Kwasababu sote ni mashahidi, kwakua ni jambo linaloonekana wazi wazi kabisa kwa kila mdau wa jf, kwamba, kuna hali ya ghafla ya kutoaminika na kutokubalika kwa viongozi wa chadema taifa hivi sasa. Na kuna viongozi wa kitaifa ambao kutokana na matendo na mienendo yao isiyoeleweka ndani ya chama, basi mashaka na hofu dhidi yao kwa wanachadema yanaongezeka zaidi. Hawaheshimiwi tena, na wala hawapewi ushirikiano na viongozi wenzao, lakini pia na wanachama wao ndani ya chadema, kama ilivyokua awali.
Changamoto hasa inaweza kua ni nini my friends, ladies and gentlemen?
Je,
ni kwasababu ya tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali za chama kwa maslahi yao binafsi?
Au ni kwasababu hawana uwezo wa mipango na ubunifu wa kimaendeleo, na wameshindwa kabisa kutambua agenda mahususi, mbadala zenye maslahi mapana ya wananchi na zenye nguvu ya kuwaunganisha wananchi, na badala yake wamekua wakivizia matukio ya kisiasa kadiri yanavyojiri?
Je,
au ni baada ya wanachadema wengi waerevu, kuona chama chao chadema, ni kama vile kinatumika kama kituo cha vibaraka na viongozi wao wana tumika kama vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ambao wanazitamani rasilimali za taifa letu, na kwahivyo wanawatumia viongozi wa chadema kama vibaraka wao kwa lengo la kuvuruga amani, kuchochea ghasia ili hatimae vibaraka hao wapate madaraka baada ya kuvuruga amani, kusababisha, uharibifu na maafa?
Kwa maoni yako,
unadhani ni kwanini wanachama wa chadema wamepoteza imani na viongozi wao hasa wa kitaifa.๐
Mungu Ibariki Tanzania