Una Degree na unafanya kazi ambayo ungeweza kuifanya hata kama ungeishia darasa la saba

Kuna mwamba maeneo fulani asubuhi unamkuta amekaa kwenye kigoda pembeni ana jiko la mkaa anachoma vitumbua nikasema hii vita ni ngumu sana na mwamba sidhani kama sio graduate[emoji23][emoji23].
Ndo hivyo maisha ni mapambano
 
😂😂😂😂🙌🏾
 
Hahahahaha daaah
 
Kuna wakati maisha yanakuwa magumu unaamua kuweka qualifications pembeni na kuangalia namna ya kusurvive.

By the way, hakukuambia kama alijiunga na usalama wa Taifa na hapo yupo kazini?
😂😂😂😂 ukiwaambia watu una degree alaf unauza machungwa wataanza kuzusha kwamba wewe ni usalama na hupo hapo kuwachunguza.
 
Kuna mwamba maeneo fulani asubuhi unamkuta amekaa kwenye kigoda pembeni ana jiko la mkaa anachoma vitumbua nikasema hii vita ni ngumu sana na mwamba sidhani kama sio graduate[emoji23][emoji23].
Hahaha hii vita ni ngumu kaka
 
🙌🏾🙌🏾
 
Very true mkuu🙌🏾
 
hii ni 50/50 unaweza ukawa vizuri kwa kazi/fani zaid ya moja na inawezekaa sana(mifano hai ipo we angalia ktk jamii uliyomo)
kwahiyo usihitimishe hivo,labda mpaka umpime kwanza
 
Hiyo still sio justification ya jamii na taifa Kwa ujumla kutopambana na kuondoa tatizo chronic la unemployment tulilo nalo , msiongee vitu vizito kama hivi Kwa kutoa points petty kama hizi. Watu hawawezi kuishi kama wanacheza kamali , eti unataifa la watu milioni 60 almost a half of it ni vijana tena wengi wenye elimu kubwa na qualifications za kufanya decent jobs ambazo zinaweza kucontribute kwenye growth ya economy , eti wawe wabeba miZigo na kazi nyingibe za kipuuzi , Acha upuuzi na unafiki

Ni Nani Kati yenu hapa Yuko radhi kumuona mtoto wake au yeye mwenyewe akifanya hizo shughuli za kipuuzi ? , Unless labda kama hamjawahi kupitia hii dhahama ya unemployment .
 
Acha kukurupuka nani kasema kuna justification hapo. Hapo inaonesha tu kama uko vizuri hata ukiamua kuanza chini utafika unapostahili.
 
Hii comment niitengenezee Frem
 
Kuna Jamaa yangu anajiita Injinia, nasema anajiita kwa sababu hata Shule ya Msingi inasemekana aliishia njiani..Lakini Jamaa ni Mtu wa site anapiga kazi yupo busy mbaya.

Jamaa umahiri wake ni wa kutoa hesabu za haraka tu, yaani atakwambia Mchanga tatu, Moram moja, tofali elfu na mia tano tiles box 25 ni milioni tatu laki saba na hamsini...na hata ukipiga kw Calculator unapata hesabu hiyo...zaidi ya hapo ni tia maji...akikuandikia orodha ya Material ni mpaka umtafute mwenyewe akusomee, maana utakuta mahali ameandika hujui kama amemaanisha tyre au tiles.

Jamaa yupo njema, kafungua Hardware, ana Mijengo kadhaa familia bora...mara ya mwisho nimewasiliana nae ameomba nikisikia Noa nzuri inauzwa nimshtue imsaidie kazi zake maana Gari aliyona ni ndogo akiweka mashine ya tarazo inaelemewa.

Sasa ndio hivyoMaisha yalivyo, wenye degree zao wapo jikoni.
 
Hakuna ajuaje kesho yake, maisha ni gwaride
 
Wakati wewe unasugua bench mwengine baada ya kumaliza la saba yeye anajifunza kuhesabu pesa. Miaka 20 mkikutana yeye anauzoefu wa pesa wewe hata hesabu ujui
 
K A
Kwa viongozi hawa tusitegemee,labda tununue management ya kutuongoza toka nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…