Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.

Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.

tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)

Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.

tuliza akili kijana!
Onesha hayo "" makosa* uliyosema umeyaona kwenye Qur'an.
 
Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
Acha kufuru kijana. Ni bora kukaa kimya kuliko kuleta ujuaji. Unajua usipende kuleta ufukunyuku usio kua na maana. Wapo watu zaidi ya wewe walitokea kukashifu ukuu wa Mungu mwenye enzi yote mwisho wa siku walikuja kugundua kuwa Mungu ni zaidi na wanavofikiria kibinadamu.
Watu kumwomba Mungu usije ukadhani ni wajinga. Mambo ya Rohoni usiyajadili mwilini hutakaa kuelewa.usitumie akili yako ya kibinadamu kumjadili Mungu.
Ndo maana Biblia huwa inasomwa kwa msaada wa roho wa Mungu ukisema uisome kama gazeti hutaweza na hutakaa uielewe. Ulishajiuliza kwanini mtu anakuambia nimesoma vitabu vingi tena vyenye kurasa nyingi..linapokuja swala biblia hata kumaliza kurasa 5 ni shuguli sababu biblia haijaandikwa kwa akili za kibinadamu kuna vita vya kiroho lazima ushinde ndio uweze soma biblia.
Take care Maada kama hizi ni bora ukae nazo mwenyewe! Swala la kiimani ni pana sana na lina nguvu sana.
 
Kwa nini imani ya Mungu inajengwa katika vitisho kama hivi? Kwa nini tutishane ili tumkubali?
Wanaokutisha ni wale ambao bado haujaujua ukuu wa Mungu vizuri.Mungu sio wa vitisho. Mungu ni wa rehema na fadhili zake ni za Milele.
Kuna hawa watumishi feki ndio huwa wanapandikiza chuki na vitisho kwa waumini wao ili mradi wawateke kifikra sababu watu hawasomi biblia na kutaka kuujua ukuu wa Mungu.
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Kabisa kaleta uzi wa kitoto sana. Anahitaji kueleweshwa kuwa uzi wake ni wa kitoto sana.
 
Kwanini kuhoji dhana yenye utata kuhusu mungu iwe ujinga,?

Ujinga ni nini?
Aiseeh umeleta utoto sana. Kwa kukushauri tu kaa na imani yako hiyo usitake kuaminisha watu ujinga wako. Mambo ya Mungu huwa hajadiliwi kama unavojadili simba na yanga. unapoanza kumtaja Mungu ni mambo ya rohoni haya hayatakiwi kujadiliwa kiwepesi wepesi.
Kijana kabla ya kuleta huu uzi ulikula kweli usije ukakuta njaa yako ilianzia kichwani ndio ikaenda tumboni ndio maana unatuletea utoto huu
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Hivi kwanini watu wasio na hoja hukimbilia kuisema FB, Jibu swali huwezi vunga FB ndio wapi sasa? Sidhani kama wewe ni Mwelevu kuliko FB wote ni vile tu unajimwambafai. Afu mbona JF penyewe viraza wote tu ni bando lako unaingia au wanaingilia akili uku?
 
Naamin Mungu yupo kulingana na Iman zetu za kidini,
Lakin si Dhambi kuhoji uwepo wake na kujifunza kwa undani bila kubase katika imani.
Kuamin bila hoja ni utumwa wa Imani.
 
Mungu ni super natural power...
Nyie ndo mnatujazia Wachungaji wahuni mtaan kwa majibu mepesi kama haya. SupaNachuro ndio nani? Maswala ya Iman si thabit inategemea tu ubongo wako umeuwekaje. Yaan hakuna Warantee ya Kuhalalisha uwepo wa yanayoaminika.
 
Hivi kwanini watu wasio na hoja hukimbilia kuisema FB, Jibu swali huwezi vunga FB ndio wapi sasa? Sidhani kama wewe ni Mwelevu kuliko FB wote ni vile tu unajimwambafai. Afu mbona JF penyewe viraza wote tu ni bando lako unaingia au wanaingilia akili uku?
Jifunze kuandika vizuri then uje na hoja ya maana,,nitakujibu ipasavyo.
 
Jinsi uulizaji wako ulivyo wa kitoto na usio wa kufikirisha napenda kukushauri achana na hili jukwaa halikufai uzi kama huu usio na kichwa wala miguu kapost FB Uko utapata wa kukuunga hoja yako
Sema huna Hoja za kumjibu sio unaleta Hofu zako za kidini na kiimani.

Unashindwa kujibu hoja unasema Uzi hauna kichwa wala miguu?



Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Aiseeh umeleta utoto sana. Kwa kukushauri tu kaa na imani yako hiyo usitake kuaminisha watu ujinga wako. Mambo ya Mungu huwa hajadiliwi kama unavojadili simba na yanga. unapoanza kumtaja Mungu ni mambo ya rohoni haya hayatakiwi kujadiliwa kiwepesi wepesi.
Kijana kabla ya kuleta huu uzi ulikula kweli usije ukakuta njaa yako ilianzia kichwani ndio ikaenda tumboni ndio maana unatuletea utoto huu
Huna hoja wewe!!!

Ulicho andika hapa ni Hofu zako za kidini na ki imani...unataka kutisha watu kwamba kuhoji uwepo wa Mungu ni kosa?

Hizo hofu zako za kidini na kiimani achia huko huko kanisani au msikitini..

Aliye kwambia Mungu hajadiliwi ni nani?


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ulishawahi kuutafakari muundo wa mwili wako unavofanya kazi?
1. Jiulize jinsi macho yako yanavoweza kutazama na kutofautisha rangi
2. Ulimi wako unawezaje kutofautisha chungu chachu na tamu
3. Mpangilio wa vitu[moyo, mapafu, ini, nk] katika mwili wako nan alivipanga?
4. Mpangilio wa nerve sysytem na jinsi znavofanya kazi nani alitengeneza?
5. Fikiria unakula ugali mwili unatenganisha kinachohitajika na kisicho hitajika kinatolewa kama kinyesi halafu unasema hakuna mungu.
Tafakari kijana
Umenena vema huyu kijana anakuwa kama yule kijana aliyekuwa anatafuta kujua kuhusu utatu mtakatibu
 
Back
Top Bottom