Unabii: Ajaye ni Mwanaume, iwe anatokea tawala au upinzani

Unabii: Ajaye ni Mwanaume, iwe anatokea tawala au upinzani

Hawa ndio wanaoweza kutuletea mabadiliko ya kweli .

(1) Tundu Lisu .
Ni mzalendo wa kweli asiye na chembe ya kuremba rushwa na Ufisadi katika historia yake yote ya siasa. Hana mambo ya urafiki,ukabila , Udini na uchama zaidi ya kupinga ufisadi.

(2) Wakili Msomi Mwabukusi:
Huyu ni hazina kubwa sana kwa Nchi ya Tanganyika na ni mpango wa Mungu kumleta Mwabukusi katika kati ya giza nene la ufisadi na dhulma na utawala usiojali sheria na katiba ya nchi. Amekua ni faraja kubwa sana kwa Wananchi wa Tanganyika kwa wakati huu . Yaendeleza mambo ya ukabila na Udini zaidi ya kupinga ufisadi na wizi wa rasilimali za umma

(3) Kasimu Majaliwa.
Huyu pia anaweza kutuvusha kwa sababu anajua mbinu zote zafisadi na namna ya kudili nao.Pia hana ubaguzi wa kidini na kikabila.

(4)Januari Makamba.
Makamba, ni mtulivu kwenye kutoa maamuzi na anajua kupanguliwa mikakati yake . Hana jazba katika kutatua changamoto
Yaendeleza mambo ya Udini na ukabila. Japo amechafuliwa sana na mahasimu wake wa siasa.

(5)Mwigulu:
Anasimamia kile anachokiamini .
Ana ka hulka ka udikteta.
Huyo mara Ubelgiji rmaa wanae ni wamarekani wa Nini.
 
Huyo mara Ubelgiji rmaa wanae ni wamarekani wa Nini.


Hakuenda huko kutembea .
Alikua anapigania uhai wake kama watu waliofukiwa kule Kariakoo.

Isiombe kukutwa na janga linalotaka kutoa roho yako uiache familia yako ambayo bado inakutegemea.
Mbaya zaidi wanataka kukuua ukiwa unatekeleza majukumu yako ya kikatiba.

Lisu ni mzalendo sana.
Kuna watu hata kukemea ubaya ni waoga kwa sababu ya kuhofia sio kuuawa bali kunyimwa vyeo.
Leo hii mpaka viongozi wa dini wanatetea uhalifu wa wanasiasa kisa tu ni fedha na madaraka na urafiki au hata Udini.

Tunataka 2025 watu wapewe nafasi ya kugombea kuanzia kwenye vyama vyao ili tuwapime. Wengi waliopo kwa kweli ni janga kubwa kwa Taifa . Wanajenga taifa la watu wasiojali utu na haki . Huko tunakoelekea uhalifu utakua mkubwa sana . Hakuna atakaye furahia mali alizozihangaikia .

Ni lazima aje kiongozi atakayesimamia haki na sheria za nchi bila kubagua vyama na dini.

Leo wa dini fulani akisema lile sio sawa anashambuliwa na kutishwa na kuambiwa anachanganya dini na siasa as if wanasiasa wao wapo huru kufanya ubaya wowote wanaotaka hata kuvunja sheria wanaotaka wengine wazifuate. Wakati huo huo akitokea wa dini nyingine akasifia mambo ya siasa anaonekana yupo sawa na anapongezwa na inakua sio kuchanganya dini na siasa .

Kuchanganya dini na Siasa Tafsiri yake imekua ni pale uovu unapokemewa
Inaonekana wanasiasa ni haki ya kufanya uovu na wizi ,kudhulumu ,kudanganya na hata kutosha watu .
Dini haijawahi kusifia mtu yeyote duniani labda marehemu siku ya msiba lakini dini kazi yake ni kukemea dhambi bila kujali aliyeifanya ni nani .


Lisu alitendewa ubaya na binadamu wenzake kwa sababu tu ya chuki .Mungu angekua anatuchukia kwa kiwango tunachochiliana basi dunia ingekuwa inawaka moto kila siku. Maana kwa sasa anayekemea ubaya ndiye anayehatarisha maisha yake . Mbaya zaidi ubaya unapimwa kwa dini. Yaani wa dini fulani akifanya ubaya unaoathiri wote,wanajitokeza wa dini yake wanamtetea tena kwa kuwatisha wale wanaokemea kwa Wazi na kunyesha kwa mifano hai makosa yanayofanywa.

Ni lazima tupate kiongozi mwenye kusimamia sheria kwa haki bila kujali dini ,kabila ,jinsia na itikadi za kisiasa .


2025 tulipoenda Vyama kuliko watanzania na Taifa hili tutaliangamiza wenyewe . Nchi za Afrika Magharibi wameshaamke wanaachana na wanasiasa walaghai ,wabinafsi na mafisadi wasiojali nchi zao zaidi ya kujilimbikizia mali , sasa majeshi yameamua kulinda nchi zao kwa kulinda rasilimali za nchi kwa kuwafukiza madarakani majambazi waliojificha kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom