Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 16,911
- 28,469
Wakuu
i salute you kinsmen
Mimi kama mimi mwenyewe nimafuatilia sana team yetu tangu mwanzo mwa msimu na mara kadhaa niligusia swala moja moja ila leo nitagusia yote yanayotukwamisha kwa namna moja au nyingine hapa.
1: KOCHA WA FITNESS.
ndugu zangu tangu mwanzo ilionekana huyu kocha wa viungo tulibugi kabisa, ni kocha wa fitness wa gym tu.
Haonekani kujua soka kabisa yeye anajua fitness ya misuli tu kama hawa mabondia au ma designer wa fashion.
Jamaa inaonekana anawapa mazoezi magumu wachezaji bila kutambia reflexibility na inapelekea kuwa na muscle reaction ndogo kwa wachezaji wetu na hili tunaliona wazi.
Wachezaji wachache wana ile fitness kubwa ya kucheza mchezo kwa dakika 90.
Duke oga abuya
Dickson job
Maxi nzingeli
Pacome zouzozua
Basi wengine ndio vile wanajiforce tu ila inaonekana wazi uongozi hauoni hili fanyeni kabla hatujaenda huko kukutana na ahly ahly mmeona wanavyocheza hapo jana huko kwao na zamalek??
Sielewi kwanini yule jamaa aliyepita bwana Talib yule mwarabu asirudishwe kuja kuendelea na kazi yake ya fitness?? Yule alikuwa ni mtu wa mpira pia sio huyu wa sasa na limiwani lake kama fundi mchomelea vyuma kutoka veta chang'ombe.
2:KUHUSU STRIKERS WETU..
hapa ndio pa kuangalia zaidi, yanga tangu kuondoka kwa mqyele tumehangaika sana kutafuta striker lakini tukaambulia wenye uwezo wa kawaida
Hafidh konkoni
Kambole
Joseph Guede( huyu kwa muda aliokaa alionyesha kitu(
Na sasa ni Dube ni Boyeli qmbao wote hawa wana uwezo wa kawaida tu ..
Kosa lingine lilikuwa ni kumuacha musonda
Huyu jamaa alikuwa anajua kucheza mechi za kimataifa na haogopi, ameshafanya mengi kwenye game za kimataifa hata tukihesabu kazi bure kabisa
Tulihitaji wachezaji majasiri kariba ya musonda kimataifa na sio Dube anayecheza kwa pressure kubwa kichwani mwake..
Sawa ni striker mzuri sana na anafanya kazi kubwa uwanjani ila apunguze uoga na pressure.
Angalia sasa Boyeli yeye dakika chache tu akafunga kwa kukaa sehemu nzuri
Dube alikuwa anapishana na mpira goli la jana la pacome dube alikuwa kashakosa kukaa kwenye nafasi ikamkuta pacome ..
Msimu wa dirisha dogo inabidi kuna watu wasiangaliwe usoni tena kwa huruma tutafute striker wa uhakika sio hawa wa kubahatisha..
3: ENEO LA UKABAJI CDM
Hapa tusiwe waongo wakuu wangu yanga ni either Bala conte aanze kuaminiwa kupewa nafasi au lah auzwe tu sasa amesajiliwa wa nini??
Duke abuya sio namba sita kiasili lakini anacheza eneo hilo kwa nidhamu na kujituma kwanini huyu Conte hachezi? Ameshindwa kuonyesha uwezo mazoezini? Basi dirisha dogo auzwe tu hakuna haja ya kumfuga otherwise kama anaonyesha kitu apewe nafasi tu.
Tunaelekea pagumu sana
Ahly ahly pale kuna jitu mwitu pale Dieng mwili jumba utadhani anakula cement.
Rabat kuna kajamaa pale kanapiga Dm pasi kama Dobi wa majengo pale
Sasa Siku Duke akichoka tutamlaumu bure na nje atakuwa conte ambaye hana game time tutaumia tu ..
Hapa tupafanyie kazi ..
Sina shida na namba nane na kumi hapo hakuna noma..
4: BEKI YA KULIA
bwana mwenda naye ameanza kupunguza umakini wake akienda kushambulia umepungua sana, cross nyingi hazina macho tena kama yule wa msimu uliopita ambaye kila alichofanya mbele ilikuwa dhahabu mpaka anafunga
Huyu mwenda wa sasa karidhika maana upande wake hakuna mshindani wa kumchallenge kabisa, kijana ajiangalie yao akija kukaa sawa itakuwa ngumu kwake..
5: ECUA APEWE MUDA ZAIDI KUCHEZA.
huyu bwana ni winga mzuri sana kushoto anachokosa ni ule ubinafsi wake sehemu ya kutoa pasi anapoa kwanza ana relay ila anaimprove sana na ni game changer game hizi mbili tatu kafanya kazi nzuri sana ..
Mwisho ni tumuache Bwana Pedro afanye kazi yake ingawa maoni kama haya sio ya kupuuzwa kabisa tunaelekea kwenye game ngumu sio muda sana na waarabu wale..
Au kocha kindo ngara23 Unasemaje?
Mzee wa kazi Tate Mkuu unasemaje?
YANGA BINGWA