Una ushauri gani kwa Binti anayeanza maisha mapya mjini?

Una ushauri gani kwa Binti anayeanza maisha mapya mjini?

Cha kukwambia ni kwamba, unakwenda kukumbana na changamoto ambazo hutaweza kuzikataa kwa akili ya kawaida.
 
1. Kama hana support system kutoka kwenye familia, maendeleo ataanza kuyaona kwenye miaka 27/28. Kama hatokuwa na tamaa hatatumika vibaya na ME.

2.Kama anatamaa ajue kuwa atatumika sana hivyo na yeye ajue kuwatumia to her advantage. (kama ana akili lakini) note; wanaume si wajinga, wana udhaifu tu.

3.Kazi yake ina age limit, hivyo afanye asave aanzishe hata side hustle.

4.Aombe Mungu na atumie akili katika mahusiano kama anapenda/wish kuolewa mapema. Kama hatopenda kuolewa in her 20’s ajitunze sana.. Ataolewa siku akitaka (it takes courage, akili, exposure na favors from God tho, na si kila mtu ataipata hiyo favor)

5.Akiamua kuzaa kabla ya kuolewa akumbuke mtoto ni wa mama unless kwa wenye bahati mtoto ni wa baba na mama.

6. Sio lazima kufanya kila dhambi, dhambi zingine zinaharibu roho na kukupeleka down moja kwa moja, Achague dhambi kwa uangalifu..Aepuke peer-pressure na maneno ya vijiweni [emoji3]

7.Asisahau sadaka na wazazi kama anao, ufunguo wa mengi uko hapa.

Kila la heri.
[emoji625][emoji625]

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Hilo swali lako haliwezi kuwa na jibu la moja kwa moja. vinginevo utadanganywa tu apa.

inategemea wew mwenyewe upo kundi gani maana kuna mwanamke wa,
●sura nzuri/shepu nzuri
●sura nzuri/shepu mbovu
●sura mbovu/shepu mbovu
●sura mbovu/shepu kinanda
●sura kawaida/shepu kawaida
●sura kawaida/shepu kinanda
●sura kinanda/shepu kawaida

sasa hao wote ni watu tofauti kabisa na changamoto zao hazifanani. kila kundi lina changamoto zake na jinsi yake ya kuzikabili. sasa labda useme apa unavojiona wewe upo kundi gani apo?
 
Mambo ya muhimu kwa binti wa kike ambae anaenda kuwa waitress
1. Tumia uzazi wa mpango wa muda mrefu either miaka 2 au 3, hakikisha kwa vyovyote vile hupati mimba wala kuzalishwa hata kama jamaa kasema anakupenda anataka kukuoa
Mwambie akajitambulishe kwenu akuoe ndipo umzalie

2. Hela ni tamu ila hakikisha, hufanyi mapenzi kinyume na maumbile hata akikuahidi utakuwa raisi au mbunge wa viti maalumu.
3. Tumia kondomu, muhimu sana hii usimuamini mtu kwa kumuangalia au uwe na vipimo mpimane na mwenzio kabla ya kushiriki tendo
4. Jiwekee akiba na malengo siku zote
5. Usije kujihusisha na uvutaji shish, banging au Aina yoyote ile ya madawa ya kulevya maana kwenye shish ndimo wanachanganyia
6. Jitunze, jipende, jua hiyo ni njia tu ya kufikia malengo yako. Usijikatie tamaa bado unaweza pata mwanaume mwema huko huko baa au club na akakuoa
7. Usije jaribu kuchora tattoo hata kwa bahati mbaya ni heri uonekane mshamba
8. Acha mashindano na wahudumu wenzako kwamba wakinunua iPhone basi na wewe lazima uwe nayo. Ku
mbuka ulikotoka.
Baki na ushamba kidogo itakusaidia sana
 
Awena bwana mwendesha boda boda, na muuza chipsi. maisha atayapatia
 
Back
Top Bottom