Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
Wasaalam Wana Jukwaa wote.
Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;
UTARATIBU;
Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;
1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.
2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.
3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.
4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.
5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.
Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.