Unajenga nyumba ya milion 300 ili upangishe laki 3, ni akili au matope?

Unajenga nyumba ya milion 300 ili upangishe laki 3, ni akili au matope?

Hoja yako inajibiwa kama hivi


Mtu kajenga nyumba ya thamani ya milioni 300.

Kumbuka bado anaimiliki hiyo nyumba bado (asset).

Kila mwezi anapata kodi ya laki 3.

Kwa hiyo:

Mwezi wa kwanza ana:

Nyumba yenye thamani ~ milioni 300

Cash ya kodi laki 3

Net worth yake inaweza kusemwa imefika milioni 300 & laki 3 (kabla ya gharama nyingine).

Baada ya mwaka:

Kodi: 300k × 12 = 3.6M

Endapo akiuza nyumba baada ya Mwaka kwa 320M:

Anapata 320M + 3.6M = 323.6M gross receipts.


Na pia

Tanzania mara nyingi thamani ya ardhi/kiwanja hupanda kadri muda unavyoenda.

Jengo lenyewe linaweza kushuka thamani (depreciation).

Lakini kwa maeneo mengi yenye maendeleo, ongezeko la thamani ya ardhi linaweza kuzidi depreciation ya nyumba, hivyo overall property value ikaongezeka.

Ndiyo maana real estate mara nyingi ina nguvu kwenye:

Cashflow (kodi)

Capital appreciation (ongezeko la thamani ya property)

Asset ownership

Ila kiuhalisia kuna vitu vinapunguza hiyo “faida halisi”, kama:

gharama za maintenance,

kodi ya serikali,

kipindi nyumba haijapata mpangaji,

marekebisho,


Kwa hiyo si kwamba kila laki 3 ya kodi ni profit yote pure, lakini bado real estate inaweza kuwa uwekezaji mzuri sana especially maeneo yanayokua haraka.
 
Hiyo ni investment ya muda mrefu. Hiyo ardhi kwa miaka ijayo ina thamani kubwa sana.

Elfu 60 ya mwaka 2000 iliweza kununua plot. Je, sasa hivi unaweza kupata plot kwa hiyo pesa?

Kama unataka biashara ya kukupa income ya haraka fanya biashara ila huko nako kuna kupoteza mtaji.
 
Tubuni njia nyingine za kuwekeza, kwenye mijengo ni kutupa pesa.
Ukishapata kimjengo cha kuishi achana na show offs ati unamiliki mijengo mingi

Ili kurudishwa milion 300 itachukua muda wa miaka 83.
Hapa hujahesabu gharama za ukarabati na muda mwingine wapangaji hakuna

Miaka 83 ni mingi mno washikaji duuuh
Miaka 83 unasubiri kupata m 300
Una umri gani na una elimu ipi kuhusiana na masuala ya pesa na uwekezaji?

Machalii mnajikuta wajuaji sana siku hizi.
Mwenyewe unajiona bonge la mbunifu kumbe kipato chako kwa mwezi pengine hakifiki hata 300k halafu unajikuta mjuaji wa kumuelekeza mwenye 300,000k aliyeamua kuwekeza surplus amount ya pesa yake kwenye ujenzi wa nyumba.

Miaka kadhaa iliyopita Quality Group walikuwa wanajenga majengo na kuyauza ndani ya muda mchache, unafikiri walikuwa hawa generate profit kubwa kwa kufanya hivyo?

Jadili mambo yaliyo ndani ya uwezo na uelewa wako.
Nje ya hapo ni kujianika uzuzu wako.
 
Back
Top Bottom