Unaikumbuka nick name yako ya sekondari? Tupia hapa

Unaikumbuka nick name yako ya sekondari? Tupia hapa

Mie labda nikuinbox, lakini kuweka hapa..... Nitapiwa lifetime BAN
 
primary- every corner,shakes
form one -mbezi chafu,chandimu,domo zege
form two-nbsujo
form three-nature,dia mama,ngumu nyeusi
form four- kama form three
5&6- makaveli,mzee wa solex,mzee wa lock,anko B,mzee wa mabungubungu, Kakabraza(brazakaka).
chuo-Makaveli,Mzee wa kukomoa,mido mkazaji
mtaani- Makaveli,Mkali wa donta,professional,Ras Simba,white
 
Kuna JAMAA alikuwa akijiita CYBORG,,jamaa alikuwa mbabe haswa pale shule,,wakati ule ile MOVIE YA CYBORG ya VAN DAMME ndy inatamba,jamaa alijifananisha na lile kubwa la maadui kwenye movie ile,,,basi jamaa alitumia nguvu nyingi hadi jina likamkaa,,sasa baadae akagunduwa kwamba kumbe CYBORG kwenye ile movie hakuwa yule kubwa la maadui,,bali CYBORG ni mwanamke mmoja mle ndani,,na sio mwanaume kama alivyodhani yeye,,basi ikawa shida kulivua jina hilo na huku tushalizoea kumwita,, jina lilitupa shida sana kulisahau,,na ukimwita elewa utafute kwa kupitia, ,HIZI NICK NAMES zingine bila kufanya upembuzi yakinifu ni balaa..
 
Hazina P. school niliitwa Predator maana nlikua napenda sn yule predator kwny ile muvi

Marian Boys sec niliitwa The Viper maana nilimpenda sn Randy Orton.

Feza Boys High school, niliitwa Kidumu/Komba maana nilikua mnazi wa ccm afu nilikua napenda kuimba nyimbo za komba class Hasa nikiona nmekaa na wale kwenye itikadi za upinzani
 
Mimi waliniita poison ship, nilikua nikipita kwenye dom lenu huko nyuma lazima niache vilio, nimewahi kufungua trunker za bweni zima nikapita na sukari ya kila mtu, nilipoichanganya ilijaa kiroba nikawa nawauzia.
 
Mh mi yangu siitaji

Pale tosa ilikua ikitoka pap two ilikua inafata yangu kwa umaarufu cha kushangaza wengi walikua hawanijui ilikua kila mtu akinijuia ni mimi anapatwa na bumbuwazi coz walikua wanajua ni bonge la mtu

Mh hizi a.k.a ni shida kwa kweli
Hahaaa Mkuu Tosa boys tunyoshe mikono juu hii 2007
 
Joka lenye makengeza ndio ilikuwa nickname yangu
 
Naikumbukaga sana nickname yangu jaman enzi hizo nipo form 3 nilianza kujiita YOUNG SINGLE n FREE!(Y.S.F)lilivuma sanaaaa! had kwenye daftar la teacher zwazwa unaandika tu sema masomo ya teacher mnoko huthubutuu ! lol
kaka yangu alikua akijiita MPUSH(akimaanisha msukuma) rip bro
dada yangu alikua akijiita ability heheheh nakumbuka wazaz hawakuwa wanayajua haya majina kbs !
tupia a.k.a yako enzi za shule
makanjanja
 
Tako boy, kisa sura yangu imekomaa kama tako! a.k.a yangu ya primary hiyo sekondary sijabahatika kufika!
 
Back
Top Bottom