Jambo liko hivi ili ukione wewe ndiyo kichwa mchunga yaani hufikirii juu ya mambo.
Mola alipo tuumba alitupa akili za kujua baya lipi na zuri lipi, lakini haikutosha akatuletea wajumbe wa kutukumbusha kutokana sisi wenyewe yaani wanaadamu wenzetu. Kisha tukaambiwa ukipenda shukuru ukipenda kufuru ila ukishukuru utapata kadha na kadha na ukikufuru utapata kadha na kadha. Huu ni uhuru kamili tena uhuru ambao uko wazi mno. Maana yake ukitenda wema unatenda kwa hiari yako na ukitenda uovu kadhalika unatenda kwa hiari yako.
Lakini katika hizo njia mbili, Mola wetu akawa ni mwingi wa kusamehe, pale unapokosea ukimuomba msamaha anakusamehe.
Swali la msingi kwanini uchague jambo ambalo ni baya na ushaambiwa ni baya ? Hii ni hiari yako kijana, sisi tutakuuliza kwanini usichague jambo jema na lipo na unaweza kufanya hivyo ? Hii ndiyo maana ya hiari. Wewe unapo zini ni kitu gani kinachokuzuia wewe usizini ?
Sasa hapa msukule ni wewe ambaye unahitimisha juu ya jambo usilo kuwa na Elimu nalo.