Unaamini katika dini Uislam/Ukristo budha/indu/wayahudi kuwa ukifa wewe sio dini flani hautaingia mbinguni

Mungu haangalii dini wakati huo huo unanukuu maandiko ya dini tena yaliyoletwa na dini.

Kamwe huwezi kujitenga na dini kwa kufuata maandiko yanayotokana na dini, ili uwe nje ya dini ni lazima uwe nje ya mfumo mzima wa kidini ikiwa ni pamoja na hayo maandiko ya kijinga kutoka kwa Biblia, Qur'an n.k, lazima uwaze nje ya box.

Je kabla ya hizi dini watu waliishi vipi?, Kama dunia ina mabilioni ya miaka, lkn ktk hizi dini zenu kuu hasa Uislamu na ukristo hakuna inayozidi hata miaka 7,000 je kabla ya kuundwa hizo dini watu waliishije?.

Kitu kingine, Kila dini ina Mungu wake na stories zake zinazotofautiana na Stories za dini nyingine jambo linaloleta utofauti wa imani na kufanya utofauti ambao kamwe hauwezi kuwa sawa.

kwa wanaosema Mungu ni mmoja tofauti ni dini hawa nao ni wajinga, mfano Yehova/elishadai/Elohim huyu ni Mungu wa wayahudi&wakristo ambaye hatambuliki na uislamu, ubudha uhindu na dini zingine, hivyo hakuna Mungu mmoja.

Mungu Krishna anaetambulika ktk uhindu hatambuliki ktk ukristo wala uislamu hivyo hii yote ni Miungu ambayo inatofautiana na dini zingine.

Kila dini inahubiri propaganda zake ili kujizolea wafuasi wa kuwadanganya, hakuna dini iliyosahihi, huwezi kuupata ukweli Ktk hizo dini.

Dini ni mfumo wa kishenzi uliotungwa kudanganya, kupotosha, kuficha, kuleta migogoro, mauwaji, ushirikina na fitna za kila aina.

Dini zote ni TAKATAKA, hakuna ukweli humo mnapoteza muda wenu
 
Sijakuuliza anayeamini bila matendo mazuri nimekuuliza mwenye matendo mazuri lakini hamuamini Yesu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…