Unakuja unanipita hujanisalimia, unakwama halafu unataka nikusaidie

Unakuja unanipita hujanisalimia, unakwama halafu unataka nikusaidie

Hujaelewa
Yaheee hao wajinga sana haoo ...yaani wakupita tu weyeee kama πŸ’₯nyuma 🌈πŸ’₯ awajakuona weyeee...yeyeee wanunie tu 😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Hata mimi nikimkosa niliyemfuata na sikusalimia nliokuwata huwa nasepa taratibu. Najua Wahafidhina wanakuwa wako standby nijichanganye niulize wanipe za uso.

"Mbongo anamaindi mambo madogo"

Darassa - Too Nuch
Na wanavyokiwaga makini kukuskilizia kama utaulizaπŸ˜„πŸ˜„,.

Ila sema salamu muhimu mkuu, tujirekebishe
 
Tumia akili wewe mpumbavu kwani kusalimia kuna kanuni ya nani aanze au nikupe visa vyangu binafsi nikuonyeshe upumbavu wenu nyinyi mnao lilia salamu ...kwanza mjue kuna tofauti ya kutokusalimiana na kuto kuitikia salamu ...wewe hapo kama umekutana na mtu ajakusalimia basi wewe ulishindwa nini kumsalimia yeye kwanza ? Mngekuwa mnalahumu mtu kutokuitikia salamu sawa ....sikumoja nilikuwa natembea nikakutana na jamaa akaniambia mbona usalimii nikamjibu kuwa mbona na yeye asalimii ...kisha nikamuuliza kwani kusalimiq ni lazima mimi nianze?...hivyo huyo aliye kupita bila ya kusalimia na wewe ukumsalimia basi nyinyi amkusalimiana hakuna mwenye haki la kumlaumu mwingine. Jobless_Billionaire
Sasa hapa ni London?
 
Mara nyingi ni wanawake ndo walio na hiyo tabia
Najua mtoa mada amemind kwa sababu amepona mwanamke huyo ni kama amemdharau hivi

Me mtu wa hivo HUWA simjibu ntabaki namuangalia tu afu nasepa zanguu
Daah! Tunao mtaani huku. Kitongoji kimoja lkn ustaarabu 'F' mbaya zaidi tunakutana mambo ya kijamii e.g msiba, sherehe n.k matokeo yake ni kutazamana tu. Wanawake wachache wakikukuta watakusalimia wengine sielewi huwa wana mtazamo gani.
NB: salamu ndio chanzo cha uhusiano mwema ktk jamii iliyostaaraibika. Unaweza salimia tu na tusijuane, which is good pia.
 
Wakuu salama?

Kuna watu ni wa ajabu sana. Sijui wanajikutaga akina nani vile. Unakuta jitu limekuja sehemu aidha dukani au popote pale, limekukuta likakupita tu. Limemkosa linaemtafuta halafu linarudi kukuuliza fulani yuko wapi?

Au limekwama huko limepotea njia ndio linajirudisha kuomba msaada ulielekeze.

Jitu linakuja linakukuta may be upo kwa mtu linaemtafuta, bahati mbaya katoka kidogo umebaki wewe. Halisalimii linafikia kumuangaza mhusika linamkosa, linarudi kukuuliza fulani yuko wapi.. Unagongwa nini? 😑😑😑

Sijajua nyie reaction yenu huwa ikoje, ila mimi sitakagi ujinga. Ukinikuta mazingira fulani ukaacha kutoa salamu hakikisha hautahitaji msaada kwangu. Naweza nikakushushia vinu (matusi) hujawahi kutana navyo. Huwa natafsiri ni kama dharau.

Salamu hufanya hata mtu kuwa mkarimu kwako pale unapohitaji msaada wa jambo fulani, utakuwa umeonyesha uungwana. Ila uje race tu kama vile unayapita mawe, utakubali.

You have got a very little understanding about human pyschology.

Mtu anaepita bila kusalimia watu tafsiri Yake ni kwamba ana pitia kipindi kigumu kwenye maisha Yake ana mambo mengi kichwani.

Next time usikatae kumpa msaada mtu aliekupita bila kukusalimia Kwa sababu utaonekana mshamba au mtu mwenye ubongo mdogo au vyote Kwa pamoja
 
Mkuu mjini mambo mengi muda mchache...... vitu ni vigumu kama ukitaka viwe vigumu.
Kwamba wewe ukitoka nyumbani kwako kila unayekutana naye popote pale unatoa salamu?...... aisee si utawehuka?

Na huo muda wa kuanza kukariri ni stranger gani hajanisalimia ili uje kum mind akikuuliza unautoa wapi mkuu?
Take it easy

Hizi ni ATHARI za UJIMA(ujamaa) nilikutana nazo sana nilipokwenda kijijini maana kijijini watu wote ni kama ndugu wanajuana wote so salamu ni LAZIMA
Usiposalimia unawekewa vikao kabisa na mwenyekiti.
Mjini watu wako race mkuu.
Mtoa Mada atakuwa anaishi mkoani na amekulia kijijini
 
KIONNGOZI; Mtu anakupita zake na boda, Bajaji au hata gari anapotea anarudi kukuuliza; Ulitaka akipita asimame akusalimia ndio apite?
Saidia watu kama unaweza maisha yamebadilika......
Mkuu huenda sijaeleweka vyema. Nilichomaanisha ni kwamba, may be nilikuja kwako kama mgeni. Labda tumekaa nje kidogo ukatoka nikabaki mwenyewe. Kaja mtu anaekufahamu, kanipita nje kapitiliza kukuita. Baada ya kuona harespond ndio arudi kwangu aniulize. Kibaya zaidi bila kusalimia tena. This is what I intended to mean na sio wapita njia. Sio issue kwangu hao sababu you can't consider everyone.
 
Ilinitokea hii πŸ˜…πŸ˜…πŸ™ŒπŸΌnilienda kwa rafiki yangu na tulikuwa tumetoka kuwasiliana muda mchache tu, akaniambia yupo.

Mimi na kiherehere changu nikapitiliza bila kusalimia ile nafungua mlango umefungwa Kumbe katoka kidogo πŸ˜œπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…nilipata aibu ya kimataifa.

Nilijifunza siku nyingine nitasalimia nipate msaada.
 
Back
Top Bottom