GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Dr. Napoleon Hill, anayesadikika kuwa alitumia kipindi kisichopungua miaka ishirini kutafiti sababu inayowafanya watu kufanikiwa na wengine kufeli, alikuwa na kawaida ya kuwashauri "wanafunzi" wake kuwa kama wanaishi mijini, basi wawe wanaenda vijijini alau mara moja kwa mwaka, na kama wanaishi vijijini, mwaka usipite bila kwenda mjini.
Naye Brian Tracy, mmoja wa waandishi maarufu wa self help books, anaamini kuwa kama asingeanza mapema tabia ya kusafiri, asingefika hapo alipo kimaendeleo. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na nane, alifanya safari kwa gari binafsi kutoka Kaskazini mwa Afrika hadi Afrika Kusini. Alikuwa na rafiki zake wawili, kama sikosei. Kimsingi, safari yao ukianzia Marekani kwa sababu ndiko walikokuwa wakiishi kipindi hicho.
Mwanzoni walitarajia kutumia usafiri wa baiskeli, lakini walipofika Afrika, waligundua baiskeli haitafaa kwa safari ya kupita jangwa la Sahara, hivyo wakachanga hela na kununua gari aina ya Land Rover, nafikiri.
Wataalam kadhaa wameshaelrza faida za kusafiri. Wewe unafikiri kwa nini ni muhimu kusafiri safari ya "mbali" alau mara moja kwa mwaka?