Unadhani vijana wakipewa mikopo ya biashara, itaondoa tatizo la ajira Nchini?

Unadhani vijana wakipewa mikopo ya biashara, itaondoa tatizo la ajira Nchini?

Mitaji ya kukopeshwa… ni ngumu kuwa a full risk taker
Mtu kakupa hela kwa dhamana ya nyumba unategemea utafanya risk taking kweli? 😀

Ila una 300M zako mahali ukaamua kuweka 10M uanze kufanya biashara unaweza ukafika mbali.

Sababu biashara ina kawaida moja, kwenye early stages ina kawaida ya kuhitaji boost za hapa na pale. Sasa imagine una mtaji limited how can you survive? Itaanza kuyumba yumba hadi kufa na huna kitu utafanya sababu hela huna.
 
Ni kweli
 
Tatizo la ajira nchi hii
Ni Kama lilivyo tatizo la Nguvu za kiume kelele kibao&linakuzwa mno kuliko uhalisia
Hahahah braza tulia, we umeingizwa kwenye ramani toka form 2 huwezi kuhisi ugumu wa tatizo hili. Tayari wewe ni Mogul!
 
Kuna ajira sio utumwa.Huna kaz za maana saana but you get paid alotno money
Ajira kuwa utumwa inategemea na channel uliopo. Kuna mwana alikuwa anadiss sana habari za kuajiriwa ila sahizi amekabidhiwa Godauni la mitumba na mchina.

Ukimwambia habari za kurudi kununua na kukamua alizeti Babati vijijini hataki hata kuzisikia tena wakati alikuwa anajifanya mpambanaji kweli kweli.

Niliwahi mwambia njoo Dar achana na mambo ya kukaa mashambani huko. 🤣🤣🤣 Sahizi ameelewa sasa kwamba kwanini Dar inaitwa Bongo.

Yuko mahali ambapo kupata laki 3 hadi million kwa siku ni kawaida. Na still ana mshahara mzuri tu mwishoni. Anakula kwa ubua tu sahizi amekaa kitengo cha hela.
 
Sasa inatia uoga sana mkuu, kwa mtoto wa bhakresa anaweza furukuta akajaribu biashara hata 5 tofauti. Wewe moja tu ukienda chali nyumba imeuzwa.
Ahahahahahahahah......sema kashkash za hiz mbinde huwa zinafanya always uwe mtu wa ku find out solutions
 
Ahahahahahahahah......sema kashkash za hiz mbinde huwa zinafanya always uwe mtu wa ku find out solutions
Lazma utafikirisha ubongo, huwezi ku relax ila finally utajikuta umekaa kwenye mfumo flani ambao huumii sana na mambo yanaenda. Huwa naichukulia biashara kama kupanda gari ilioshona kweli kweli kama mwendokasi.

Mwanzo utabanwa sana utashikilia mkono mmoja na kukanyagia vidole ila kadri gari inavyoenda mnajichekecha utashangaa umeweka miguu yote chini na kuwa na balance nzuri ya kusimama.
 
Habari wanajukwaa.... karibu uchangie hii mada kwa leo inakujia mara moja kwa week.
#FUNGUKA.
.......
View attachment 2592653
siyo rahisi kutoboa kwa mkopo, kama wewe huna kitu kabisa labda msaada kidogo kama una akili nzuri hauna wenge, umepewa msaada ambao hufanyi rejesho kabisa unaweza kutoboa. nina experience na mikopo
 
Habari wanajukwaa.... karibu uchangie hii mada kwa leo inakujia mara moja kwa week.
#FUNGUKA.
.......
View attachment 2592653
HAPANA - HAPANAAA. Hapana Kabisa.
Vijana kupewa mkopo lazima kigezo kimojawapo na cha lazima kiwe ni kijana awe/aoneshe Andiko la Mradi au Business Plan. Tena awe na Mdhamini ambaye sio kijana mwenzake - ingefaa Mdhamini awe ni mtu mzima (45-50 yrs old) na ni mwajiriwa Serikalini. Uzoefu unaonesha kuwa Serikali ya Kijiji kuwa ni mdhamini wa Mkopaji haifai kuna mapungufu mengi sana.
Tukumbuke wahenga waliwalinganisha vijana na maji ya moto na kusema hayachomi nyumba.
Kijana Leo yupo huku Umasaini akipata mkopo kesho utamkuta ni mlinzi Dar, kesho kutwa kazamia machimbo ya madini cabo del gado (Hao ni Me) kwa upande wa Ke ndo usipime; leo kaanzisha saloon, wiki ijayo kaolewa hukoo... mara paap kaachika n.k. n.k. Ufuatiliaji ni mgumu sana.
 
Back
Top Bottom