Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Huyo Mungu Mbambaishaji Unayemsemea Ni Kutokana Na Uelewa Wako Mdogo wa Mambo.Tena Usisema Umesoma Vizuri Qur'an.Kwan Qur'an Imeeleza Na Hakuna Palikosewa Kimantiki.
Ungekuwa Umeisoma Vizur Qur'an Majibu Yako
Qur'an 2:255.

Pia ww Umuelewa Mungu Umekuwa Nani,Sifa za Mungu Ni za Kipekee Kumtofautisha Na Mwanadamu Hicho Kinafanya Usimuelewe Mungu.

Kama Ukisoma Kwenye Biblia Ndo Utagundua Mungu Mbabaishaji Yupo
Mwanzo 32:24-28.Ila Sio Kwenye Qur'an

Rudi Ukasome Vizuri Umekurupuka Kuandika Uzi Sidhan Hata Kama Umefatilia Kuhusu Mungu Na Hujui Lolote Pia
 
Isa 40:28 SUV​

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Wewe endelea kumchunguza Mungu uone kama utaweza
Haina haja ya kutaka kujua kaumbwa au hakuumbwa. Ninavyojua Mimi na kuamini yeye ni WA milele na hakuumbwa inatosha

Kumbukumbu la Torati 29:29 (KJV)

Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
 
Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
Inna Lilah waina ilaih ragiun

Msiba mkubwa huu ndugu yng
 
Unaamini Kuna "Infinity Series" ?
Ndiyo infinity series zipo.
Hata 1+2+3... Ni infinity series.
Kila kitu kina chanzo isipokuwa Mola pekee,
Ulianza kwa kusema sheria kali sijui uliitolea wapi, kwamba kila kilichopo lazima kina chanzo, nkakwambia Mungu yupo ina maana ana chanzo??

Ukabadili na kusema yeye hana chanzo, Kumbe ile sentensi ulikosea...kumbe sio kila kilichopo kina chanzo.

Na kama hii sheria ni batili, ina maana inawezekana hata vitu vikawepo bila chanzo (mfano Mungu)

Na kama sio kila kilichopo kina chanzo (kwa mfano Mungu yupo na haihitaji chanzo) basi kumbe inawezekana hata vitu vikawepo bila chanzo.

Maana kumbe sheria yako ni batili.

Nini kinazuia vitu vingine visiwepo bila chanzo kama Mungu ameweza kuwepo bila chanzo?
.sababu hakuna kinachofanya awepo aliyefanya kuwepo kwa kila kitu, haya yatakuwa ni matumizi mabaya ya akili na kufikiria kitoto.
Hapo nilipopabold ukipathibitisha, itasaidia sana hata kutetea hoja yako ya juu.
Ni nani aliyefanya? Kwa ushahidi upi??
 
Kuna kujionyesha kujua na Kuna kujua na kujua kama unajua. Kijana jifunze maana za maneno na kutofautisha kauli. Sasa unajadiliana vipi na Mimi hali ya kuwa hata kutofautisha maana za maneno hujui ?
Kitendo cha kusema mimi najua tayari ni kujionesha unajua.
Na kama hujui unachodhani unajua, huwezi kujua kama hujui bali utajua kuwa unajua.

Kwahyo hata wewe huna tofauti na unachokikemea.
 
Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.

Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.

tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)

Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.

tuliza akili kijana!
Mie namwelewa kabisa, kama kweli wewe ni mfuatiliaji na ukasema ukweli lazima ukubali jamaa anaongea kitu reasonable, mmefundishwa mungu na mzungu hata miaka 200 haijapita lakini dunia ipo millions of years, babu zako walikuwa wanaamini nini kabla ya mungu wa mzungu na mwarabu, ukristo na uislam ni dini ambazo wafrica mnazijua kwa sababu ya kutawaliwa na wakoloni na hakuna sababu nyingine yeyote, ukienda sehemu nyingine kama Asia ambako kuna watu wengi kuliko hata Africa kule wanaamini mungu tofauti kabisa mnavyojua, idea ya mungu ni creation ya mwanadamu tuu hata babu zetu walikuwa na mungu wao ambaye ni tofauti na huyu tuliyeletewa na mzungu
 
Hapa ndipo huwa mnapoteana vijana. Nani amepinga Sayansi ? Mimi naishi katika Sayansi ila kuna ngano na visasili vya Sayansi yaani uongo upo mwingi kuliko ukweli. Kwahiyo wewe Jenga hoja kama unaijua Sayansi.

Mtu kama wewe unaonyesha wazi kabisa huijui Sayansi ndiyo unasema vitu vimethibitishwa na Sayansi. Wewe tu mfano mdogo unao ushahidi wa Kisayansi unaonyesha ya kuwa Dunia inazunguka katika Muhimili wake ? Yaani kwa kutumia zile hatua za ithibati za Kisayansi ? Jibu sahihi hakuna, Sasa kwanini unaamini ya kuwa Dunia inazunguka ?

Sasa acheni uoga vijana tunawasaidia kufikiria kwa usahihi.
Kila mtu ana mpaka wake, mimi nishajiwekea mpaka kuwa siwezi kupoteza muda wangu kubishana na watu wanaopinga sayansi.

Watu wanaomini sijui dunia ni flat, dunia ina miaka 6000, Dunia haizunguki jua nk. Huwa sipotezi Muda wangu mtukufu kujadiliana nao hayo maswala....utanisamehe mkuu, Huo ni mpaka wangu binafsi.
 
Jibu la swali lako litakujulisha ni nini au nani.
Ahaa kumbe jibu linaweza kuwa nini au nani.
Sasa kwanini uulize nani??
Kwanini usiulize ni nani au nini??

Maana ukiuliza nani tu, umeshalimit kwamba unataka utajiwe mtu mwenye akili, elimu, maarifa.
 
Nawahakikishia ndugu zangu watanzania idea ya Mungu ni creation ya mwanadamu tuu, imagine tungetawaliwa na wahindi au mchina leo majority ya watanzania tungekuwa wahindu au mabudha, na hao wote mungu wao ni tofauti na wa waislam au wakristo na hata wanachoamini ni tofauti kabisa
 
Mtu anaejifungia kwenye box la elimu moja tu ya sayansi pekee Ili kupata majibu ya hoja zake huwa kajifunga kwenye ufahamu.
Utadhani sayansi pekee ndio jawabu la KILA kitu
 
Wapi nimesema kwamba wewe umesema "nini ?
Kwanini unanihoji kuelezea kitu ambacho sijakitolea madai?
Unaniuliza " nini" ina sifa gani wakati hakuna mahala nimeitaja hiyo " nini"
 
Mpumbavu tu ndiye anaweza sema Mungu hayupo
Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
 
Mpumbavu tu ndiye anaweza sema Mungu hayupo
Hivyo unaamini kwa kuogopa kuitwa mpumbavu? Kama yupo kwanini aniache niwe mpumbavu na mwingine awe mwelewa? Unaweza kuthibitisha kuwa yupo?
 
Mtu anaejifungia kwenye box la elimu moja tu ya sayansi pekee Ili kupata majibu ya hoja zake huwa kajifunga kwenye ufahamu.
Utadhani sayansi pekee ndio jawabu la KILA kitu
Niambie ni wapi tutaupata ukweli.
 
Niambie ni wapi tutaupata ukweli.
Zipo elimu nyingi tu nje ya sayansi zenye uwezo wa kutoa majibu ambayo sayansi imeshindwa kutupa.
Sayansi imeweza kujibu 20% tu ya mambo yaliyopo Dunia.
 
Isa 40:28 SUV​

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Wewe endelea kumchunguza Mungu uone kama utaweza
Haina haja ya kutaka kujua kaumbwa au hakuumbwa. Ninavyojua Mimi na kuamini yeye ni WA milele na hakuumbwa inatosha

Kumbukumbu la Torati 29:29 (KJV)

Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
Unajua kuwa hii post yako inathibitisha madai yangu kuwa dhana ya mungu inasababishwa na uvivu wa kufikiri?

Kwanini kuamini kuwa mungu alikuumba inatosha?
Kwanini hutakiwi kuhoji mungu asili yake ni ipi?
 
Back
Top Bottom