Unadhani ni jambo gani ambalo Watu wengi hawalifahamu kuhusu kupata Mtoto/Watoto?

Unadhani ni jambo gani ambalo Watu wengi hawalifahamu kuhusu kupata Mtoto/Watoto?

Wazazi wengi wanatafuta pesa hata wanafikia kusahau upendo na bond kati yao na watoto wao.
 
Uko sawa Mkuu?
Nina uzoefu wa ninachoongea maana mi mwenyewe nilikuwa Mtoto na nilishuhudia nikiwa Mtoto kuwa jinsi ilivyo kwa Ke kuhitaji muda kukaa na Me ktk ndoa mbali na pesa tu na uwajibikaji kifamilia ndivyo hivyo pia Watoto huhitaji muda wetu Wazazi kukaa nao kuwasikiliza, kuwatania, kuwafundisha, kuwaonya na hata kuwaadhibu inapobidi, mbali na hapo Watoto huhamishia upendo wao zaidi kwa house maids kuliko sisi Wazazi.

Chukulia Baba na Mama tuko bize 24hours/7days kuhangaikia chapaa kwaajili ya Watoto na kukosa hata siku 2 tu kuwa karibu na Watoto kimalezi, unadhani akina Juniors, Mashoga, Panya roads n.k tulio nao mitaani ktk karne hii wanapatikanaje ilihali muda wote tumewaachia Watoto wetu housemaids na kurudi majumbani hoi sababu ya uchovu wa kazi?

Tafakari na chukua hatua kwa haki za Watoto.
 
Kama ulivyotangulia kusema nikweli upande wangu nilijikuta hata maamuzi nivyokuwa naamua mwanzo na sasa nitofauti Kila jambo nilifanyalo lazima wakufikilia ni mtoto
Na mambo mengine nimeyagundua baada ya kupata mtoto
 
Ikafika kipindi nataka nijisalimishe kwenda sober house, at the same time demu alokua na mimba yangu amejifungua,,,, binafsi nimelelewa kwa upendo malezi ya baba na mama…. So do her ?

In short life lilichange from that point, niliacha vitu ambazo sikudhania kama ningeweza kuacha, kila nikimuwaza mtoto wangu napata strength, Sitakiwi nimuangushe
 
Back
Top Bottom