Una Degree na unafanya kazi ambayo ungeweza kuifanya hata kama ungeishia darasa la saba

Una Degree na unafanya kazi ambayo ungeweza kuifanya hata kama ungeishia darasa la saba

Hii nchi pamoja na mama samia anasema anaifungua ila angeruhusu vijana waende nje ya nchi kutafuta fursa za ajira bila hvyo hatuwezi kutoboa kwa kweli.
 
Hii nchi pamoja na mama samia anasema anaifungua ila angeruhusu vijana waende nje ya nchi kutafuta fursa za ajira bila hvyo hatuwezi kutoboa kwa kweli.
Hakuna siku serikali itafanya hivyo,

Hili ni jukumu la kijana mwnyewe anyejitambua atoke kwenda kuangalia fursa nje ya nchi... walioshtuka wametoka wengine bado wanapambana na nyomi la usaili ,unakuta wanatakiwa watu 50 wana apply 6,000 na kila mwaka idadi inaendelea kuongezeka ya wahitimu ma jobless mtaani , so ni either wajiajiri or wasepe
 
We acha tu! Mie ningezaliwa Ulaya, sasa hivi ningekuwa dereva wa magari ya formula one. Ningekuwa na pesa nyingi sana at this age...
 
Hakuna siku serikali itafanya hivyo,

Hili ni jukumu la kijana mwnyewe anyejitambua atoke kwenda kuangalia fursa nje ya nchi... walioshtuka wametoka wengine bado wanapambana na nyomi la usaili ,unakuta wanatakiwa watu 50 wana apply 6,000 na kila mwaka idadi inaendelea kuongezeka ya wahitimu ma jobless mtaani , so ni either wajiajiri or wasepe
Ngoja waanze kujiajiri Kwa kuwa criminals na waunde organised crime cartels za scammers , drug traffickers , human traffickers , robbery , extortion NK tuone kama patakalika hapa , unajua siku zote akili za mtu mweusi huwa zinamhingia pale anapoanza kufeel maumivu directly , soon hii nchi haitakalika kama unavyoona nchi za Nigeria , Mexico NK huko , scammers na criminals every where . Panya road wamewanyoosha Tu wiki hapa mnajamba jamba ngoja toughened criminals ambao hawana cha kupoteza waanze kuoperate mtaona effects zake .

Passport zenyewe Tu za kufmsafiria kutoa wapuuzi wanaona ni kama wamekupa mabilioni .
 
Mkuu vipi maslahi ambayo ameyapata kutokana na hiyo kaz? Mlijadili hayo...
 
Kazi ni kazi
Wakuu kwema!

Huyu Rafiki wa zamani tulipotezana miaka mingi kidogo, enzi za chuo chuo miaka ile mwamba akisomea moja ya fani ya Engineering pale DIT. Miaka hiyo tukiongelea future jamaa alikuwa akijiweka katika nafasi kama tisa hivi za juu za nchi vile akiamini uinjinia utakapo mweka.

Juzi nipo chimbo moja hapa mjini, namkuta yeye ndio mpishi mkuu wa eneo hilo, akiwauzia watu supu na vyakula vingine, kavaa nguo zile za ki chef, nilishtuka ila sikujisikia vibaya maana pesa inatafutwa bwana! Ikabidi tuzungumze na nijue what happened? Chief Engineer imekuwaje kuaje mpaka uwe chef cooker?

Mwamba alistuka lakini akawa mkweli tu mzee na vile tumeshakuwa watu wazima, akasema ni mchakato tu wa maisha, ila aka kazia 'anachosikitika kitu alichokisomea hajawahi kukifanyia kazi, miaka minne yote aliyosomea uinjinia imepotea bure tu na sasa anafanya kazi ambayo hata kama angeishia darasa la saba angeifanya tu'.

Anasema, maisha yalikuwa magumu kweli kweli, kazi hakuna so akaomba kazi ya u dj bar flan sababu alikuwa anapenda sana muziki. Baadaye kwenye u dj kukawa kugumu basi akaona kuna bar imeanzishwa maeneo jirani yake akaomba kazi pale wakampa chaka la jiko, na amekuwa akihama toka bar flan kwenda nyingine na sasa ndo kabobea hapo kwenye karia ya majiko.

Maswali ya kujiuliza, hivi watu hua wanazingatia kweli muda walioupoteza kwenye masomo yao? Kweli hustles zile zimeenda bure? Wanazingatia mamilioni waliyoyalipa vyuoni kwa ajili ya icho walichokuwa wanakisomea? au shida ni kwamba watu wengi walienda kusomea vitu ambavyo sio kusudi lao ambalo Mungu aliliweka ndani yao so degree zao zinakua ni gabage?

Watoto wetu tunawaandaa vp na tunawaambia vipi kwamba baba ako mimi usinione ni chef mimi nina degree ya uinjinia. So hatuwezi kuwa ving'ang'anizi kwenye vile tulivyovisomea kwa miaka mingi na kulipia fedha nyingi?
Kazi ni kazi mradi tu:
1. Mwenye uipende na kuenjoy
2. Iwe halali
3. Inakufikisha pale unapopataka(rejea namba moja)
 
Huyo jamaa hata simshangai,tuna wasomi kibao wazoefu lakini wamekimbilia kwenye siasa,akina Prof.Muhongo na Taaluma zao wapo kwenye siasa.Sasa kama jamaa kaamua kufanya kazi hiyo sawa tu.Kuna Injinia anamiliki duka la vipodozi,watu wake wa karibu walimwambia aachane na fani hiyo aingie kwenye biashara.Siku walipompeleka Dubai,fani ya Uinjinia akaiweka pembeni.
Serikali inapaswa kulegeza sheria za kupata passport na kuwaombea fursa vijana kwa nchi kama Malawi,Sudan Kusini,Burundi ili vijana wakafanye kazi huko.Hivi hatuoni jinsi viongozi wa kutoka mataifa kama Uturuki,China,Morocco wanavyokuja kuwaombea fursa watu wao.
 
Hiyo still sio justification ya jamii na taifa Kwa ujumla kutopambana na kuondoa tatizo chronic la unemployment tulilo nalo , msiongee vitu vizito kama hivi Kwa kutoa points petty kama hizi. Watu hawawezi kuishi kama wanacheza kamali , eti unataifa la watu milioni 60 almost a half of it ni vijana tena wengi wenye elimu kubwa na qualifications za kufanya decent jobs ambazo zinaweza kucontribute kwenye growth ya economy , eti wawe wabeba miZigo na kazi nyingibe za kipuuzi , Acha upuuzi na unafiki

Ni Nani Kati yenu hapa Yuko radhi kumuona mtoto wake au yeye mwenyewe akifanya hizo shughuli za kipuuzi ? , Unless labda kama hamjawahi kupitia hii dhahama ya unemployment .
Poin
 
Kwa hatua tuliyofikia sometimes mashuleni/vyuoni tunapiga Mark time tu watu wakue waingie kwenye michakato ya maisha pasipo kuzingatia sana walichokisomea. Ukisubiria kupata post ya ulichosomea utajikuta umezeeka na bahasha mkononi
 
Back
Top Bottom