Mimi nitakuwa wa kwanza kunyanyua bango kumtaka mkuu wa nchi aachia ngazi sio mtu asiye na nafsi ya kufanya chochote katikati ya aina ya utawala uliopo. Waziri mkuu kwa sasa hivi anaendeshwa kinyume na anavyotamani kushughulika na matatizo wanayokumbana nayo wananchi ikiwemo kwenye majanga (disaster).
Ili kuwezesha kamati ya maafa kutekeleza majungu yake ipasavyo inatakiwa kila mkoa uwe na vifaa na wafanyakazi waliojitosheleza ambapo zinazohitajika ni fedha kuwekezwa. Anayeidhinisha ni mkuu wa nchi sio waziri wa fedha wala waziri wa fedha. Ni bora hata waziri mkuu alifika eneo la tukio kuliko mwenye mamlaka husika kuendelea kuchanja mbuga ughaibuni.
Kwanini hamjamsakama waziri wa ujenzi/uchukuzi na mawasiliano/habari kuhoji kitu gani kilichotokea hadi hali hiyo ikatokea na watendaji bado wapo ofisini?
Ninakupongeza kuwa unapandisha uzi zenye kutia changamoto kwa wahusika lakini usipendelee wala kuwaogopa watu ambao unadhani ukiwagusa utafuatwa na Noah maana bado zipo zinavizia tu nani anasema nini
Nyanyua uzi wa maji, chakula, bei za bidhaa kupanda, umeme kukatika, kwanini waziri wa mazingira hakwenda mkuu wa COP27 wakati unamhusu moja kwa moja badala yake wanaenda watu wengine ambao wanatuhumiwa kusababisha mojawapo ya madhara ya ukatikaji wa umeme hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wanaowekeza kufanya biashara wakitegemea nishati hiyo.
Nakupa 'Assignment' upige kampeni ya visima vya maji kwa ajili ya wakaaji wa Dar Es Salaam vichimbwe Mkuranga ambako maji yake hayana chumvi wala uchafuzi wa mazingira sio huko Kigamboni.
Kwa sasa bahari ya hindi inasukuma maji kuingia mto Ruvu (salty ocean water surging) hivyo kuufanya uende kinyume nyume hadi Ruvu juu. Ukipita Mlandizi-Ruvu mto una maji mengi tu lakini ni ya chumvi ambayo yanasukumwa na bahari kutokea Bagamoyo.
Chanzo cha mto Ruvu hiki hapa, uoto wake unatakiwa uendelezwe hadi unafika baharini kuhakikisha unaendelea kutiririsha maji mwaka mzima
View attachment 2412110
View attachment 2412112
View attachment 2412115
Hapa chini ni Dutumi kuna miamba na miti iko mbali na mto
View attachment 2412119
*Matatizo ya upungufu wa maji yaanzia kabla ya Ruvu stesheni kuja Kwala kutokana na shughuli za kibinadamu
View attachment 2412126
Kijiji cha Kilangalanga kabla ya Mlandizi maji yako vizuri ikichagizwa na uoto wa asili kuwepo
View attachment 2412137
View attachment 2412156
Mto Ruvu ukiwa umbali mchache kutoka kijiji cha Vigwaza Pwani hapo chini
View attachment 2412160
Matatizo mengine yanaanza kwa kasi baada ya Kilangala kuja Kwala, Vigwaza, Ruvu stesheni hadi Ruvu darajani shughuli za kibinadamu ikiwemo mashamba, ukataji wa miti mifugo na kadhalika
View attachment 2412174
Please preserve Ruvu river for a continued water utility generation for the human being and environmental sustainability