Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

sababu kubwa shule za Dar kufanya vibaya mfano zilizopo maeneo ya Temeke, kuna Msimbazi wanavaa blue bahari, kuna chanika na nyingine ipo bunju ni ya kata.

1. Utandawazi; hii ni sababu moja kubwa ya watoto wengi wa dar kufeli. Hili linasababishwa na usimamizi mbovu wa wazazi kwa watoto wao wakiwa busy kukimbizana na maisha, watoto kuingia kwenye starehe za mapema, kuangalia video za ngono.

2. Serikali; maisha ya dar ni magumu, kada hii ya ualimu imesahaulika, miundombinu Mibovu, hakuna Hamasa kwa kwa walimu kufanya kazi kwa asilimia zote wanafanya bora liende.

Nimeona mtaala mpya mambo mengi sana, lakini kama serikali haitajitahidi kuboresha maisha na masilahi ya walimu hatutaona mabadiliko.

Wizara husika waliangalie hili suala kwa kina, usitegemee ukafanya vitu kwa njia ile ile ukategemea matokeo tofauti.
Hili neno maslahi ya walimu ni kichaka kikubwa cha wanasiasa na walimu wapumbavu kujifichia.
Kipindi mwalimu analipwa laki sita kwa mwezi na kuiona ndogo kuna sisi wazazi ambao hatuna ajira wala biashara ya kutuingizia hata alfu kumi kwa kutwa.
Mwalimu ana mshahara pia ana access yakupata mikopo vitu ambavyo wazazi wengi hawana.
Kingine ukipewa kazi ifanye kwa uaminifu km haikufai achana nayo kuliko kufanya kitu chini ya kiwango.
Ninachojua mimi walimu wengi ni vilaza.
Wamepewa majukumu yakufundisha vitu ambavyo hata wao hawaviwezi.
Km mnataka kuamini hili siku itokee mpe mwalimu mtihani uleule anaowapa wanafunzi afanye pamoja na wanafunzi wake, hapo ndipo utaona vioja.
 
Kuna mtu alisema matokeo ya kidato cha nne yakitoka tuyaweke, hayo hapo.
Screenshot_20240125-130305_1.jpg
 
Back
Top Bottom