Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Hilo swali utajiuliza na ninakuhakikishia hautapata jibu, utawauliza wanafalsafa hautapata jibu! Kibaya zaidi utawauliza wanateolojia(waliomjifunza Mungu) na bado hawatakupa jibu!!

Kwa hiyo mimi nikukatishe tamaa kabisa kwamba hakuna jibu la swali lako.
 
Hili nshakujibu. Nshakuambia mfano wa series za namba 1, 2, 3, 4...hazina mwisho kwasababu unaweza ukaendelea kuongezea Moja mbele milele na milele na usifike mwisho.
Kama unadai zina mwisho utaje apa, ni namba gani hiyo ya mwisho?? Mimi ntakuambia ijumlishe na moja.
Soma swali langu vizuri.
 
Mwanadamu bhana kapewa pumzi baada ya kumshukuru Muumba wake yeye anamkufuru kama hivi

Subiri siku iyo pumzi ikate ndo utamjua Mungu vizuri kma saivi hutaki kumjua

Mtu akishakufa ndio Mungu hujulikana, kwahiyo tukiwa hai hawezi kujulikana mpaka pumzi ikate?

#YNWA
 
Huo ni uamuzi wake yeye Mwenyewe[Muumba] na yeye tu ndo anajua kwanini unaumba hivo.
Hivi wewe unajua siku yako ya kufa? Unajua kifo chako kitakuaje?
Hicho kifo nani au nini kilikiweka?

Kama huwezi kumjibia KWANINI UNAMTETEA?
Mwache ajitetee mwenyewe.

#YNWA
 
Ukisema MUNGU aliumbwa na binadamu njoo na majibu yote yenye utata kuhusu ulimwengu na mauti.

Kama huna majibu yaliyopelekea watu kuamini uwepo wa MUNGU ni kupoteza muda.

NB: Watu wanaamini kuhusu MUNGU sababu binadamu amefeli kujibu ulimwengu ni nn na kifo ni nn na vimetokana na nn.

Kwanini huwa mnapenda kutumia KIFO na KUKATIKA PUMZI kama defend ya uwepo wa Mungu?

Hatuna point nyengine ZAIDI YA KIFO?

#YNWA
 
Na uzima wa Milele ndio Huu, Wakujue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yohana 17.3.

Ila Quran.
Imeandikwa na Jesuit+ Mohamed+ Shetani+ Majini.

MJUE SANA MUNGU.
SOMA SANA BIBLIA.

Kila mwenye dini HUVUTIA PAKWAKE.

Kwanini Mungu asiweke mambo kirahisi ili tujue dini ya kweli kirahisii bila misuguano?

#YNWA
 
Utoto wako umeanza kwa kusema Mungu ameumbwa na mwanadamu na nikikuuliza binadamu ametoka wapi au kaletwa na nani?? Si ndo utaniletea hoja za mtoto wa chekechea.

"Watu wa Mungu" Hamuwezi kujibu hoja bila kum "attack" mtoa hoja?
Hamuoni hata huyo Mnayemyetea anawashangaa?

#YNWA
 
Huna lolote unalojua wewe pamoja na kufatilia hili jukwaa kwa miaka miwili bado hujapata kitu cha kutushawishi zaidi ya kutaka watu wakujazie comments Tu "NI KIJANA KIMWILI ILA KIFIKRA WE NI MZEE TENA KIKONGWE" Huna tofauti na mtoto aliyetoka kuachishwa kunyonya na mama yake

Mungu ndio ANAYATAKA HAYA?

#YNWA
 
Dogo usitafute sifa kupitia MUUMBA wako, kama nilivyokushauri hapo juu uvitazame na utafakari ni namna gani vingeweza kuwepo bila nguvu ya uumbaji na haujatilia maanani.

Kama tu ambavyo huwezi kuyageuza macho yako na kukitazama kisogo chako tambua pia fikra na akili zako zina ukomo, hivyo utakuwa sahihi sana kuamini uwepo wa MUNGU.

Kwanini watetezi wa Mungu mnaopenda kutumia vitisho ili mshinde hoja?

#YNWA
 
Mzee unadhani kila mtu anaishi kwa shemeji kama wewe? yaani nipoteze muda wangu kukuthibitishia kuwa wewe ni cha asubuhi, like seriously? nyie vijana falsafa zinawaharibu sana na sijui mnatoa wapi ujasiri wa aina hii.

Na mnapojificha ni hapo kwenye upuuzi wa thibitisha thibitisha, yaani nikuthibitishie kuwa wewe ni mwafrika na unajiona mwenyewe kwenye kioo ulivyo mweusi tii na pua kubwa ya kibantu, mkuu sina muda wa kupoteza wewe kama unaona hiyo picha ni ya mtoto wa mbuzi, fine.

Sasa si umwite Mungu ajitokezee Mwenyewe kuthibitisha...

Mungu yupo sawa, ila kwenye utetezi kwanini tunatumia nguvu nyingii kumtetea ilihali yeye mwenyewe yupo?

#YNWA
 
Sasa si umwite Mungu ajitokezee Mwenyewe kuthibitisha...

Mungu yupo sawa, ila kwenye utetezi kwanini tunatumia nguvu nyingii kumtetea ilihali yeye mwenyewe yupo?

#YNWA
Unadhani mungu ni gatusso sio, aje akujibu wewe mwana jamiiforums kuweni na adabu wazee, hakuja kuwajibu babu zenu tangu enzi ya nuhu ndio aje kujibu leo? hatowajibu na atakuja kuwauliza nyote ana kwa ana siku ya mwisho.
 
MUNGU anatetewa?

Unatakomaa kuthibitisha kuwa yupo "Unafanya nini?," Una " Prove his existence" unatetea uwepo wake.

Nadhani, ikifike wakati waislamu waache kubeba silaha ili kumtetea yeye na sheria zake.

Wakristo tuache kuchanganya madesa "Nani (kanisani gani) yupo sahihi?""

Ajitokeze mwenyewe AMALIZE KESI.

#YNWA
 
Unadhani mungu ni gatusso sio, aje akujibu wewe mwana jamiiforums kuweni na adabu wazee, hakuna kuwajibu babu zenu tangu enzi ya nuhu ndio aje kujibu leo? hatowajibu na atakuja kuwauliza yote ana kwa ana siku ya mwisho.

Ni kawaida yenu.

Huwa mnatumia vitisho kumaliza hoja zenu.

Kama serikali, ikiona mmezidi "Wanawatumia vitisho tu ili muogope"

Na hasa misikitini kumejaaa vitishoooo tu vya kifooo yaani ni full vitishoooo.

Haya nishaogopa NANYAMAZA.

#YNWA
 
Back
Top Bottom