Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Onesha hayo "" makosa* uliyosema umeyaona kwenye Qur'an.
 
Acha kufuru kijana. Ni bora kukaa kimya kuliko kuleta ujuaji. Unajua usipende kuleta ufukunyuku usio kua na maana. Wapo watu zaidi ya wewe walitokea kukashifu ukuu wa Mungu mwenye enzi yote mwisho wa siku walikuja kugundua kuwa Mungu ni zaidi na wanavofikiria kibinadamu.
Watu kumwomba Mungu usije ukadhani ni wajinga. Mambo ya Rohoni usiyajadili mwilini hutakaa kuelewa.usitumie akili yako ya kibinadamu kumjadili Mungu.
Ndo maana Biblia huwa inasomwa kwa msaada wa roho wa Mungu ukisema uisome kama gazeti hutaweza na hutakaa uielewe. Ulishajiuliza kwanini mtu anakuambia nimesoma vitabu vingi tena vyenye kurasa nyingi..linapokuja swala biblia hata kumaliza kurasa 5 ni shuguli sababu biblia haijaandikwa kwa akili za kibinadamu kuna vita vya kiroho lazima ushinde ndio uweze soma biblia.
Take care Maada kama hizi ni bora ukae nazo mwenyewe! Swala la kiimani ni pana sana na lina nguvu sana.
 
Kwa nini imani ya Mungu inajengwa katika vitisho kama hivi? Kwa nini tutishane ili tumkubali?
Wanaokutisha ni wale ambao bado haujaujua ukuu wa Mungu vizuri.Mungu sio wa vitisho. Mungu ni wa rehema na fadhili zake ni za Milele.
Kuna hawa watumishi feki ndio huwa wanapandikiza chuki na vitisho kwa waumini wao ili mradi wawateke kifikra sababu watu hawasomi biblia na kutaka kuujua ukuu wa Mungu.
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Kabisa kaleta uzi wa kitoto sana. Anahitaji kueleweshwa kuwa uzi wake ni wa kitoto sana.
 
Kwanini kuhoji dhana yenye utata kuhusu mungu iwe ujinga,?

Ujinga ni nini?
Aiseeh umeleta utoto sana. Kwa kukushauri tu kaa na imani yako hiyo usitake kuaminisha watu ujinga wako. Mambo ya Mungu huwa hajadiliwi kama unavojadili simba na yanga. unapoanza kumtaja Mungu ni mambo ya rohoni haya hayatakiwi kujadiliwa kiwepesi wepesi.
Kijana kabla ya kuleta huu uzi ulikula kweli usije ukakuta njaa yako ilianzia kichwani ndio ikaenda tumboni ndio maana unatuletea utoto huu
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Hivi kwanini watu wasio na hoja hukimbilia kuisema FB, Jibu swali huwezi vunga FB ndio wapi sasa? Sidhani kama wewe ni Mwelevu kuliko FB wote ni vile tu unajimwambafai. Afu mbona JF penyewe viraza wote tu ni bando lako unaingia au wanaingilia akili uku?
 
Naamin Mungu yupo kulingana na Iman zetu za kidini,
Lakin si Dhambi kuhoji uwepo wake na kujifunza kwa undani bila kubase katika imani.
Kuamin bila hoja ni utumwa wa Imani.
 
Mungu ni super natural power...
Nyie ndo mnatujazia Wachungaji wahuni mtaan kwa majibu mepesi kama haya. SupaNachuro ndio nani? Maswala ya Iman si thabit inategemea tu ubongo wako umeuwekaje. Yaan hakuna Warantee ya Kuhalalisha uwepo wa yanayoaminika.
 
Jifunze kuandika vizuri then uje na hoja ya maana,,nitakujibu ipasavyo.
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Sema huna Hoja za kumjibu sio unaleta Hofu zako za kidini na kiimani.

Unashindwa kujibu hoja unasema Uzi hauna kichwa wala miguu?



Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Huna hoja wewe!!!

Ulicho andika hapa ni Hofu zako za kidini na ki imani...unataka kutisha watu kwamba kuhoji uwepo wa Mungu ni kosa?

Hizo hofu zako za kidini na kiimani achia huko huko kanisani au msikitini..

Aliye kwambia Mungu hajadiliwi ni nani?


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Umenena vema huyu kijana anakuwa kama yule kijana aliyekuwa anatafuta kujua kuhusu utatu mtakatibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…