Unadhani ni nani anafaa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya Kassim Majaliwa kumaliza muda wake?

Kwakuwa wewe ni Mwanachadema, ebu nidokezee kwanza nani atamrithi Freeman Mbowe kwenye Uwenyekiti na baada ya hapo nitakwambia nani atakuwa PM baada ya Majaliwa.
 
Ya CHADEMA yamewashinda mnaanza kurukia CCM , Najuwa hata wewe unaamini kuwa ccm ndio chama kiongozi na kinachotumainiwa na kuaminiwa na watanzania wote Ndio sababu ya Kuendelea kuamini kuwa viongozi Bora ni lazima watoke CCM, Nakukaribisha Sana mkuu ndani ya CCM, karibu CCM ili unapokuwa Mbeya uanzage kuwapa Elimu Wana wapotevu
 
Unanikaribisha ili nilogwe ?
 
Seriously sijaona kati ya hao walioko mjengoni.. Labda atoke nje ya mfumo
 
Mimi nampendekeza Ashura Cheupe. Huyu ni mtu wa watu, anaudhubutu, anajulikana nchi nzima na ana koneksheni hadi uarabuni.
 
Mkuu hakuna Waziri Mkuu wa Milele , mimi utaniloga bure tu .
Mimi nitakuwa wa kwanza kunyanyua bango kumtaka mkuu wa nchi aachia ngazi sio mtu asiye na nafsi ya kufanya chochote katikati ya aina ya utawala uliopo. Waziri mkuu kwa sasa hivi anaendeshwa kinyume na anavyotamani kushughulika na matatizo wanayokumbana nayo wananchi ikiwemo kwenye majanga (disaster).

Ili kuwezesha kamati ya maafa kutekeleza majungu yake ipasavyo inatakiwa kila mkoa uwe na vifaa na wafanyakazi waliojitosheleza ambapo zinazohitajika ni fedha kuwekezwa. Anayeidhinisha ni mkuu wa nchi sio waziri wa fedha wala waziri wa fedha. Ni bora hata waziri mkuu alifika eneo la tukio kuliko mwenye mamlaka husika kuendelea kuchanja mbuga ughaibuni.

Kwanini hamjamsakama waziri wa ujenzi/uchukuzi na mawasiliano/habari kuhoji kitu gani kilichotokea hadi hali hiyo ikatokea na watendaji bado wapo ofisini?

Ninakupongeza kuwa unapandisha uzi zenye kutia changamoto kwa wahusika lakini usipendelee wala kuwaogopa watu ambao unadhani ukiwagusa utafuatwa na Noah maana bado zipo zinavizia tu nani anasema nini

Nyanyua uzi wa maji, chakula, bei za bidhaa kupanda, umeme kukatika, kwanini waziri wa mazingira hakwenda mkuu wa COP27 wakati unamhusu moja kwa moja badala yake wanaenda watu wengine ambao wanatuhumiwa kusababisha mojawapo ya madhara ya ukatikaji wa umeme hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wanaowekeza kufanya biashara wakitegemea nishati hiyo.

Nakupa 'Assignment' upige kampeni ya visima vya maji kwa ajili ya wakaaji wa Dar Es Salaam vichimbwe Mkuranga ambako maji yake hayana chumvi wala uchafuzi wa mazingira sio huko Kigamboni.

Kwa sasa bahari ya hindi inasukuma maji kuingia mto Ruvu (salty ocean water surging) hivyo kuufanya uende kinyume nyume hadi Ruvu juu. Ukipita Mlandizi-Ruvu mto una maji mengi tu lakini ni ya chumvi ambayo yanasukumwa na bahari kutokea Bagamoyo.

Chanzo cha mto Ruvu hiki hapa, uoto wake unatakiwa uendelezwe hadi unafika baharini kuhakikisha unaendelea kutiririsha maji mwaka mzima



Hapa chini ni Dutumi kuna miamba na miti iko mbali na mto

*Matatizo ya upungufu wa maji yaanzia kabla ya Ruvu stesheni kuja Kwala kutokana na shughuli za kibinadamu

Kijiji cha Kilangalanga kabla ya Mlandizi maji yako vizuri ikichagizwa na uoto wa asili kuwepo

Mto Ruvu ukiwa umbali mchache kutoka kijiji cha Vigwaza Pwani hapo chini

Matatizo mengine yanaanza kwa kasi baada ya Kilangala kuja Kwala, Vigwaza, Ruvu stesheni hadi Ruvu darajani shughuli za kibinadamu ikiwemo mashamba, ukataji wa miti mifugo na kadhalika

Please preserve Ruvu river for a continued water utility generation for the human being and environmental sustainability
 
Nakushukuru , Lakini uzi wangu hauhusiani na ajali ya ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…