Bila shaka chikunde mnamjua, kile kidada kinatolewa out na jamaa, kinajifanya sehemu nzuri ndo maeneo yangu kumbe ki asha ngedere hakijui kitu...Ulishawahi kudate na mtu mambo safi kiasi cha kuogopa kukaa nae mahali ukihofia kuaibika? Labda akikuuliza unatumia ketchup unajibu hapana halafu unamuita mhudumu alete tomato?😛
Mimi nilichokua nafanya ni kukataa tu najifanya nmeshiba kumbe tumboni ni empty, tumbo linaunguruma tu gruuu gruuu akisema tupite sijui burger point sijui pizza hut namwambia thanks much nimeshapata msosi am okay kumbeee minyoo imechachamaa tumboni, atakaponiacha lazma nikimbie fasta kula, nlikua nawaza labda nitakutana na menu siijui niishie kuabika. Nawaza mambo ya kula na uma na kisu naona tabu, mi napenda nikila samaki nimvuruge vuruge yani nisagesage mifupa ukiikuta mifupa usijue ni ya kiumbe gani. Kama ni kuku hivo hivo sasa nikiwa na huyo mambo safi si nitajitia aibu.
Siku moja nlikua so down nikaenda pale tilapia hotel kupunga tu upepo, nimeorder chips kuku uma na kisu pembeni. Sijui ndo kujali mteja jamaa kasimama pembeni nikashika ile uma na kisu nazuga zuga pale huku nikijiona chikunde, ikawa sasa nakula kwa kuvizia utadhani naiba akigeuka nakamata kuku kwa mkono kahkakah vunja vunja mifupa then nashika kisu utadhani nimekitumia nlipataje tabu!!!nashukuru aliondoka nikala kwa raha.
Siku nyingine tumekaa mezani mambo ni yale yale kikuku hiki hapa mara uma, nikajitahidi tu hivo hivo nikamuacha na nyama nyingi roho ikiniuma, kwakifupi nikiona dalili za kuwa chikunde nakataa mtoko muda ntakaoenda kutafuta wali maharage na chachandu naujua mwenyewe sitaki aibu!!!!