ni rahisi sana. chukua kitabu cha Matendo ya mitume, kisome chote mara tano hivi. inaweza kuchukua muda, halafu jifunze kanisa la kwanza lilikuwaje, fuata hayo. ila kukusaidia tu, vitu vya msingi ili kujua kuwa kanisa fulani ni kikundi cha wanadamu kinachoweza kukusaidia umtafute na kumwona Mungu, zingatia haya;
1. wanahubiri wokovu.kwa maana ya kwamba, mtu amkiri na kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake kwa kumaanisha kuacha dhambi. na katika hili, sabato, katholic, jehova na hao wanaohubiri miujiza na kuuza maji badala ya kuokoka na kuukulia wokovu, ni cults.
2. angalia kama wanahubiri umuhimu wa ujazo wa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha. Yesu Kristo alituambia wazi kwamba, Roho Mtakatifu ndiye atatuongoza na kututia kwenye kweli yote. kinachotutia kwenye kweli yote sio katekisimo, liturgia nzuri au mapokeo ya dhehebu, au kukariri Biblia. ndio maana sote tunatumia Biblia na wengine kama ndugu zangu wasabato na mashahidi wa jehova wanaweza kumeza Bible nzima kichwani lakini haipo moyoni na hawana Mungu. ni kwa sababu wanamkosa Roho Mtakatifu na hawataki kujazwa, wanasema ni mapepo na sio muhimu kwa sasa. Yesu alisema wanafunzi wasiondoke Yerusalemu hadi wampokee huyo kwani ndio Nguvu. Petro aliyekuwa mvuvi tu, asiye na elimu, aliyekuwa mgomvi hadi siku Yesu anakamatwa alikata mtu sikio, alipojazwa Roho Mtakatifu kule gorofani, alihubiri mno na watu wakamshangaa maana sio yule waliyemzoea. watu waliuliza tufanyeje sasa ili tupate icho kipawa tuwe kama wewe? Petro akasema tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina lake Yesu mpate ondoleo la dhambi nanyi mtapata kipawa cha Roho Mtakatifu, maana ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu na wote watakaomjia Bwana. Kumbe hii ni ahadi kwa sisi sote, sio kwa wachache tu kama waalimu wenu wanavyowafundisha. kwa hiyo ukienda kwenye kanisa ukaona mwezi mzima hawajafundisha umuhimu wa ujazo wa Roho Mtakatifu na hakuna madhihirisho yake, kimbia, hapo hapakusaidii. na kwa maana hiyo, madhehebu kama wasabato, wayehova, wakatoliki, walutheran (ukiondoa kwa mbali fellowship), anglican, moravian etc ambao hawahimizi icho kitu, wanatembea bila Roho, na kinabakia kikundi fulani tu cha fanatics au waabudu dini.
3. angalia, wanahubiri toba na utakatifu au la. kama jibu ni hapana kimbia. Kanisa la kwanza hata kama waliponya wagonjwa, walifufua wafu, walifanya chochote, msisitizo haukuwa kwenye mali na mambo ya dunia hii. msisitizo mkuu ulikuwa ni UTAKATIFU. walikuwa wanakemea dhambi, sio siku hizi wamekuja watu wanajiita watu wa imani ya neema. wao wanaamini ukishamkiri Yesu tu unakuwa umeshaweka maisha yako mikononi mwa Yesu, hata ukitenda dhambi Yesu anaziondoa automatically. hawajui kuwa, Neema inayoongelewa hapa ni neema ya kufuta dhambi na kukukomboa tena. Mfano; ukishaokoka ukatenda dhambi, haiondoki bila kuitubia, usipotubu itakutafuna na kukuondoa kwenye uso wa Mungu. zamani ukitenda dhambi ulikuwa unagarimia binafsi kwa kuchinja mnyama, maana ya neema ni kwamba Yesu anakulipia deni la dhambi hiyo husika, sio dhambi zote zingine. Neema haipo ili tuendelee kutenda dhambi. hivyo ukiona kuna kikundi cha watu hawahubiri utakatifu wao ni mafanikio tuuu, kimbia hapo. hata kufanikiwa kwenyewe hautafanikiwa.
4. waangalie wachungaji, ukiona wanajipenda sana, wanavaa sana, masharobaro, kimbia hapo. watakuambia ukiokoka haimaanishi usiwe smart. kuna usmart, ila kuna usharobaro ambao hauwezi kuutofautisha na dunia hii. wala msiifuatishe namna ya dunia hii ndugu zangu, hayo yote yanapita.
5. Kiburi, ukiona wachungaji wana kiburi, kimbia hapo. wengi wa wachungaji wa uongo, utakuta waumini maskini, ila wao ni matajiri wakubwa na wana viburi vya pesa mno, wanaongea kwa dharau, midomo yao imejaa kulaani badala ya kubariki, wanapenda kuinuliwa, wanazunguka na mabodigadi rundo (though sio wote wenye bodigadi ni wa uongo), hawa hawana tofauti na kina hamonize wanavyozungukwa na mabodigadi, wanapenda kusifiwa, kutukuzwa wao badala yakumtukuza Mungu.
6. Jambo kubwa, ni CONTROL. ukiona mchungaji anawacontrol waumini kupita maelezo, anawatishia wasiposikiliza anachosema watapata madhara, kimbia hapo. hii ni kwa sababu mchungaji pia ni mwanadamu, ana madhaifu, na kuna wakati huwa anaweza kusaidiwa na waumini wake kurudi kwenye njia. manabii wa uongo wengi ni wakali mno kimwili, wanalazimisha ufuate wanachotaka, usipofuata wanakutishia hautabarikiwa au utakufa au utapata madhara fulani au Mungu atakuua n.k. kwa njia hiyo wamepora pesa sana, na wamelala sana na wanawake wadhaifu, na hata ukijua siri zao chafu wanasema unatakiwa kuwafunika kama watoto wa Nuhu walivyofunika uchi wa baba yao hawakulaaniwa. hawa ni watu hatari sana. yaani yeye pale anajiweka kama ndio malaika wa hapa duniani, mtakatifu kuliko ninyi nyote, anayepokea moja kwa moja toka kwa Mungu, ninyi wengine hamwezi kupokea, kila kitu lazima kipitie kwake. KIMBIA HAPO. Mchungaji halisi ni yule anakufundishe Neno ujitegemee, usimtegemee yeye kudownload toka kwa Mungu, sasa hawa wa uongo wanakuweka kwenye position kwamba, bial wao hauwezi fika popote na hautasikia toka kwa Mungu maana wao ndio njia.
7. mahubiri yao hayana uwepo wa Mungu. ndugu zangu, Mungu ni dhahiri, na giza ni dhahiri. mtu huwezi kuwa wa gizani ukatoa kinywani mwako yale ya nuru, na huwezi kuwa wa nuru ukatoa ya giza. uwepo wa Mungu umejitenga kabisa na uwepo wa kipepo. wengi wa wahubiri wa uongo, wanahubiri kwa kutumia akili na theolojia, hakuna uvuvio wa Roho Mtakatifu, na popote pasipokuwepo Roho, hapana wokovu. ni Roho Mtakatifu huwa anagusa moyo, sio maneno yako ya ujanja au uzoefu.
8. wanakuambia "madhabahu yangu ndio imekuponya", au mungu wangu amekuponya, badala ya kumtukuza Yesu moja kwa moja. wengine huwa wamechukua upako kwenye madhabahu fulani, na utasikia watu kwenye ushuhuda wanamwambia "madhabahu ya ...........ina nguvu", ni madhabahu gani? ya Mungu au ya mungu wao, maana kuna miungu mingi duniani lakini aliye MKuu ni mmoja tu, Mungu wa Ibrahim Isaka na yakobo. madhabahu ya siloam, madhabahu ya kanisa la baba mungu, madhabahu ya mwamposa, madhabahu ya ngurumo, madhabahu ya kuhani, madhabahu sijui ya nani, hao wote jiulize, ni madhabahu gani hiyo tofauti na Jina la Yesu? na wao wanapenda useme hivyo. kwanini wasiseme tu Yesu Kristo ameniponya, au Jina la Yesu Kristo limeniponya, kwanini wanataka utukuze madhabahu yao badala ya Jina la Yesu?
ALL IN ALL, ukiona mchungaji sharobaro, kama hao manabii wa uongo, sometimes wala usiende hata kuuliza kwa watu, KIMBIA, anapata wapi muda wa kuomba na kumtafuta Mungu na