Unabadilisha simu kila baada ya muda gani? Na vipi vipaumbele vyako unavyobadilisha?

Unabadilisha simu kila baada ya muda gani? Na vipi vipaumbele vyako unavyobadilisha?

Wakuu.
Mimi uwa inachukua miaka miwili au mitatu kubadilisha simu, tukitoa emergency za kupoteza, kuibiwa au kuharibika.

Mara zote nanunua used, uwa natafuta flagship ya miaka miwili iliopita napata kwa bei nzuri.

Uwa naangalia sana camera, then memory, screen sio ishu, rangi ndio kabisaaa kwasababu lazima nivishe kava.
Simu yangu niliyotumia kabla ya hii nilinunua 2018-2025
 
Simu used HAPANA, nanunua simu mpya SAMSUNG duka la SAMSUNG Mlimani City nakaa nayo miaka 2 hadi 3 ndio nanunua tena.
 
Hizi simu mbili hazitifautiani sana aspect nyingi kama kioo, speakers, build quality nk. Redmi Note 13 Pro has slightly better camera though
Lakini utofauti mkubwa upo kwenye chupset ambako Redmi Note 12 Turbo in way better chipset
Kwa hiyo Redmi Note 12 Turbo ni bora zaidi.
5179.png

Kama utaamua kuchukua Redmi note 12 turbo usichukue iliowekewa global rom, hii kesi nilikutana nayo niliitatua kwa kurusdisha Chinese rom.
 
Hata kama haujali screen ila kama unanunua flagship ya miaka 2 iliyopita ni lazima tu upate screen nzuri
Mimi pia huchukua 2-3 years kubadili simu

Vipaumbele, ni processor, kamera, kioo, speakers, iwe inakaa laini mbili (zote ziwe physical, sio eSIM)
Pia iwe kampuni ya Xiaomi
Ninatumia Poco X6 Pro 5g nataka ku-upgrade mwaka huu niende kwenye flagship ila brand ni humuhumu Xiaomi. Ipi ni unyama mkali? Maana nasikia hata POCO F7/8 ni hatari.. navyozingatia kwenye simu ni battery capacity kubwa, speed ya kuchaji, camera na storage, na lazima iwe laini 2.
 
Natumia i phone X niliyonunua Dubai mwezi mmoja baada ya kuzinduliwa na sina mpango wa kubadilisha nimebadili battery mara mbili

Watu wangu wa karibu huwa wananitania na kunicheka ila sijari
 
Ninatumia Poco X6 Pro 5g nataka ku-upgrade mwaka huu niende kwenye flagship ila brand ni humuhumu Xiaomi. Ipi ni unyama mkali? Maana nasikia hata POCO F7/8 ni hatari.. navyozingatia kwenye simu ni battery capacity kubwa, speed ya kuchaji, camera na storage, na lazima iwe laini 2.
Poco F7 hautajutia, huhitaji kubeba charger hatakama nyumbani utarudi saa 6 usiku.
 
Kila wanavyo release iPhone Pro Max yoyote hapo naenda kubadilisha na kutoa pesa kidogo napata tambo jipya yaani kila wiki ya 3 ya mwezi wa 9 nabadilisha
 
Kuna watu hamjui kufanya topup mnapigwa hela ndefu zaidi ni heri utafute mteja mdogo mdogo ndo uongezee hela
 
Mi mtu akfka bei tu imeenda na uzuri wng huwa nanunua cm ninayoipenda siangalii brand hapo toa tecno, redmi, infinix, itel na nduguze wa aina yake sizpendi tu heri nitumie samsung A03 core kuliko hzo. ni mpenz wa aqous now nina r6 natamba nayo, samsung, iphone napendelea bt si mtu wa matumiz makubwa ya pesa kwny kununua cm isizd laki 4 bs.
 
Back
Top Bottom