Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Alikuwa anaongea na simu huku akifoka.. nikamuuliza vipi mama unaongea na nani mbona unamfokea ivo akaniambia ni mtu wangu wa zamani bado ananililia lia hapa.. nikasema duu.. akajibu..

" wakati wake ulishapita , sahizi ni wakati wako bhana, ukitoka wewe utakuja wakati wa mwingine pia , ndo maisha yenyewe"..
Nilidhani nishasikia kila kitu humu dunian[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
'' kunihudumia unanihudumia, kunijali unanijali lakini najikuta sikupendi tu ujiongeze na wewe" ...hii kauli sitaisahau niliamua kusepa kimya kimya mwisho akianza kunitafuta nikamwambia na Mimi nimejikuta tu simpendi, Hadi Leo anajifanya rafiki namimi namchora tu.
pole Sana mkuu
 
" Aisse, mama pendo na mme wake ndio wanakula laifu, sisi wengine ni wasindikizaji tu " Hilo nilirushiwa na bidada kipindi ndio Kwanza tuna anza anza maisha...!!! sikumsemesha kwa pale, ila siku ya pili katoka kwenye mishe zake akakuta kitasa kipya, aliponipigia simu nikamwambia atizame kwenye simu nimemtumia hela ya nauli ya kwao, na mabegi nimeshayatanguliza na basi. Kisha nikabadilisha laini na kuhama mtaa kwa miezi minne. Nilipomrudisha na kumueleza kosa lake, alibaki anashangaa tu, ila ninaishi nae mpaka sasa, watoto 3, nikikohoa tu, anaruka, Na akitaka kuongea anaomba ruhusa, Kisha anaongea taratibu kwa kuchagua maneno...[emoji41][emoji41][emoji41] !!!!
Wewe ni miongoni mwa wanaume wachache waliobakia

Nilikuwa nasoma comments za wadau humu nikawa bado sipati picha ni mazingira gani hadi mwanamke anijibu hivo
 
Kuna binti flani nilikua na date nae kipindi nipo chuo hapa mjini. Huyu binti sijui ni usichana mwingi, u much know sana, sijui ndio alikua ame hit peak yake au lah.

Alikua anapenda sana matusi ya reja reja. Leo akwambie acha usenge bhasi, mara upo slow sana, acha uboya na mengineyo mengi. Ila on top ni hili "**** you boy". Alinambia mara ya kwanza nikamkanya hakusikia.

Aliporudia mara ya pili, nikasema acha iwe. Mwanaume nikapiga chini. Cha ajabu sasa alinililia sana. Mno mpaka kunitishia amebeba ujauzito wangu, mpaka nikabaki nashangaa sasa matashtiti yots yale yalikua ya nini.
😂😂
 
Back
Top Bottom