Una ushauri gani kwa kijana wa kiume aliyopo umri wa 18-29.

Una ushauri gani kwa kijana wa kiume aliyopo umri wa 18-29.

Umenikumbusha kuna siku mdogo angu rubii aliandika jf unaweza kutukanwa na mtu hata kitanda....nilichekaaa sisahau.

Muda ndo huu kijana, panga, amka, tekeleza..... Maana yake ukipanga jambo amka muda huo fanya, epuka sana nita....nita...nita zinachekewesha hizi.
Mkuu hata kama nina maisha magumu ila siwezi kukosa kitanda🤣🤣 nachangamsha genge tuu. Uko wapi kwanza?
 
1. Kuwa mbahili. Soma vitabu vingi. Fanya biashara au jiongeze kielimu.

2. Wanawake na pombe humaliza fedha sana. Kuwa na manzi mmoja anayeweza kujihudumia walau kidogo. Usijipe mzigo kulea girlfriend wako kwa kila kitu.

3. Usijipe umuhimu sana kwa watu.
Watu wameishi bila msaada wako kwa miaka na miaka na hizo shida zao, hivyo wewe huwezi kuzimaliza zote na hata bila msaada wako wataendelea kudunda tu. So, msaada uwe wa kadri tu. Yaani kuwa mchoyo wa jasho lako.

4. Usipumbazwe na mambo ya dini, yakakupotezea muda na fedha.
Kusali hakuongezi chochote maishani mwako. Kutokusali pia hakuongezi chochote. Jitihada zako, ujuzi na maarifa ndivyo vitakavyokufaa maishani.
 
Mimi sijafika 30+

Ila naweza kushare some hints to be considered.

At the age of 29+ jitahidi uwe Unapambania sana kujenga familia na sio relatives

Nikisema familia namaanisha familia yako wale watu ambao unashirikiana nao kutafuta MAISHA na kusaidiana katika hili na lile..

Ndugu yako anaweza kuwa sio familia yako Ila rafiki anaweza kuwa familia yako.

Hivyo at the age of 29 make sure you build a family and not relative .

Network jaribu Kuwa na network katika kila sehemu uliyopo - iwe chuoni , iwe kazini , iwe nyumbani.

Connection - kuwa na connection mbalimbali na watu ambao wamekuzidi kila kitu na ambao umewazidi kila kitu. Connection huwa inasaidia Ku -achieve dreams zako kirahisi.

Kuheshimu watu - hasa watu usiowafahamu kuanzia mitandaoni jiepushe na kuwa na personal attack mfano kutukana wanawake au wanaume. That is hell.

GOD /universe at the age of 29 make sure unaelewa kuwa ipo nguvu inayoendesha haya maisha you need to connect ur self with ur higher power either GOD /universe.

Give back - unabidi kutambua kuwa katika kipato chako kuna riziki za watu so usiwe mchoyo katika kutoa.

Kujipenda
Penda watu
Hekima
 
Katika umri wa miaka 30 ndipo maisha ya mwanaume yanaanza kujibu au kuonyesha muelekeo. Hapa ndipo huwa tunagundua wapi tulikosea wapi tulipatia.

Kwa mabroo, wakina baba na wazee ambao mpo 30+ una ushauri gani kwa madogo sana sana kwenye suala la mahusiano na uchumi.

Mwaga sumu kwenye comments madogo wachukue yanayowafaa.
1. Kijana tafuta mwanamke / mwanaume mkubaliane mzae na kutoa malezi kwa usawa si lazima muowane

2. Kijana wekeza akili na jitihada kubwa ktk kujijenga kiuchumi. Ktk hili uaminifu ni msingi wa yote

3. Acha umalaya uliopitiliza na ktk huo umalaya utakaokuwa nao basi kuwa makini na afya yako kwa kuchukua tahadhari

4. Kumbuka ibada

5. Ongea kidogo, sikiliza zaidi. Mazuri beba, yasiyokuhusu achana nayo

Kwa mwanaume real life begins at 30s
 
Katika umri wa miaka 30 ndipo maisha ya mwanaume yanaanza kujibu au kuonyesha muelekeo. Hapa ndipo huwa tunagundua wapi tulikosea wapi tulipatia.

Kwa mabroo, wakina baba na wazee ambao mpo 30+ una ushauri gani kwa madogo sana sana kwenye suala la mahusiano na uchumi.

Mwaga sumu kwenye comments madogo wachukue yanayowafaa.
Atrombeee mpaka mbru iwe yakijani
 
1. Ahakikishe anamalizana na ishu za shule. Kwa mfano kama kasomea accounts ahakikishe pia CPA anapata kwenye huo umri. Wale wa IT nao wamalizane kabisa na zile professional certificates.
2. Afanye kazi yoyote ya halali kuanzia zile za nyumbani, kanisani/msikitini, na sehemu yoyote atakayohitajika. Asiwe mvivu.
3. Asiwe mwoga kujaribu chochote ili mradi havunji sheria.
4. Atumie sana condom. Asiuze mechi kwa namna yoyote. Hata akisafiri awe na condoms za tahadhari.
5. Huo ndo umri wa kumpata soulmate. Akimpata aoe tu kama anaona kisaikolojia atamudu jukumu la ndoa.
6. Awe na kitambulisho cha NIDA, Leseni ya udereva, na ikiwezekana passport ya kusafiria.
 
Asante sana., vijana wamekusikia
 
Back
Top Bottom