Unakubaliana na Boateng kuhusu Ronaldinho?

Unakubaliana na Boateng kuhusu Ronaldinho?

Gaucho namna nyingine hajapatatokea mwingine nakumbuka kuna mechi na Chelsea jamaa alitingisha kiuno nje ya 18 katikati ya mabeki 4 na kufunga jamaa ni kufuru
 
Ndio mchezaji pekee wa Barcelona ambaye aliifunga Real Madrid na mashabiki wa Real Madrid wakasimama kumpigia makofi aaaah Bravo Gaucho
 
Mkitaka ushuhuda mwengine unaofanana na wa Jerome mtafuteni Ashley Cole juu ya madhira aliyokumbana nayo wakati wa World Cup 1994 quater final, alitenguliwa nyonga hakurudi tena uwanjani. Mpira ulikuwa ukimuona Gaucho ulikuwa unamtii kama vile Mbwa amwonapo chatu.
Hii si kweli
 
Ndio mchezaji pekee wa Barcelona ambaye aliifunga Real Madrid na mashabiki wa Real Madrid wakasimama kumpigia makofi aaaah Bravo Gaucho
Ilikua nov 2005 el classico santiago ambapo kama sikosei madrid ilikua na watu wenye majina makubwa sana kina beckam nk.

Ronaldinho aliwapiga goli mbili kama wamesimama, ilikua haijawahikutokea mchezaji wa timu pinzani kupokea heshima ya standing ovation pale madrid kwa miaka mingi toka kwa mashabiki lakini walilazimika kumfanyia Dinho.

Hiyo ilikua kuwaonyesha madrid kua rais wao alifanya kosa kwa kutokumnunua yeye akakimbilia kumnunua beckam, maana wote walikua kwenye rada zake mwisho akaakua kumnunua beckam nabarca wakamchukua Ronie.

Ronie alikua akicheza soka hata mbinguni inakua ni siku ya mapumziko.
 
Mkitaka ushuhuda mwengine unaofanana na wa Jerome mtafuteni Ashley Cole juu ya madhira aliyokumbana nayo wakati wa World Cup 1994 quater final, alitenguliwa nyonga hakurudi tena uwanjani. Mpira ulikuwa ukimuona Gaucho ulikuwa unamtii kama vile Mbwa amwonapo chatu.
Duh!! Bro hiz ni fix za 1st class world cup 1994 quarter final.. Hao wote walikuwa mavi matupu.. Mtu pekee alienda km kijana alikuwa ronaldo de lima.
 
A best footballer he ever played with... Sawa
Lakin hao wengine hajacheza nao si maradona,wala pele... Hata zidane tu nna hofu hajacheza nae..

Japo namuheshim gaucho
 
lol! hahahahahah....Mie Mkuu mpaka leo hii huwa nakaa kwenye utube masaa hata mawili naangalia video zake, jamaa mwache aende zake, GAUCHO hana mfanowe.

Ronaldinho alikua akicheza mpira hata malaika wanacha kazi zao wanamuangalia na kushangilia huko mbinguni.

Alizaliwa kucheza mpira na kuuchezea mpira. Hata mpira ulipokua ukifika miguuni kwa Dinho ulikua unajua umefika nyumbani.
 
Mkitaka ushuhuda mwengine unaofanana na wa Jerome mtafuteni Ashley Cole juu ya madhira aliyokumbana nayo wakati wa World Cup 1994 quater final, alitenguliwa nyonga hakurudi tena uwanjani. Mpira ulikuwa ukimuona Gaucho ulikuwa unamtii kama vile Mbwa amwonapo chatu.
Wacha uongo ni 2002.
 
Huyu anatutungia hadithi..
Halafu badae anasema ilikuwa 98 .Mwanzo nilimchukulia kakosea bahati mbaya ila baadae nikajiridhisha kuwa hamjui hata huyo Ronaldinho.Hakumuona akicheza anamuona kwenye clips tu.

Sijui ni kwa nini mtu unataka kujadili vitu usivyovijua kabisa.Halafu kama mtu ameweza kuingia JF anashindwa nini hata kugugo tu apate kwanza uelewa hata mdogo tu ndo achangie?

Tabia hii kwakweli ya watu kupenda mijadala na kuchukia kujisomea inakera sana.Tupende kujisomea ndugu watanzania angalau tupate introduction ya kinachojadiliwa kuliko kujidhalilisha.
 
Nadhani ufike wakati tufunge mjadala kuhusu uwezo wa huyu jamaa tuanze kuwajadili wanaomkaribia. Alikuwa na kila kitu unachohitaji kukipata kwa football player
 
Mkitaka ushuhuda mwengine unaofanana na wa Jerome mtafuteni Ashley Cole juu ya madhira aliyokumbana nayo wakati wa World Cup 1994 quater final, alitenguliwa nyonga hakurudi tena uwanjani. Mpira ulikuwa ukimuona Gaucho ulikuwa unamtii kama vile Mbwa amwonapo chatu.
Acha uongo kaka au rudi kachek kumbukumbu zako upya.
Ni kwamba,world cup ya kwanza kwa Ashley Cole ni ya mwaka 2006 kule ujeruman ambako England ilitolewa na Portugal, kumbuka ugomvi wa Rooney na Ronaldo.

Halafu world cup ya kwanza kwa Gaucho ni ya mwaka 2002 pale Japan,

kumbuka ugomvi wa Scolari na mashabiki kule Brazil, mashabiki wanataka Romario na Edmundo waitwe lkn Scolari akasema "hao watu wenu siwaiti na nisiporudi na kombe basi niuawe" nafikiri mnakumbuka zile 4 R zilivyofanya mambo,

Ronaldo de Lima,Rivaldo,Robarto Carlos na Ronaldinho from Gaucho walikuwa on fire.

Fainali ujerumani anakufa 2-0
 
Back
Top Bottom