Unadhani ni kwanini Rais Samia na CCM wamemtosa mazima Shaka katika nafasi ya Uenezi?

Unadhani ni kwanini Rais Samia na CCM wamemtosa mazima Shaka katika nafasi ya Uenezi?

Ana tuhuma za rushwa JPM alimpiga chini ukatibu wa mkoa wa morogoro kwa kula mlungula na pia kuna faili limepokelewa toka Mombasa jamaa anataka nkewe
Makandokakando machafu yamemfanya kutokuwa na mvuto ndani ya CCM iliyopasuka vipande vipande, sasa hivi pale panahitaji mtu wa kuwaunganisha wa bara na visiwani pia kuunganisha makundi yanayoparurana ndani kwa ndani kitu ambacho tayari Shaka anakundi lake la Chawa, naona Shaka kutolewa pale ni dalili za mama kujiswafi kwa kutupa nguo zenye chawa na 2025 abaki akiwa msafi
 
Je,.....

1. Hatoshei Kiushawishi?

2. Mnafiki?

3. Mpika Majungu?

4. Muongo?

5. Hana Mvuto / Mvutoless?

6. Si Mpayukaji?

7. Usoni Mama na Rohoni January?

Kazi yangu Kubwa ( Kuu ) leo GENTAMYCINE ni Kutulia na Kusoma Kiumakini mno Comments zenu na naamini hamtoniangusha.
Labda uliyoandika ndio kweli
 
SHAKA AMSHAURI RAIS MAGUFULI KUACHANA NA CHADEMA,AENDELEE NA MIKAKATI YAKE YA MAENDELEO!.

Mwandishi Wetu, Dodoma
Friday,Sep,2016.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema hakuna haja ya mazungumzo, majadiliano wala mijadala inayostahili kufanyika kati ya Serikali ya CCM na Chadema na amemuomba Rais Dk John Magufuli kuendelea na mikakati yake ya kisera ili kuimarisha uchumi.

Pia umoja huo umeeleza kuwa dunia inajua, ulimwengu unaaelewa na Chadema wanafahamu kuwa Tanzania hakuna mgogoro wa kisasa zaidi ya serikali kupigania mabadiliko, nchi kuwa ya viwanda na kutokomeza maadui umasikini, ujinga na maradhi.

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mkoani hapa.

Shaka alisema UVCCM ilijua, ilielewa na kutambua mapema Chadema na viongozi wake walikuwa wakifanya maigizo katika siasa, hawakuwa na ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai aliyoyaita ni ya kipuuzi ambayo hayana msingi kwa mustakabali wa nchi na maendeleo yake.

Alisema viongozi na wafuasi wa Chadema walishindwa kuandamana Septemba Mosi, hawataweza na wala hawatajaribu kufanya hivyo Oktoba Mosi kwa sababu wanachotaka kukifanya ni utoto wa kisiasa baada ya kushindwa kubuni mkakati wa kukiendesha chama chao ili kiaminike na kukubalika
Tunazo habari wabunge wa Chadema wamechachamaa na kumbana Mbowe kwa hoja wakitaka kurudi bungeni ili kushiriki vikao kwa kuwa hawaeleweki kwa wapiga kura wao majimboni lakini pia wanakabaliwa na 'waya mkali', hawaoni kwa nini wasishiriki vikao vya Bunge huku baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho wakiwa na utajiri na wengine wafanyabiashara,"alisema Shaka.

"Cha ajabu hata na wale wazee tuliokuwa tukiwaheshimu bila soni wanashiriki kuudanganya ulimwengu wakitoa madai ati kuna mgogoro wa kisiasa unaohitaji suluhu, yafanyike mazungumzo na majadiliano,"alisema Shaka.

Alisema UVCCM imeshangazwa na madai ya Chadema na kusema kwamba chama hicho na viongozi wake wamekuwa wakikutana na viongozi wa madhehebu ya dini na mashirika ya kiraia, kisheria yaliyowataka ati wasiteshe maandamano kwa muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.

"Tumekuwa tukijiuliza bila kupata majawabu ya kina pale Mbowe na Chadema wanaposema wameshauriwa na viongozi wa madhhebu ya dini na taasisi zingine. Je hapo awali pia walishirikiana na viongozi hao kupanga na kuitisha maandamano yenye lengo la kumdhihaki Rais na kumwita dikteta?" alihoji Kiongozi huyo wa Vijana.

Hata hivyo, alisema si jambo linaloingia akilini na mtu alazimike kuyamini maneno ya Chadema kama kweli viongozi wa dini na taasisi zilizotajwa, walihusika na kushiriki mpango wa uitishaji maandamano ya vurugu na sasa wahusike tena kuwakataza Chadema wasifanye maandamano.
"UVCCM, wananchi wema, wapenda amani na utulivu, viongozi wa mashirika ya kiraia na madhehebu ya dini, hatuwezi kusimama hadharani kuitbitishia dunia kama Tanzania kuna mgogoro wa kisiasa unaohitaji yafanyike mazungumzo, majadiliano hadi kufikia mapatano," alieleza Shaka.

Alisema ulimwengu mzima unafahamu, mashirika na jumuia za kimataifa nazo zinaelewa kwamba katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, wananchi walitekeleza wajibu wao wa kikatiba na kupitia demokrasia ya uchaguzi walimchagua kwa kura Rais Dk. Magufuli kuwa Rais wao na matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa na chombo chenye dhamana ya kisheria na kikatiba ambacho ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Shaka, alisisitiza kuwa wananchi wote, mashrika ya Kimataifa na ulimwengu unaelewa Dk. Magufuli baada ya kuchaguliwa, serikali yake bila kupoteza wakati imekuwa ikihimiza kwa nguvu zote mpango wa uwajibikaji, utendaji wenye ufanisi, nidhamu, huku serikali yake ikipiga vita ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma pia ikikusanya kodi na kuongeza mapato ya taifa.

"Chadema na UKUTA wao wanachotaka ni siasa za mitaani na maandamano haramu. Wanataka kukithiri kwa malumbano na mabishano yasiyo na maana badala ya wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji wafanye kazi kwa bidii, kujituma ili wazalishe mali na kujienga uchumi na kimaendeleo alisema,"alisema Shaka .

Shaka alieleza kuwa haipendezi na haiwapi hadhi au heshima mbele ya jamii watu wanaojiita viongozi wa kisiasa wa Chadema kuwa na uhodari wa kutunga uongo, wakauamini, kuueneza na kuutetea kwa misuli ya unafiki na upotoshaji.

"UVCCM tunawaasa viongozi wa Chadema waache mara moja siasa za utoto na tabia ya kuwatia hofu wananchi, wasiwafanye waishi kwa wasiwasi kwa siasa zao uchwara ambazo zimekosa afya na wala haiwapi heko au heshima mbele ya dunia,"alisema Shaka.
View attachment 2483407

My take!
Shaka huyu huyu ndie alimgeuka Magufuli baada ya kufa!
Akawa amehamia ofisi mpya na chini ya Rais Mpya!

Akageuka na kuwa muumini mpya ndani ya CCM.

Unafiki ukaendelea kwa 110%..

Huenda Sasa Msoga Gang wamekumbuka baadhi ya wana CCM na kuanza kuwaondoa wale sampuli ya Shaka.
Kwa hofu ya kumsaliti mama Tozo na Msoga Gang at all.....
 
Aheri wizi wa Magufuli,aliiba na kazi tuliiona.
Wizi wa Magufuli tuliupenda na hata angeendelea kuiba tungependa wizi wake kama tunavyopenda Bondia Mandonga anapopigwa....ndio tunazidi kumpenda na kumshabikia zaidi.
Isitumie neno Tulimpenda,sema ulimpenda.

Mimi yule fisadi papa ningekuwa Rais na hajafa ningemtia kolololoni.

Mtu ambae madarasa tuu ya Watoto yalimshinda ndio eti mambo yake mliyaona
 
Isitumie neno Tulimpenda,sema ulimpenda.

Mimi yule fisadi papa ningekuwa Rais na hajafa ningemtia kolololoni.

Mtu ambae madarasa tuu ya Watoto yalimshinda ndio eti mambo yake mliyaona
Sema wewe.....
Magufuli anao wafuasi kibao na msione wamekaa kimya mkachukulia poa.

Na Magufuli aliwatumbua watu kama nyinyi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mmemuua lakini hamuwezi ua legacy yake!

Mtakufa mtamfuata akhera mkiwa na chuki zemu milele.

Vinginevyo nikushauri 8nunue nyundo kubwa uende nayo kaburini kwake chato ukavunje vunje kaburi kama unao uwezo huo.

Wasaliti wa Magufuli hawatakaa waishi kwa amani nchi hii.

Kivuli chake kinawatesa muda wotee!

Madarasa yapi yaliyomshinda?

Mpaka sasa miradi yote ambayo CCM inategemea kuingia nayo kwenye kampeni 2025,ni miradi ya Magufuli tupu.

Taja mradi aliobuni Samia kama Samia,tangu ameingia Madarakani??

Mama yenu anachofanya ni kutembelea nyota ya Magufuli tu!

Na asipoangalia na yeye itakula kwake,kupitia box la vikaratasi,ashukuru Poli-CCM tu.
 
Sema wewe.....
Magufuli anao wafuasi kibao na msione wamekaa kimya mkachukulia poa.

Na Magufuli aliwatumbua watu kama nyinyi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mmemuua lakini hamuwezi ua legacy yake!

Mtakufa mtamfuata akhera mkiwa na chuki zemu milele.

Vinginevyo nikushauri 8nunue nyundo kubwa uende nayo kaburini kwake chato ukavunje vunje kaburi kama unao uwezo huo.

Wasaliti wa Magufuli hawatakaa waishi kwa amani nchi hii.

Kivuli chake kinaeatesa muda wote!
Angekuwa na wafuasi kibao ngeiba uchaguzi wa 2020? Nani ambae hana wafuasi? Ndo hamna Cha kufanya Wala sio kukaa kimya..

Mwisho mtu ambae madarasa y Watoto yalimshinda ni WA nini Sasa huyo?
 
Angekuwa na wafuasi kibao ngeiba uchaguzi wa 2020? Nani ambae hana wafuasi? Ndo hamna Cha kufanya Wala sio kukaa kimya..

Mwisho mtu ambae madarasa y Watoto yalimshinda ni WA nini Sasa huyo?
Mpaka tunapoongea na kuandika!
Nchi nzima ya Tanzania!
Hakuna Chama, wala taasisi wala wanasiasa uchwara kama nyinyi,kwamba mmewahi kuonyesha ushahidi ni wapi na kwa namna gani Magufuli aliiba kura!

Mlipigwa chini na wananchi,na mkiendelea na ujinga....

Mtakataliwa tena na tena!
 
Mpaka tunapoongea na kuandika!
Nchi nzima ya Tanzania!
Hakuna Chama, wala taasisi wala wanasiasa uchwara kama nyinyi,kwamba mmewahi kuonyesha ushahidi ni wapi na kwa namna gani Magufuli aliiba kura!

Mlipigwa chini na wananchi,na mkiendelea na ujinga....

Mtakataliwa tena na tena!
Alikwapua Til.1.5 ,,ccm mnajitahidi kuficha huu wizi ila jinai haiozi, Mwendazake hayupo ila nyie wanufika mpo
 
Back
Top Bottom