M O N S T E R
JF-Expert Member
- Sep 26, 2022
- 2,818
- 8,465
Dini zote ni usanii, hizo references zote ulizoziambatanisha zimekuwa crafted na wasanii wabobezi wa enzi hizo. Imani hizo za vitu/mambo ya kubuni na kwa watu wenye upeo mdogo wa ku-analyze mambo.Dini zote iwe Christian au Islam ,budha,Shinto,Shiva, Buddhism, madhehebu yote uyajuayo hata ambayo yalikuwa hayajawa cult ,yote yamekuwa cult, Kuna mengine yamezidi sana ,mengine kiasi mengine kidogo,
Sababu Shetani aliahidi kabisa
ISAYA 14
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo
Hapo tunaona Shetani akiapa kwa MUNGU akisema"Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini."
UKISOMA
Zaburi 48
1 Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
2 Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
UTAONA PANDE ZA KASKAZI NDIPO LILIPOKUWEPO HEKALU PALE MLIMA SAYUNI NA NDIPO MAHALI PALIPOKUWA NA UWEPO WA MUNGU , HIVO SHETANI ALIAPA KUKAA NADNI YA MAKANISA KWA SIKU ZETU AMBAPO TUNAKUSANYIKA TUKIAMINI TUNAMUABUDU MUNGU
Tuanze mada yetu sasa, fatana nami....
Katika FREEMASON Degree ya 33 ( hii ndio hatua ya juu ya Fremason kwa ujumla Duniani, huitwa"Degree of the Craft", na mwanachama mwenye Degree 3, anaitwa Mastermasonry/Grand master, hawa ndio wapangaji wa mipango, hawa ndio wanao jua siri ya free masoni na hii degree unaipatia katika Blue Lodge.
Freemason, imegawanyika katika Vyama mbali mbali lakini vyote hujulikana kwa jina la freemason, na kila chama kina jiendesha kwa misingi yake, mfano York rite na scottish rite.
York rite, hii inapatikana marekani katika lodge za huko, na katika york rite , wao waliongeza degree 10, za ziada, lakini huwezi kupata hizi degree bila kuwa na degree tatu , ambazo ndio msingi wa freemason Duniani kwote..na katika York rite degree ya 10, na maanisha ya 13, ukijumlisha na zile degree tatu za msingi, hiyo ni hatua ya juu ambayo inaitwa the Order of the Temple, na mwanachama mwenye degree hizi anaitwa "Knight templar".
Katika Scottish rite, katika chama cha scotiland, kupitia Lodge zao, wao waliongeza Degree 30, na kuzifanya ziwe 33, na huwezi kupata hizi degree bila kuwa na degree 3, za msingi. katika hizi degre, degree ya 32, ndio degree ya juu kabisa ambayo mwana chama mwenye hatua hii anakuwa Master of the royal secreat, siri zote za freemason unapewa.
Japo katika scottish rite , kuna jumla ya degree 33, lakini freemason wana amini degree ya 33, haipo, kwasababu ni adimu sana , labda mtu mwenye IQ, kubwa kama 160, na kama wapo basi wana fahamika na freemasoni wenye degree za juu kabisa.
wapo watu wanao amini labda hii degree ya 33, hii ndio degree inayo muhusu Lucifer.. pia baadhi wana amini Albert pike, mwandishi wa kitabu cha "Morals and dogma" alikuwa na degree 33, lakini wapo ambao wana amini hakufikia hatua hiyo.
Freemason ni chama ambacho kina daiwa kuwa na mambo ya siri mengi, na hawa inasemekana wanachama wake wengi wenye degree za juu , wapo katika chama cha Illuminat.
Unaweza kuona aina za digrii hizo; kwa mfano digrii ya 18 inayoitwa ‘Knight of Rose Croix’ hushughulika na elimu ya aina za misalaba na jinsi ya kufanisha kuziingiza ndani ya taasisi na madhehebu mbalimbali kwa imani ya Illuminati na freemason na kwa kweli freemason wa digrii hiyo wamefanikiwa kwa kiwango cha juu kabisa kuingiza aina nyingizi za misalaba ndani ya makanisa na taasisi bila ya waumini kujua maana ya misalaba hiyo.
Ukatoliki ni Cult, uislamu ni cult,kumbuka uislamu umeanzishwa na Ukatoliki
Kina martin Luther,John Knox,Isack Newton, John Zwingil, na wengine wengi waliondoka ndani ya Ukatoliki ili kusafisha au kufanya matengenezo,matokeo yake walipokufa na wao Freemason na illuminati wameteka hayo madhehebu
Hapa nitakuonesha baadhi ya madhehebu na jinsi yalivyoingiliwa , soon nitaandika kitabu kuelezea kila dhehebu jinsi ma freemason walivyoingia
Brethen Assemblies: Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na familia ya freemasons.
Makanisa ya Kipentekoste au kilokole: Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya kilokole kama kina mwamposa. Kwa wakati huu nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!
Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.
Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.
Seventh –Day Advetist Church: Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya “Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye kanisa hilo likawa chini ya rais wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani. Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na ‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na kazi yake.
Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la ‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba kanisa hilo limeingiliwa na freemasons.
Wengi wa waumini wa SDA waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’ mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA kwa sababu,
tukio kubwa ikiwa ni freemason kuingiza nembo yao,huku wakiiondoa ile nembo ya UJUMBE WA MALAIKA WATATU,Freemeson huingiza mafundisho, au alama zao kupitia viongozi wa juu wa kanisa kama ilivyo kawaida ya makanisa yote uyajuayo.
Leo ngoja niishie hapa
Brainwashing at it's highest level.