Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Angalia hili lidubwana hapa chini;
Sasa madudu ya kutisha kama haya, serikali yako ya Tanzania imeyanunua kwa ajili ya kuumiza wananchi wake, ambao sio kwamba wana makosa makubwa kama uasi dhidi ya serikali, ujambazi, uharamia, ujangili, ubakaji, uuaji wa watu wasio na hatia, utapeli, ufisadi nk, bali madudu kama haya ni kwa ajili ya kuwaumiza na kuwakomesha Watanzania ambao wanadai haki zao, na mara nyingi wakiamua kuzidai kwa kufanya maandamano ya amani.
Jiulize, kuna maandamano yeyote ya kudai haki ambayo Polisi wanakubali ni maandamano ya amani?
Au umewahi kusikia serikali yako ya Tanzania imenunua madudu kama haya ya kutisha kwa ajili ya kupambana na mafisadi, wauza rasilimali za taifa, majangiri katika mbga zet, panya road, nk?
Kimsingi, serikali ya Tanzania inakuambia hivi wewe unaetaki haki hasa katika mambo ya uchaguzi, ni bora uwe jambazi, jangiri, fisadi, mbakaji wa watoto, nk, kuliko uwe mtu anaedai haki yake ya uchaguzi hiru, kwa sababu madudu haya ni kwa ajili yako wewe unaetaka uchaguzi huru
Sasa jiulize, katika hali kama hiyo, unajiona mtu huru katika nchi yako?
Kumbuka, hili dudu la kutisha, lisipotumiwa dhidi yako, litatumiwa dhidi ya baba yako, mama yako, dada yako, mdogo wako, kaka yako, mjomba wako, binamu yako, jirani yako, rafiki yako, mfanya kazi mwenzako nk. Unaona ni sawa kwa sababu anaeumizwa si sawa?
Au hata jiulize, ni sawa serikali yako itumie madudu kama haya kwa Mtanzania mwenzako, unaesali kanisa moja au unaswali nae msikiti mmoja, kwa sababu tu yuko chama cha upinzani?
Hili sio dude serikali ya DRC inataka kutumia dhidi ya M23, ni dude serikali ya Tanzania inataka kutumia dhidi ya watu wake yenyewe! Kosa lao kubwa sana ni nini? Kusem tunataka kuwe na haki kwenye uchaguzi.
Ni sawa watuwanaojiita viongozi wa wananchi kuamuru Polisi watumie madudu haya dhidi ya wananchi katika nchi yao wenyewe kwa sababu tu wanadai mambo yafanyike kwa kufuata haki na usawa?