Hakuna tofauti. Point yako ni gani? Hivi wewe hujui kuwa msemo wa pesa yenu kuwa madafu ni ligi hapa Jf? Huo ni mchezo tu wa kutaniana bali sio jambo la wewe kunifunza mambo ya uchumi. Mimi ninafahamu kuwa hamna tofauti ya malipo ikiwa mtu analipwa ksh 25,000 au Tsh 500,000. Pia ikiwa bei ya bidhaa TZ ni nafuu kushinda Kenya basi anayelipwa Tsh 500,000 ndiye anayeweza kununua bidhaa nyingi kushinda anayelipwa ksh 25,000. Bei ya bidhaa pia inachangia uwezo wa wananchi kusurvive katika uchumi fulani. Uchumi kama wenu ambapo bei ya bidhaa ni nafuu kushinda Kenya basi mwalimu wenu, hata kama analipwa pesa sawa na mwalimu wa Kenya, ana uwezo wa kununua bidhaa nyingi zaidi kwa sababu ya bei kuwa nafuu. Haya ni mambo rahisi kwangu lakini sitawacha kutania pesa yenu eti kwa sababu umekasirika