Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Kwahiyo mtoa mada umekimbia sababu ya vitisho uchwara vya hawa jamaa?
Hapana mkuu. Siwezi kutishwa na vitu vya kufikirika.
Nmeamua kuwa msomaji tu baada ya kuona nabishana na watu wapo brainwashed na wengine hawana hoja wanakimbilia kuni attack mimi binafsi. Nmeamua kuwaangalia tu
 
Nimesikitishwa sana na andiko hili kama unadhani Mungu anachunguzika kojoa ukalale.
 
Hapana mkuu. Siwezi kutishwa na vitu vya kufikirika.
Nmeamua kuwa msomaji tu baada ya kuona nabishana na watu wapo brainwashed na wengine hawana hoja wanakimbilia kuni attack mimi binafsi. Nmeamua kuwaangalia tu
Hapana.
Hautakiwi kukaa kimya kwasababu kuna wachache wanaoleta hoja unatakiwa kujibu hoja zao.
Ila yale mazombi mengine ambayo yamefilisika kihoja yanaishia kutoa vitisho uchwara na mipasho ya taarabu hayo yapeleke ignore list huko. Simple
 
Kutokujua uliumbwa na nani doesn't guarantee kwamba tuliumbwa na mungu.
Ishu ya Mungu ni Uongo... Je ulijiumba mwenyewe!? Mfano maji ni kitu muhimu sana kwa ajili ya uhai wetu.. Je haya maji uliyaleta WEWE(AU KIBURI TU NDUGU YANGU??)
 
Imagine unaambiwa eti umepewa uhuru wa kuchagua halafu ukichagua upande tofauti na mungu unaadhibiwa.Na bado watu wanakubali wana uhuru wa kuchagua!!
Watu kama hao napowaita misukule siwatukani.

Yani mtu ni mwanafunzi wa shule A, Mwalimu mkuu wa hiyo shule anatangaza kuwa kawapa uhuru wa kuchagua kati ya masomo ya sayansi na masomo ya uchumi lakini wajue kuwa atakaechagua masomo ya uchumi atafukuzwa shule!!

kwa anaependa uchumi na hapendi kufukuzwa shule atasema ana uhuru wa kuchagua?
Mfano umekaa vizuri sana
 
nashangaa kwannn hii thread ipo mpaka saiz ,una uzi ,ina tupa makwazo sana
 
Daah kazi IPO mungu sasa fanya jambo waamini kama upo....
 
Kama uamini nje ya sayansi utaelewaje
Ukishindwa kujua wapi kwa kuweka "h" napata mashaka juu ya uwezo wako wa kujadili mada kubwa zaidi.

Nakwambia hivi, huko nje ya sayansi jaribu kunielezea bila kutumia sayansi hata sehemu moja, tuone kama utaweza.
 
Imagine unaambiwa eti umepewa uhuru wa kuchagua halafu ukichagua upande tofauti na mungu unaadhibiwa.Na bado watu wanakubali wana uhuru wa kuchagua!!
Watu kama hao napowaita misukule siwatukani.
Jambo liko hivi ili ukione wewe ndiyo kichwa mchunga yaani hufikirii juu ya mambo.

Mola alipo tuumba alitupa akili za kujua baya lipi na zuri lipi, lakini haikutosha akatuletea wajumbe wa kutukumbusha kutokana sisi wenyewe yaani wanaadamu wenzetu. Kisha tukaambiwa ukipenda shukuru ukipenda kufuru ila ukishukuru utapata kadha na kadha na ukikufuru utapata kadha na kadha. Huu ni uhuru kamili tena uhuru ambao uko wazi mno. Maana yake ukitenda wema unatenda kwa hiari yako na ukitenda uovu kadhalika unatenda kwa hiari yako.

Lakini katika hizo njia mbili, Mola wetu akawa ni mwingi wa kusamehe, pale unapokosea ukimuomba msamaha anakusamehe.

Swali la msingi kwanini uchague jambo ambalo ni baya na ushaambiwa ni baya ? Hii ni hiari yako kijana, sisi tutakuuliza kwanini usichague jambo jema na lipo na unaweza kufanya hivyo ? Hii ndiyo maana ya hiari. Wewe unapo zini ni kitu gani kinachokuzuia wewe usizini ?

Sasa hapa msukule ni wewe ambaye unahitimisha juu ya jambo usilo kuwa na Elimu nalo.
 
Yani mtu ni mwanafunzi wa shule A, Mwalimu mkuu wa hiyo shule anatangaza kuwa kawapa uhuru wa kuchagua kati ya masomo ya sayansi na masomo ya uchumi lakini wajue kuwa atakaechagua masomo ya uchumi atafukuzwa shule!!
Ushajua Hilo na wewe ukichagua kinyume lazima ufukuzwe sababu umefanya hiari hali ya kuwa unajua mafikio yake ni wapi. Kijana huna akili, mambo yako wazi namna hii bado unashupaza shingo kwamba hakuna uhuru wa kuchagua ?
 
Yani kwenye huo mfano wangu, ni sawa na kusema hivi.
"Ama usome sayansi ama ufukuzwe shule"

Sasa vipi kama mimi sipendi masomo ya sayansi na sipendi kufukuzwa shule?

Nikichagua sayansi utasema nimechagua kwasababu ya uhuru wangu wa kuchagua?

Unajua nini maana ya uhuru wa kuchagua?

Ushakariri kulazimishwa kitu ni mpaka ushikiwe bunduki?
 
Jambo liko hivi ili ukione wewe ndiyo kichwa mchunga yaani hufikirii juu ya mambo.

Mola alipo tuumba alitupa akili za kujua baya lipi na zuri lipi, lakini haikutosha akatuletea wajumbe wa kutukumbusha kutokana sisi wenyewe yaani wanaadamu wenzetu. Kisha tukaambiwa ukipenda shukuru ukipenda kufuru ila ukishukuru utapata kadha na kadha na ukikufuru utapata kadha na kadha. Huu ni uhuru kamili tena uhuru ambao uko wazi mno. Maana yake ukitenda wema unatenda kwa hiari yako na ukitenda uovu kadhalika unatenda kwa hiari yako.

Lakini katika hizo njia mbili, Mola wetu akawa ni mwingi wa kusamehe, pale unapokosea ukimuomba msamaha anakusamehe.

Swali la msingi kwanini uchague jambo ambalo ni baya na ushaambiwa ni baya ? Hii ni hiari yako kijana, sisi tutakuuliza kwanini usichague jambo jema na lipo na unaweza kufanya hivyo ? Hii ndiyo maana ya hiari. Wewe unapo zini ni kitu gani kinachokuzuia wewe usizini ?

Sasa hapa msukule ni wewe ambaye unahitimisha juu ya jambo usilo kuwa na Elimu nalo.
Uislam bila uongo unakufa

Nani alikwambia mola Allah kakupa hiari?

Allah kapanga kila mtu kwamba atafanya Nini na mwisho wake kashapanga huna uhuru wa kubadili alicho panga

Nenda kasome dini Yako na uache mara moja kudanganya umma
 
Back
Top Bottom