UN: Wakenya wasio na uhakika wa kula kuongezeka zaidi ya mara mbili

UN: Wakenya wasio na uhakika wa kula kuongezeka zaidi ya mara mbili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kwamba idadi ya wakenya wasio na uhakika wa chakula na kuhitaji msaada wa haraka wa kibinadamu sasa kuongezeka zaidi ya mara mbili mwaka huu .

Kwa mujibu wa taarifa ya WFP iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi, mwishoni mwa mwaka 2019 kulikuwa na Wakenya milioni 1.3 walioathirikavibaya na ukosefu wa chakula lakini sasa shirika hilo inasema mwezi huu wa Julai idadi inatarajiwa kuongezeka na kufikia kati ya milioni 3 hadi milioni 3.5 wakati familia zitakapoishiwa kabisa chakula msimu wa muambo utakapofikia kilele.

Kwa kusaidia juhudi za serikali ya Kenya ambayo kwa sasa inapambana na janga la corona au COVID-19 WFP “inatoa msaada wa fedha taslim za miezi mitatu kwa watu 279,000 wanaoishi katika makazi yasiyorasmi mjini Nairobi kwa familia ambazo tayari zilikuwa zinahaha kujilisha hata kabla ya janga la corona.”

Akizungumza na waandishi wa Habari kwa njia ya mtandao mjini Geneva msemaji wa WFP Elisabeth Byrs amesema wanazisaidia pia familia zingine 70,500 ambazo kipato chake kimepunguzwa au kimetoweka kutokana na COVID-19 “WFP itatoa shilingi 4,000 za Kenya kila mwezi sawa na dola 40 kupitia utaratibu wa M-pesa kwa kila kaya ambayo inastahili ili kufidia karibu nusu ya gharama za chakula kwa wastani wa familia ya watu wane kulingana na mwongozo wa programu ya serikali ya msaada wa fedha .

Ameongeza kuwa uhakika wa chakula na lishe wa watu hao umesambaratishwa na janga la COVID-19 na kuwafanya watu masikini wa mijini sasa kutumia karibu nusu ya pato lao kwa chakula.

Kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na wizara ya afya ya Kenya, WFP pia itatoa msada wa chakula cha kutibu watoto wa chini ya miaka mitano 16,000 walio na utapiamlo uliopindukia, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha 5,700 na wazee 6,800 ambao wanaishi kwenye makazi duni.

Ili kufanikisha hilo WFP inahitaji dola milioni 33.9 kuhakikisha chakula na lishe sio tu raia wa Nairobi kwenye makazi yasiyorasmi bali kupanua wigo wa msaada kwa maeneo mengine kama Mombasa, Nakuru, Kilifi na Kwale.

Chanzo: UN Swahili
 
Kwa hii taarifa unaweza kuona ni jinsi wakenya walivyo na maisha magumu hasa linapokuja suala la msosi!

Vitu kama hivyo huwezi kuvikuta hapa tz. Jiji la dar kwa mfano ukiwa na elfu moja yani nusu dola mtu unakula na kushiba kabisa.

Nlishangaa sana kuna kajamaa kalileta uzi uko humu eti kanasema tz ina makazi duni na umasikini wa kutisha, alafu analeta picha za sehemu zenye huduma zote muhimu kama maji na umeme eti reference ya hoja yake.

Ukisoma hiyo habari ya UN hata kama hujawahi kufika Nairobi unapata picha ni jinsi gani maisha yalivyo magumu.
 
Sioni hata sababu inayoifanya Kenya kuwa inauchumi wa Kati maana chakula hawana, bajeti %kubwa deni , sasa huo uchumi mkubwa unatumika sehemu gani.
corruption na sehemu kubwa ya uchumi wa kenya umeshikiliwa na walio wachache na faida inayopatikana inaenda kujenga nje, kunyaland wenyewe ni watumwa kwenye miradi mikubwa. Huoni wakenya wanavyofurahi wakiajiriwa TANZANIA?
 
Chanzo cha Njaa Kenya ni Sera Mbovu ya Ardhi. Poor Land Policy.
Adhi yote imemilikishwa na kuhodhiwa na watu binafsi.
Jambo hili linamfanya maskini kuwa maskini zaidi kila kukicha.
Sera ya Tanzania, Ardhi ni Mali ya Serikali, na Mwananchi anakodishwa tu, au kupewa bure au kunua kwa mda maalum.
Jambo hili lina mwezesha Kila Mtanzani kuwa na Ardhi ya kulima chakula.
Nawapa pole jamaa zangu wa Kenya.
Ni fulsa kwa nchi jirani kufanya Biashara ya mazao ya chakula kwa hawa jamaa zetu.
 
Wanakuambia GDP kubwa
Ushuzi mtupu!!
Kinachowadanganya zaidi wakenya thaman yao ya shilingi , wanasahau hiyo thamani haisaidii katika malipo au kulipwa mshahara unaokidhi mahitaji .mfano kazi utakayoifanya Kenya ukalipwa Kwa pesa ya Kenya na ukaifanya kazi hiyo hiyo Tanzania ukalipwa Kwa pesa ya Tanzania ukija kuichenji kua pesa ya kenya unaweza kukuta aliefanya kazi Tanzania kalipwa vizur au ikawa sawa sawa sasa dhaman ya pesa inamsaidia nini mwananchi wa kawaida? . Nandio maana wakenya wanashangilia thamani ya pesa yao huku wachezaji wenye viwango wanakuja kuchezea mpira TZ lakini pia kenya haiwezi kumchukua mchezaji wa mpira mwenye kiwango kutoka Tanzania sasa watabaki tu kujifariji ela za madafu ila zina nguvu kuliko pesa zao .
 
Sasa hii ndio inanipa picha kwanini wanawake wa kunyacountry wanapenda kuolewa huku, wengine wanawalilia hata wasanii wa Tz.

Kuweni wakweli ombeni chakula Tz vitu vinaozea mashambani na kulisha nguruwe si bora kula hata makombo ya Tz?
 
Back
Top Bottom