Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Wewe ulizaliwa unajua kila kitu?
Najadili ili nijifunze.
Kuna kujadili na kujifunza kijana, tofautisha haya maneno na ujue namna ya kuyatumia. Mjadala ni kwa wenye hoja na kufahamu kile wanachokijadili, Sasa wewe huna sifa za kujadili hii kadhia, sababu hujui yaani unatakiwa uulize maswali ujibiwe na wale wenye kujua.
 
Wapi nimesema najua??? Kwanza kitendo cha wewe kuniita mpumbavu nisiyejua, tayari kimeashiria wewe sio mpumbavu na unayejua...sasa kwanini unitukane mimi kuwa najiona najua huku wewe mwenyewe kwa kusema hivyo tu, tayari umeojiona kuwa wewe ndo unajua??
Kuonyesha kwamba unajua siyo mpaka useme au uandike, Bali namna ya uwasilishaji wako. Hili weka akilini kwanza.

Sijakutukana bali nimekupa stahiki yako, sisi Waswahili matusi tunawajua Mpumbavu si tusi. Kwahiyo nitake radhi kwa kunizulia uongo.

Hiki ninacho kijadili nakijua, Naam.
Upepo unavuma na kusababisha miti kuanguka, Hapo mtu akiuliza nani kaangusha mti atakuwa sahihi?? Sio kila kitu kinakuwa caused na kitu chenye akili.
DNA haina akili lakini inacode kila kitu kwenye kiumbe.
Jitahidi uwe unasoma vizuri kwanza ninacho koandika ili uepuke makosa kama haya uliyo yafanya ya kuchukua nukta moja na kuacha nyingine kadhaa. Ukiangalia sifa anuani za "Nani ?" nilizo zitaja ni zaidi ya Moja, nimesema "Nani ?" ana maarifa, nani anajua, nani ana malengo, nani ana sanifu. Sasa jihukumu mwenyewe Upepo una unasanifu ? Upepo unajua ? Upepo una malengo ? Upepo una maarifa ?

Achana na habari za DNA huo ni utoto mwingine ? Ushasema zipo kwenye mwili wa kiumbe ? Tayari kiumbe hicho kina mfumo na hizo DNA mnaziamini nyinyi sababu ni zao la fikra na mtazamo wa mtu. Hili ukitaka tutalijadili.

Vijana muwe mnasoma haya mambo kiundani na myajue.
 
Kama huna uhakika kuwa si MUNGU unahakika kuwa ni nani? MUNGU anatajwa kwa sababu ww usiyetaka atajwe hujasema ni nani aliyefanya haya . Ukitaka watu waseme si MUNGU aliyefanya haya sema aliyeyafanya. Kama hakuna aliyefanya basi MUNGU ataendelea kuwepo hata kama kuna wasiotaka awepo.
Mimi sina hakika na chochote kile.
Kwahyo unaponiambia ni Mungu natamani pia unithibitishie ili niwe na uhakika.

Tatizo la sisi homo sapiens, hatupendi kukubali kukosa majibu hivyo kila kitu tunakitafutia jibu (Hili ni jambo zuri kuhusu sisi) lakini pia tuko radhi tukubali jibu la uongo kuliko kutokuwa na jibu kabisa (Hili ndio jambo baya kuhusu sisi)
 
Kuna kujadili na kujifunza kijana, tofautisha haya maneno na ujue namna ya kuyatumia. Mjadala ni kwa wenye hoja na kufahamu kile wanachokijadili, Sasa wewe huna sifa za kujadili hii kadhia, sababu hujui yaani unatakiwa uulize maswali ujibiwe na wale wenye kujua.
Yes, na nipo kujifunza ndio maana kila post huu uzi nimeweka swali
 
Sawa, Karibu uthibitishe.
Nakuthibitishia kwa namna tatu.

1. Self evident truth.
2. Mazingira
3. Ufunuo

Self evident Truth
Uwepo wa kitu fulani huonyesha uwepo wa yule aliyesababisha kuwepo kitu husika. Ukiona simu ? Unapata vitu vingapi au unaona nini katika simu hiyo, bila shaka unaona vitu vifuatavyo au utajua vitu vifuatavyo. Yaani yupo msababishaji, mwenye Elimu ya kitu husika, mwenye malengo ya kufanya kitu husika kiwepo yaani kwanini kimekuwepo, ni msanifu mwenye maarifa. Unakubali hili ?

Jibu la swali lako au ithibati ni hii je Ulimwengu umetokea pasi na chochote au umejiumba ?

Naendelea ...
 
Kuonyesha kwamba unajua siyo mpaka useme au uandike, Bali namna ya uwasilishaji wako. Hili weka akilini kwanza.

Sijakutukana bali nimekupa stahiki yako, sisi Waswahili matusi tunawajua Mpumbavu si tusi. Kwahiyo nitake radhi kwa kunizulia uongo.

Hiki ninacho kijadili nakijua, Naam.
Mimi kujionesha najua umesema ni upumbavu, ila wewe unapisema unajua ndiyo hekima sio?
Jitahidi uwe unasoma vizuri kwanza ninacho koandika ili uepuke makosa kama haya uliyo yafanya ya kuchukua nukta moja na kuacha nyingine kadhaa. Ukiangalia sifa anuani za "Nani ?" nilizo zitaja ni zaidi ya Moja, nimesema "Nani ?" ana maarifa, nani anajua, nani ana malengo, nani ana sanifu. Sasa jihukumu mwenyewe Upepo una unasanifu ? Upepo unajua ? Upepo una malengo ? Upepo una maarifa ?
Upepo hauna maarifa, kwahiyo kumbe tukikuta mti umeanguka porini hatupaswi kuuliza 'Nani' kauangusha, maana hata upepo usio na maarifa unaweza kuangusha mti.
Achana na habari za DNA huo ni utoto mwingine ? Ushasema zipo kwenye mwili wa kiumbe ? Tayari kiumbe hicho kina mfumo na hizo DNA mnaziamini nyinyi sababu ni zao la fikra na mtazamo wa mtu. Hili ukitaka tutalijadili.

Vijana muwe mnasoma haya mambo kiundani na myajue.
Okay, tukifikaga stage ambayo mnaikataa sayansi iliyothibitika ili kutetea imani zenu huwa ndiyo naishia hapo.
 
Jibu 1. Binadamu anayeamini mungu yupi? Historia ya MUNGU ni tofauti tofauti kulingana na imani za binadamu.

Kuna ambaye anamuongelea MUNGU wa biblia na Quran, yupo anayeongelea mizimu, ng'ombe n.k. Sasa unataka kujua walioanza kumuongelea yupi?
Swali langu limeenea halijajifunga kwenye Mungu Fulani. Kwahiyo usiulize maswali yasiyo na msingi mbele ya swali la ujumla. Jibu swali nililo kuuliza.

Umesema mwanadamu amemuumba Mungu baada ya kushindwa kupata majibu ya kifo na mengine Sasa ndiyo uniambie lini kwa mara ya kwanza, Sasa unapo uliza kwamba ni Mungu yupi naona unaletwa utoto, swali langu kwa mara ya kwanza. Sababu siyo sawa kwamba Ubudha ulianza muda sawa na Ukristo au Uyahudi au Uhindu. Kwahiyo jibu swali langu.
 
Nakuthibitishia kwa namna tatu.

1. Self evident truth.
2. Mazingira
3. Ufunuo

Self evident Truth
Uwepo wa kitu fulani huonyesha uwepo wa yule aliyesababisha kuwepo kitu husika. Ukiona simu ? Unapata vitu vingapi au unaona nini katika simu hiyo, bila shaka unaona vitu vifuatavyo au utajua vitu vifuatavyo. Yaani yupo msababishaji, mwenye Elimu ya kitu husika, mwenye malengo ya kufanya kitu husika kiwepo yaani kwanini kimekuwepo, ni msanifu mwenye maarifa. Unakubali hili ?

Jibu la swali lako au ithibati ni hii je Ulimwengu umetokea pasi na chochote au umejiumba ?

Naendelea ...

Uwepo wa kitu fulani huonyesha uwepo wa yule aliyesababisha kuwepo kitu husika
Okay, Mungu yupo...inamaanisha uwepo wake huonyesha uwepo wa yule aliyemsababisha.....Nani alimsababisha Mungu kuwepo???
 
Tatizo kubwa ni watu kutokujua Mungu ni kitu gani.
Mungu ndiyo asili ya yote (nature).
Siyo kiumbe.
 
Jibu 2. Hatujajua ndo maana bado tumehitimisha yote katika concept ya lazima kuna chanzo cha haya yaliyopo, hicho chanzo ndiye MUNGU. Kama ww una ukweli ulio na uhalisia badala ya kiimani zaidi ya huu tulionao uweke wazi.
Umekisoma vizuri ulicho kiandika ? Usiwasemee wengine sababu ulicho kiandika kimeonyesha hujielewi unahitimisha vipi jambo pasi na Elimu ?

Kwani Imani siyo uhalisia ? Weka sawa kwanza kuhusu Imani, maana naona unataka kuitenganisha Imani na uhalisia. Fanya hivyo kwanza Kisha niendelee hapa napoishia.
 
Okay, Mungu yupo...inamaanisha uwepo wake huonyesha uwepo wa yule aliyemsababisha.....Nani alimsababisha Mungu kuwepo???
Unaamini Kuna "Infinity Series" ?

Kila kitu kina chanzo isipokuwa Mola pekee, sababu hakuna kinachofanya awepo aliyefanya kuwepo kwa kila kitu, haya yatakuwa ni matumizi mabaya ya akili na kufikiria kitoto.
 
Mimi kujionesha najua umesema ni upumbavu, ila wewe unapisema unajua ndiyo hekima sio?
Kuna kujionyesha kujua na Kuna kujua na kujua kama unajua. Kijana jifunze maana za maneno na kutofautisha kauli. Sasa unajadiliana vipi na Mimi hali ya kuwa hata kutofautisha maana za maneno hujui ?
 
Okay, tukifikaga stage ambayo mnaikataa sayansi iliyothibitika ili kutetea imani zenu huwa ndiyo naishia hapo.
Hapa ndipo huwa mnapoteana vijana. Nani amepinga Sayansi ? Mimi naishi katika Sayansi ila kuna ngano na visasili vya Sayansi yaani uongo upo mwingi kuliko ukweli. Kwahiyo wewe Jenga hoja kama unaijua Sayansi.

Mtu kama wewe unaonyesha wazi kabisa huijui Sayansi ndiyo unasema vitu vimethibitishwa na Sayansi. Wewe tu mfano mdogo unao ushahidi wa Kisayansi unaonyesha ya kuwa Dunia inazunguka katika Muhimili wake ? Yaani kwa kutumia zile hatua za ithibati za Kisayansi ? Jibu sahihi hakuna, Sasa kwanini unaamini ya kuwa Dunia inazunguka ?

Sasa acheni uoga vijana tunawasaidia kufikiria kwa usahihi.
 
Upepo hauna maarifa, kwahiyo kumbe tukikuta mti umeanguka porini hatupaswi kuuliza 'Nani' kauangusha, maana hata upepo usio na maarifa unaweza kuangusha mti.
Jibu la swali lako litakujulisha ni nini au nani.
 
Mungu yupo,ametupotezea tujiendee tu,
Vitabu vimechakachuliwa ila kila mmoja amepewa utashi wa kuchanganua mambo,sema wakristo wengi hawataki kujifunza wamekariri bila kutafakari..

Ameumbwa na nani?ni sawa kuhoji ila liko nje ya upeo wetu...hata udadavue vipi uwezi kupata jibu Mungu aliumbwa na nani.
 
Wapi nimesema ni " nini"?
Kwanini unadhani lazima ' nani' mwenye maarifa ndio asababishe uhai na so michakato tu ya kisayansi ambayo haijagundulika?
Sababu sayansi haina uwezo wa kutoa uhai wa kiumbe. Ushawahi kusikia Wanasayansi wametengeneza hata bawa la Mbu ? Si unamjua Mbu ? Sayansi haipo kumpa mtu ukweli huu ndiyo ukweli ulivyo.
 
Back
Top Bottom