika na maji? Jamani maamuzi mengine tuwe tunayapinga, sio bendera fuata upepo. Mimi niko upande wa UN full stop.

HABARI,
"Gullam,
Nakupongeza kwa msimamo wako na kusema wewe uko upande wa UN safi sana ila kama kuna mwingine hayupo upande wa UN yupo upande wa Serikali kama mimi naomba utambue na kuheshimu uamuzi litakuwa ambo jema sana hakuna haja ya kumwambia mtu mjinga.

Unaposema umeme wa nguvu za maji umepitwa na wakati sawa hiyo ni wewe ila kwangu mimi na wengine bado haujapitwa na wakati na ndio umeme wenye bei rahisi kuliko mwingine wowote.

Nakupa mfano mdogo sana Nchi kubwa yenye technologia kama China imejenga Three Gorges Dam bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme duniani lenye uwezo wa kuzalisha MW 22,500 Kama mara 10 uzalishai umeme wa hilo tunalotaka kujenga sisi la Steiglers Gorge,Sasa ukiniambia umepitwa na wakati kwetu sisi bado haujapitwa,Ethiopia wana The Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD)bwawa ambalo limekwisha na wameanza kuaza kujaza maji litakuwa na uwezo kuzalisha MW zaidi ya 5000 Na tayari Nchi za sudan,Kenya zimeshaomba kuuziwa umeme huo kwani ni wa bei rahisi sana.
Unapozungumzia mambo ya Uranium hapo ndugu kwa uchumi wetu sahau mpaka leo africa kusini wanahangaika kuwa na mradi huo,Nigeria wenye uchui mkubwa wa mafuta bado wanahangaika na kuwa na mtambo wa kuzalisha umeme kwa nyuklia kwa Nchi kama yetu ni gharama kubwa sana hatuwezi kuendesha mtambo kama huo,

Makaa ya mawe nakubaliana na we ila Hayaazidi urahisi kama maji,Shida ndugu ya Gas ni moja leo lile bomba la Gas likipasuka Utalazimu kuzimwa mitambo yote mpaka litengenezwe,Leo mtambo wa kupokea ges pale kinyerezi ukiharibika uzalishaji wote unasimama mpaka mtambo upone hicho ndiko kimewatokea mtwara mpaka sasa bado hawana umeme wa uhakika na Gas inatoka kwao.Kisima kikiharibika matatizo ni hayohayo.

Leo maendeleo ya marekani umeme wa maji unamchango mkubwa sana kwenye maendeleo yao Angalia na wanazaidi ya mabwawa 15 makubwa wanayoyategemea mpaka sasa.

Kama ni marekani sasa fikiria Tanzania.

LUMUMBA
 
Nzuri,
Patrice.
Niombe radhi kwanza kwa kutumia neno mjinga, nilikosea kwa kuwa sikulitolea ufafanuzi.
Nashukuru kwa kunipa mtiririko wa mifano hai kabisa, ya nchi zinazotumuia umeme wa maji.
Lakini ukiangalia nature ya hizo nchi zenye hayo mabwawa utakuta ni tofauti kabisa na sisi. Kwanza ukubwa wa nchi zenyewe, utayari, mipango na mikakati yao pamoja na utaalamu. Kwahiyo nafuu ya mradi kama huo kwa China na USA ni tofauti kabisa na nafuu yetu. Sijui kama unanielewa hapo.
Kwanza rasilimali pesa, watu, wataalamu na vifaa vyote wanatengeneza wenyewe, kwahiyo suala la nafuu zitoe hizo nchi.
Ukienda kwa Ethiopia nature yake ni milima na misitu mikubwa inayotunzwa kwa hali ya juu sana, kwa maana hiyo mvua kwao ni suala la lazima na bwawa lile litadumu sana.
Ukija kwetu Tanzania, linapotaka kujengwa hilo bawa hakuna misitu yoyote ya kupandwa, zaidi ya wenyewe kuona hill bonde eti ndio lizibwe ili ilijazwe na maji ya mvua, nakuambia hatujajiandaa na hatutafanikiwa, na ghalama zake zitazidi kuongezeka siku hadi siku.
Hayo mabwawa yanajengwa kwenye miinuko ya zaidi ya 1000 kutoka usawa wa bahari, lakini sio kwenye mabonde yaliyobondeni hapana nakuambia tena kwetu sio kipaumbele, muda utakuja kukuambia.
Mwisho wanataka kujenga ndani ya hifadhi ya wanyama, moja kwa moja itakuwa ni uharibifu wa mazingira.
Tuwe wa kweli tumeshindwa kuendeleza bwawa la Hale, Mtera na Kihansi leo tuje tena na Rufiji?
Jamani kupanga ni kuchagua yetu macho.
 
Back
Top Bottom