Unahitaji Kuchangia Taasisi ? FAHAMU HAKI ZAKO/TARATIBU WEWE KAMA MCHANGIAJI (Philanthropist/Donor)

Unahitaji Kuchangia Taasisi ? FAHAMU HAKI ZAKO/TARATIBU WEWE KAMA MCHANGIAJI (Philanthropist/Donor)

Joined
Jun 21, 2021
Posts
6
Reaction score
12
1639317799429.png


Katika masuala ya Harambee (fundraising), Tanzania bado hatujaweza kuwa na chombo maalum ambacho kinapaswa kutoa utaratibu pia muongozo katika suala zima la Harambee. Kutokuwa na chombo hiki kwa Tanzania haimaanishi kwamba, Harambee inapaswa kufanywa pasina kufuata taratibu, la hasha. Kuna taratibu za kiujumla (General Rules) ambazo hufuatwa na mataifa mbalimbali katika Harambee.
Ikiwa unahitaji kuchangia kiasi cha fedha au rasilimali yoyote kwa Taasisi, wewe kama mchangiaji (Philanthropist/Donor) unapswa kufahamu haki zako kwa Taasisi unayoichangia, pia kanuni za kijumla zinazoendesha mchakato wa Harambee. Kanuni/Taratibu hizi ni kama ifuatavyo;
  • Kabla ya kuichangia Taasisi yoyote, una haki ya kujulishwa " Lengo la kuanzishwa kwa Taasisi husika" kwa kiingereza tunaita "Mission Statement"
  • Kabla ya kuchangia Taasisi yoyote, una haki ya kuwajua watu wanaohudumu kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi husika (To be informed about Board's Members)
  • Kuhakikishiwa kwamba mchango wako (gift) utatumika kwa kile ulichoombewa. Kama Taasisi imekuomba uchangie ujenzi wa Shule, basi una haki ya kuhakikishiwa kwamba mchango uliotoa utatumika kwa ujenzi wa shule TU na si vinginevyo.
  • Kutambuliwa kwako kwa mchango uliotoa. Hii huweza kufanyika kwenye ripoti ya mwisho baada ya Mradi, pia kwenye mitandao ya Kijamii/Tovuti ya Taasisi husika
  • Uhusiano baina yako (mchangiaji) na muwakilishi wa Taasisi katika Harambee unapaswa kuwa "professional in nature"
  • Unahaki ya kufahamishwa kwamba, wawakilishi wa Taasisi waliokufuata kwa ajili ya Harambee ni waajiriwa wa Taasisi husika (employees), wanajitolea (volunteers) au wamekodishwa kwa ajili ya Harambee (Hired Solicitors)
  • Una haki ya kuuliza swali lolote juu ya mchango unaotoa, na Taasisi inayonufaika na mchango wako ina wajibu wa kukujibu kwa haraka na utaratibu mzuri juu ya kile ulichouliza.
  • Una haki ya baadhi ya taarifa zako (kama mawasiliano n.k) kutokutolewa kwa umma ikiwa utataka hivyo.
AHSANTE
HEINZ Consulting
Consultancy, Project Management, Strategy, Fundraising & Training
PC 12119
Email: heinzconsultancy@gmail.com
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom