Kazakh destroyer
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 3,278
- 6,843
Nakupa mtihani mwepesi, usiku wa leo toka nje kisha tazama anga halafu zingatia macho yako yatacover kiasi gani katika ukubwa wa mbingu halafu geuka nyuma tizama mbingu bado inaendelea na huwezi kuidhibiti kwa macho yako, ukilijua hilo basi tambua aliyeiumba hiyo mbingu ana haki zaidi ya kuwa mkubwa na mtukufu.Sasa na yeye Mungu kwanini ajiweke complex hivo? Kwann asirahisishie maisha viumbe wake kama mtoa mada ili wamwelewe kiwepesi.
"....na ninyi hamtomuona mola wenu mpaka mfe {kwanza}.." hadithi sahihi.
Unachopaswa kujua mkuu ni kwamba hadhi, cheo, utukufu na mamlaka aliyonayo muumba wetu ni makubwa sana na ya kiwango kisicho na mfano kwa viumbe vyake, na huku kutokumuona wala kumjua sasa hivi ndio salama yetu kwani lau angejidhihirisha tumuone basi tungeangamia sote kutokana na ukali wa nuru yake.
"hayamdiriki yeye macho{kumzunguka} na yeye anayadiriki macho, na yeye ndiye mwenye kuyajua ya ndani zaidi, mtambuzi wa habari"
Quran 6:103