Unajisikiaje kuwa na mwanamke mwenye 'Wigi'

Unajisikiaje kuwa na mwanamke mwenye 'Wigi'

Sometimes tukiwashobokea mnataka tuwashobokee sanaaaa ndio nuelewe kama tumewashobokea. Tuko tofauti kidogo, wengine tunashoboka kidogo tu na ukiwa hujaelewa mshoboko wetu unataka tushoboke sana tunaona kama mnatichosha.

Mimi kiukweli haya mambo artificial siyapendi haswa na naweka hisia zangu wazi
Hujaelewa mshoboko[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila chakushangaza ukivaa wigi utasifiwa sana umependeza.....Tanzania.
Kama hakuna maslahi mengine ya msingi yatakayowekwa rehani akikwambia, wanaume wengi watapenda kuwa waaminifu kwa kukwambia ukweli kwamba hayo makatani hatuyapendi!
 
Ukiona unalo na hausemwi, au ulisemwa mara moja tu halafu kimya, sio kwamba linapendwa. Ni unavumiliwa tu kwa maslahi mapana ya mahusiano. Ila kimsingi hayo Mawigi yanakera, hasa yale ya rangi rangi. Yani unakuta mdada amevaa nyweli ina mchanganyiko wa bluu na njano! Yana harufu, yanawasha , bla bla bla.
Binafsi, napenda sana kushika nywele halisi. Akija amezichana, ameziremba, amezifunika siku hiyo ntazivuruga tu.
Haya maswala ya kutundika nywele kwenye msumali usiku na kuziokota asubuh hamna asee. Toshekeni na mionekano yenu.
 
Nawaambiaga sana dada zangu kuwa mambo wanafanya wakidhani wanapendeza machoni kwa wanaume kumbe ndo wanatuchukiza mno
1.Kuvaa mawigi
2.Kucha bandia
3.Kope bandia
4.kujichubua
5.LIPSTICK
6.KUACHA MAPAJA WAZI

hivi vitu huwa vinanikera mno, sijui ni nani aliyewaambia wakiwa wasafi tu wa kawaida hawatongozwi
yaani hata marashi tu mtu anajipulizia utadhani anajiandaa kuzikwa ukikaa mita nne toka alipo tayari ushapata kipanda uso, warembo wa hivyo nakaa nao mbali kabisa
Hapo kwenye kuacha mapaja wazi sio pabaya. Mie napapenda
 
Karibia vidume vyote hapa vimeponda wavaa mawigi, ninachojiuliza ni nani anadate nao huku mtaani? 😃😃 Acheni unafiki nyie viumbe
Mpaka mimi mnafiki???😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom