Unakabiliana vipi na waumini wanaolazimisha salamu za kiimani bila kujuwa imani ya mtu mwingine

Unakabiliana vipi na waumini wanaolazimisha salamu za kiimani bila kujuwa imani ya mtu mwingine

Asalam Alaykum warhamtullah wabarakatuh.
Maana yake ni "Amani iwe juu yako na rehema za Mungu na baraka zake".

Haifai kumuombea rehema mtu asie amini uwepo wa Mungu au kuwa Mungu ni mmoja na yeye tu ndo anapaswa kuombwa na kuabudiwa kwa jina lake.

Wengine wanaomba kwa majina ya viumbe kwahiyo salam hiyo ya Amani ni strictly prohibited kwa asiekua muislam.
Lucha we ni mtu safi sana..
Ukija kwenye ishu za dini uwa nainjoi comment zako mkuu
 
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Ndo naona ushamba wa watanznaia mtu anaamini dini yake ni universal na amna din nyingine na anakushangaa kwa nini upo kwenye hilo dhehebu
 
Huku mtaani kuna baadhi ya watu ukikutana nao hata kama hamjuwani unakuta mtu analazimisha kukusalimu kwa salamu ya imani yake.

Jambo ambalo wakati mwingine linakuwa kama kero.

Ukisalimu mtu kwa salamu ya kiimani hakikisha unajuwa imani ya mtu huyo ili wakati mwingine kupunguza kumkwaza mtu.

Mimi binafsi huwa siitikii salamu ya kiimani, anayejipendekeza kusalimu kiimani awe mzee, kijana, mwanamke, mwanaume mimi naitikia "POA". JE wewe unakabiliana vipi na mazingira kama hayo.
Sema wengi kwenye hawajui maana yake halisi ya hio salaam. (yaani tafsiri yake) Ndio maana wengi wanakwazika, ila mimi binafsi huwa sina shida yoyote. Naitikia tu kwakuwa nilisha jifunza tafsiri ya salamu hizo.
 
Mimi huwa sijibu kabisa.
Maana unaweza kujibu majibu ambayo sio ukaonekana mbaya au una dharau dini za watu.
 
Back
Top Bottom