Unaamini katika dini Uislam/Ukristo budha/indu/wayahudi kuwa ukifa wewe sio dini flani hautaingia mbinguni

Unaamini katika dini Uislam/Ukristo budha/indu/wayahudi kuwa ukifa wewe sio dini flani hautaingia mbinguni

**
NAUNGA MKONO HOJA kuwa DINI YA MTU HAIMPELEKI MTU MBINGUNI ILA MATENDO YAKE.


Luka 10:25-42
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Simulizi Kuhusu Msamaria Mwema
25 Kisha mwanasheria mmoja alisimama ili amjaribu Yesu. Akasema, “Mwalimu, ninatakiwa nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26 Yesu akamwambia, “Imeandikwa nini katika torati? Unaielewaje?”

27 Yule mwana sheria akajibu, “‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote.’ Pia ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.’”

28 Yesu akasema, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivi nawe utaupata uzima wa milele.”

29 Lakini mwanasheria alitaka kuonesha kuwa alikuwa mwenye haki na aliishi kwa usahihi. Hivyo akamwuliza Yesu, “Lakini si kila mtu aliye jirani yangu, au unasemaje?”

30 Katika kujibu swali hili, Yesu akasema, “Mtu mmoja alikuwa anasafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akiwa njiani alivamiwa na majambazi, wakamchania nguo na kumpiga. Kisha wakamwacha amelala chini akiwa katika hali ya kufa.

31 Ikatokea kuwa kuhani mmoja alikuwa anasafiri kupitia njia hiyo hiyo. Alipomwona, hakusimama ili amsaidie, alikwenda zake. 32 Kisha Mlawi[a] alipokaribia na kumwona yule mtu, alipita upande mwingine. Hakusimama ili amsaidie, Alikwenda zake.

33 Ndipo Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri kupitia njia ile ile, alipofika mahali ambapo mtu aliyejeruhiwa alikuwa amelala, alipomwona alimhurumia. 34 Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai,[c] kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko. 35 Siku iliyofuata, Msamaria alitoa sarafu mbili za fedha na kumpa mtunza nyumba ya wageni, akamwambia, ‘Mtunze mtu huyu aliyejeruhiwa. Ukitumia pesa nyingi zaidi kwa kumhudumia, nitakulipa nitakapokuja tena.’”

36 Kisha Yesu akasema, “Ni yupi kati ya hawa watu watatu unadhani hakika alikuwa jirani wa yule mtu aliyepigwa na majambazi?”

37 Mwanasheria akajibu, “Ni yule aliyemsaidia.”

Yesu akasema, “Basi nenda ukafanye kama alivyofanya.”
Mungu haangalii dini wakati huo huo unanukuu maandiko ya dini tena yaliyoletwa na dini.

Kamwe huwezi kujitenga na dini kwa kufuata maandiko yanayotokana na dini, ili uwe nje ya dini ni lazima uwe nje ya mfumo mzima wa kidini ikiwa ni pamoja na hayo maandiko ya kijinga kutoka kwa Biblia, Qur'an n.k, lazima uwaze nje ya box.

Je kabla ya hizi dini watu waliishi vipi?, Kama dunia ina mabilioni ya miaka, lkn ktk hizi dini zenu kuu hasa Uislamu na ukristo hakuna inayozidi hata miaka 7,000 je kabla ya kuundwa hizo dini watu waliishije?.

Kitu kingine, Kila dini ina Mungu wake na stories zake zinazotofautiana na Stories za dini nyingine jambo linaloleta utofauti wa imani na kufanya utofauti ambao kamwe hauwezi kuwa sawa.

kwa wanaosema Mungu ni mmoja tofauti ni dini hawa nao ni wajinga, mfano Yehova/elishadai/Elohim huyu ni Mungu wa wayahudi&wakristo ambaye hatambuliki na uislamu, ubudha uhindu na dini zingine, hivyo hakuna Mungu mmoja.

Mungu Krishna anaetambulika ktk uhindu hatambuliki ktk ukristo wala uislamu hivyo hii yote ni Miungu ambayo inatofautiana na dini zingine.

Kila dini inahubiri propaganda zake ili kujizolea wafuasi wa kuwadanganya, hakuna dini iliyosahihi, huwezi kuupata ukweli Ktk hizo dini.

Dini ni mfumo wa kishenzi uliotungwa kudanganya, kupotosha, kuficha, kuleta migogoro, mauwaji, ushirikina na fitna za kila aina.

Dini zote ni TAKATAKA, hakuna ukweli humo mnapoteza muda wenu
 
Yesu anawajua walio wake ni wale wanaoyafanya matendo mema.

maana wafanyao dhambi wote ni wa IBILISI.
KUAMINI tu pekee haitoshi..sio wote wanaoamini Yesu wataingia mbinguni maana hata SHETANI mwenyewe na MAJINI mapepo yote yanamwamini YESU tena KWA KWA KUTETEMEKA.
IMANI PEKE YAKE bila matendo haifai kitu imekufa.
huwezi kumuonyesha mtu imani matendo ndio uthibitisho
Sio wote wanasema YESU Yesu wataingia mbinguni kuna manabii wa uongo pia wanatumia jina la Yesu.

Yakobo 2:17 B
Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

Yak 2:18 S
Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu

Yak 2:19 S
Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Mathayo 7:21
“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mt 7:22
22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Lk 6:46-49
Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

Yn 10:27-30
Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.


Yn 10:16
Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.

AISEE kuna watu wasio kuwa na dini kabisa wana matendo mema sana kuna waislamu wana matendo mema huwa nawaona wanapita asubuhi kusaidia wagonjwa mahispitali kuwapa uji,chakula ,mchana chakula,nguo,kuwavalisha,kusaidia masikini..na kuna
HITIMISHO...ANAYEJUA atakayeingia mbinguni ni nani ni YESU mwenyewe ,na mbingu ni ya kwake ,na yeye anawajua walio wake hata ambao sio wa zizi hili anao watu wengi ambao mimi na wewe hatuwajui NA SIO KAZI YETU SISI KUJUA WANAOENDA MBINGUNI NA WASIOENDA MBINGUNI..sisi tufanye yanayotuhusu.
Sijakuuliza anayeamini bila matendo mazuri nimekuuliza mwenye matendo mazuri lakini hamuamini Yesu.
 
Back
Top Bottom