Unadhani nani anafaa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Serikali Mpya ya Rais Samia Suluhu?

Unadhani nani anafaa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Serikali Mpya ya Rais Samia Suluhu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Nimesoma humu wadau wengi wanajadili nafasi ya Makamu wa Rais, pengine ni kwa vile inaonekana dhahiri kuwa wazi kutokana na aliyekuwepo kupandishwa na kuwa Rais kamili, lakini tunapaswa kufahamu kwamba Rais Mpya anapoapishwa kimsingi ni kwamba nafasi zote za uongozi automatically zinakuwa wazi, hii haijalishi kama uliteuliwa juzi au jana na rais aliyepita, nafasi yako anaweza kupewa mwingine ili kwenda na kasi ya Rais mpya kwa kadri ya matakwa yake.

Hivyo basi ni vema kila mwenye maono apendekeze jina la Mbunge yeyote anayedhani aweza kuwa Waziri Mkuu wa serikali mpya , usiogope kumtaja umtakaye unayedhani anao uwezo wa kusimamia shughuli za serikali , hivi vyeo ni kama mbio za kupokezana vijiti tu , leo huyu kesho yule.

Mungu ibariki Tanzania mpya.
 
Back
Top Bottom