Unajua kwanini Wazungu wanapenda kusoma vitabu?

Mkuu unaona sasa what came out of that task...

Vitabu ni muhimu sana.... Nimekuwa msomaji sana siku za karibuni duuh sijui nilikuwa wapi siku zote, my life is changing for the better hata hapa nipo na kitabu changu nasoma.
Utafanya vizuri endapo utamwambukiza alau mtu mmoja hiyo tabia ya usomaji.
 
Sababu vimeandikwa lugha yao ya nyumbani, wewe unataka kuniambia Watoto wa Mama Ntilie haukukisoma? Machozi Jasho na Damu haukukisoma? Rais anamtaka Mke wangu haukukisoma? Vingeandikwa kigriki ungesoma?
Point
 
Kuhusu bei nakubali 100%kwetu watu masikini sana tunahangaika na shillings za kula,kitabu elfu 30 anasa,Mimi Kuna kitabu kinauzwa 120k,Kila nikifikiria gharama najikuta naghairi,
Hujaamua kufuatilia tu. Mimi nasoma vitabu vya tech na vingi Amazon vinaanzia laki moja ila nivapata free kwa pdf format kwenye magroup na online libraries.
 
Hawana stress, hivi huna Akira, unadaiwa kodi, Ada za shule, bado wazazi wanakutegemea hiko kitabu hata ukisoma utaelewa?
 
Hayo magazeti yote kwa sasa naweza kusema yamekuwa replaced na mitandao kama ifuatavyo.
1.Sani - Facebook
2.Tabasamu- Instagram
3. Bongo - Twitter/X
 
Kitabu kinaweza kuwa njia ya kupunguza stress. Kudaiwa kodi,ada ni vitu vya kawaida kwenye maisha.
Mkuu vitabu ni vizuri mno ila possibility ya Mtanzania wa hali ya chini kuwa na muda wa kusoma vitabu kwa sisi wapambanaji ni ngumu. Wenye uchumi stable kamba wazee walioko kwenye cabinet na mifumo ya hela ni rahisi kusoma.
 
Mkuu vitabu ni vizuri mno ila possibility ya Mtanzania wa hali ya chini kuwa na muda wa kusoma vitabu kwa sisi wapambanaji ni ngumu. Wenye uchumi stable kamba wazee walioko kwenye cabinet na mifumo ya hela ni rahisi kusoma.
lakini ajabu zaidi hata hao stable's hawasomi. reading culture ni utamaduni mgumu kwa watu wa ukimani
 
Hao ni makafiri, na makafir wote yao ni jeham ya kiama, hakika Quran ndio kitabu tukufu kinapaswa kusomwa na bin adam yeyote chini ya jua
 
Mkuu vitabu ni vizuri mno ila possibility ya Mtanzania wa hali ya chini kuwa na muda wa kusoma vitabu kwa sisi wapambanaji ni ngumu. Wenye uchumi stable kamba wazee walioko kwenye cabinet na mifumo ya hela ni rahisi kusoma.
Ni tabia tu. Kusoma inaweza kuwa ndio muda wako wa kupumzika. Hao watu wa chini uwasemao ndio wanaongoza kukaa vijiweni.
Huhitaji muda mrefu kusoma hata nusu saa, pages 2/3 kitabu kimoja kwa mwezi inatosha.
 
Kusoma vitabu ni tabia ambayo ukishaijenga hauwezi kuiacha.

Wala haina uhusiano na uchumi kuwa tajiri ,uchumi wa kati au uchumi wa chini.


Mimi binafsi nimeanza kusoma vitabu kupitia majarida ya FEMA.

Ila niongee tu ukweli vitabu vizuri vineandikiwa katika lugha ya kiingereza na hii yaweza kuwa kikwazo watu kutokusoma vitabu Sana.

Wazungu wanaelewa msingi mkubwa wa maarifa unapatikana vitabuni. Maana vitabu ni experience za wat u za maisha na utafiti.


Wasomi ambao hawajitambui ni kwasababu hawasomi vitabu
 
Kwa mara ya kwanza naona uzi wa kuwasifia wazungu bila kuponda Waafrika ndani yake. Umetumia lugha nzuri
 
Ukimkuta Mzungu ana Maktaba kubwa imejaa Vitabu vya Kiswahili nitafute nikulipe dollar 100,000
Mkuu lugha siyo kii ngereza na kiswahili tu, ziko nyingi. Ni kawaida kabisa kumkuta mfaransa ana vitabu vilivyoandikwa kwa kiingereza, kispaniola na kiitaliano. Au hoja yako nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…